Wimbo wa Hainaga ushemeji umenishangaza

Wimbo wa Hainaga ushemeji umenishangaza

Hainaga ushemeji ya ManFongo ni wimbo uliobamba sana kwenye hizi nyakati za Tanzania ya wazinzi. Cha ajabu nilikuwa nasikilizaga chorus tu sijawahi kuconcentrate kusikiliza verse zake, jana wakati nimetulia napata moja moto moja baridi nikawa nasikiliza mstari mmoja baada ya mwingine, nikashangaa sana kumbe verse na chorus havina mahusiano kabisa.

Kwenye chorus anazungumzia kitu kingine, verse vitu vingine sasa nikajiuliza huu wimbo umetambaje na kwanini watu wengi wamekomalia kwenye chorus tu au ndo mwisho wetu wa kufikiri ulipoishia? Maana nilichogundua tukiuliza watu 10 waliousikiliza wimbo huo uenda ni mtu mmoja tu anaweza akawa ameelewa verse zinazungumzia nini.

Alichokifanya ManFongo ni kama kwenye kichwa cha habari cha gazeti kiandikwe kuhusu Tetemeko la Kagera halafu kwenye content waelezee kuhusu msambwanda wa Wema Sepetu.
Ndo wasanii wetu walivo....kuna wanaobana pua had husikii anaimba nn..wengine wanakusanya maneno yasiyo na maana ilimrad kupata rhyme...tunasikia chorus au labda na hizo bits..wabongo fleva wabadilike sasa..wafate kanuni za uimbaji!!!
 
Mimi pia huwa nasikia kelele tu, sasa nikiona vijana wanavyowehuka na huo wimbo ndio naamini kweli nishazeeka!

Ha ha ha, uzee tayari mkuu.

Siku moja niko home mwanangu wa miaka 5 anaimba wimbo siuelewi, kuuliza nikaambiwa ni Chafu Pozi, ikabidi niingie youtube ndo kuuona wimbo.

Uzee haupigi hodi mkuu.
 
Back
Top Bottom