Wimbo wa King Kaka wa Wajinga nyinyi!!! (Kenya)

Afrika ni Afrika tu, Kenya haipo Ulaya. Soma hii: Kwa nini mwanamuziki huyu wa Kenya anataka ulinzi?

Kuna tofauti kubwa sana usitufananishe na jinsi mlivyo, huyu msanii angekua Bongo kwa sasa yangekua tayari yamemtendekea, hapa anaomba ulinzi kwa kuogopa ogopa mwenyewe tu ila hamna chochote kimemtendekea.
Huko Bongo nilisoma eti msanii anakamatwa kisa kamtakia rais heri njema ya siku ya kuzaliwa huku akitumia picha ya rais.

Mko bado sana hata kuwaza kujifananisha na Kenya, kwanza desturi yenu nyie ni waoga waoga sana, ukitaka kujua mlivyo waoga, muulize Mange Kimambi alivyo achwa mwenyewe.
Hapa Kenya sisi ni full mzuka...fireee....waambie wamguse huyu msanii uone mziki wenyewe wa Kikenya.
 
Haha! tatizo lako unasoma sana habari za udaku. Alikamatwa, then what happened?... By the way, umesikia jinsi gavana Mutua anavyolialia?...
 
Kwamba tu alizinguliwa na dola kisa kamtakia heri njema rais kwa kutumia picha, hilo limetosha kuonyesha mlivyo.
Kwetu hapa hatuvumilii upumbavu wa kihivyo maana ilitu-cost sana kuupata huu uhuru tulionao.
Mimi hapa ni shabiki wa hii serikali, wakitenda mema huwa nawashabikia, na pia ni mzalendo wa nchi hii, ila wakizingua huwa sikawii kuwabadilikia, sio kama nyie unakuta mtu wa CCM anashaikia Lissu kulishwa risasi 38.

Haya makelele baina ya Mutua na Ruto ni ya kawaida kuelekea 2022, ndio kama hayo nayaona huko ya Membe, kawaida ikikaribia uchaguzi utayaskia.
 
Hawa bado wako stone age. Wachana nao.
Wakati Alfred Mutua akitishiwa na naibu rais uso kwa uso kwasababu ya kutoa maoni yake, wakati Jacob Juma akiuliwa kwasababu ya kuekeza ukweli juu ya serikali ya Jubilee, Miguna Miguna akifurushwa nchini kinyume cha sheria na kudharauliwa amri ya MAHAKAMA iliyotaka arudishwe nchini, mwanamuziki King Kaka ameanza kupokea vitisho sawa na Alfred Mutua, toka vyombo vya usalama, huku Waiguru akitishia kumpeleka kotini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwamba tu alizinguliwa na dola kisa kamtakia heri njema rais kwa kutumia picha, hilo limetosha kuonyesha mlivyo.
Kwetu hapa hatuvumilii upumbavu wa kihivyo maana ilitu-cost sana kuupata huu uhuru tulionao.
Mimi hapa ni shabiki wa hii serikali, wakitenda mema huwa nawashabikia, na pia ni mzalendo wa nchi hii, ila wakizingua huwa sikawii kuwabadilikia, sio kama nyie unakuta mtu wa CCM anashaikia Lissu kulishwa risasi 38.

Haya makelele baina ya Mutua na Ruto ni ya kawaida kuelekea 2022, ndio kama hayo nayaona huko ya Membe, kawaida ikikaribia uchaguzi utayaskia.
Wala si vyombo vya dola vilivyomsumbua ila tatizo ni huyu bosi wa Dar es Salaam (na wenziwe wachache) anadhani nchi inaongozwa kwa matamko na amri (badala ya sheria), hata hivyo, naona siku hizi Mkuu wa Kaya anampotezea. Kwenye suala la Lissu, mmh, wala sina usemi...
 
Sasa nini kinasababisha mkulu ashindwe kufanya maamuzi magumu kwa Bashite, ama tumbua tumbua huwa kwa vidagaa tu, ila papa wanaachwa wanapeta bila bughudha.
Kuna video niliona mkulu anampuuza kwenye salamu......
 
Eti inasemwa kuwa Mkulu analipa fadhila maana wakati wa kampeni za urais 2015 Bashite alimwokoa na kifo baada ya kumtonya kuwa asitumie helkopta iliyopadaliwa kwani ilikuwa imetegeshwa ili imuue (inasemwa kuwa hakuwa chaguo la wenye chama chao), badala yake helkopta hiyo ikaishia kumuua Mbunge wa Ludewa ambaye (pia inasemwa) aliandaliwa kuwa Waziri Mkuu. Hata hivyo hizi zitabaki kuwa tetesi tu...

Kila nikiyafikiria mambo kama haya (plus yale yanayowakuta kina Lissu) ndiyo maana naichukia siasa...
 
Inasemwa kuwa Mkulu analipa fadhila maana wakati wa kampeni za urais 2015 Bashite alimwokoa na kifo baada ya kumtonya kuwa asitumie helkopta iliyopadaliwa kwani ilikuwa imetegeshwa ili imuue (inasemwa kuwa hakuwa chaguo la wenye chama chao), badala yake helkopta hiyo ikaishia kumuua Mbunge wa Ludewa ambaye (pia inasemwa) aliandaliwa kuwa Waziri Mkuu...

Kila nikiyafikiria mambo kama haya (plus yale yanayowakuta kina Lissu) ndiyo maana naichukia siasa...

Hehehe!! Ndio hayo hayo ya siasa, ukiamua kuyafuatilia ukubali presha na msongo wa mawazo, mimi kwetu Kenya nilikua napenda sana siasa, kwanza nilikua mmojawapo wa viongozi kwenye vuguvugu la Bunge la Mwananchi, ujana wangu niliutumia sana kwenye haya mambo, ila baadaye nikaja kuzichukia kupita maelezo baada ya kupata undani wa hawa watu wote, iwe wa upinzani au serikalini. Uanaharakati ulinielimisha sana nikafaulu kuwasoma wote jinsi walivyo, wanafiki na wazandiki kupita maelezo.

Siku hizi labda nione tu vichwa vya habari ila hutanikuta nasoma kila kitu kwa undani, nimekomaa tu kwenye kufuatilia mazuri ya nchi kizalendo, miradi ikifanywa naipokea na kuishabikia, japo wanaume wanapiga cha juu maana hamna jinsi naweza kuwazuia, ila kinachosalia na kufikia wananchi nakipokea na kukiombea.

Kuna kipindi ningekua mstari wa mbele kwenye haya yanayotokea baina ya Ruto/Raila/Uhuru/Mutua na kajamba wote, ningetokwa mipovu na kushinda kutwa nzima nikiponda na kuegemea kwenye mlengo mmoja. Lakini kwa sasa wayafanye tu, atakayezaliwa tutamlea.

Huko kwenu naona mumewaalika akina Membe kwenye NEC, sijui kipi kinasukwa, yeye ameshasema amejiandaa kupangua kila hoja, upinzani wa kwenu nao huwa hawaeleweki, wapo wapo tu, naona kwenye mitandao wanamsubiri Membe kwa hamu aje kwao wampe kiti moja kwa moja kama walivyofanya kwa Lowassa ambaye aliishia kuwatema kwa dharau.
 
Acha walumbane tu na mapovu yawatoke ila wasituletee machafuko. Ila kuna wakati nahisi kuwa hili suala la Membe VS CCM ni mchezo tu wa kutaka kutusahaulisha mambo ya msingi. Siwaamini kabisa wanasiasa, hasa kwa mtu aina ya Membe (mwanadiplomasia na shushushu aliyebobea) eti analumbana na viongozi wa chama chake kwenye twitter! Hainiingii akilini...
 
Uko sahihi kutia shaka kwa hilo, halafu eti maongezi yake yanadukuliwa kizembe pamoja na sifa zote alizo nazo, ila naona wapinzani wameingia kichwa kichwa, nyuzi za kumsifia Membe zimechachamaa.
 
Back
Top Bottom