Habari wana JF.
Nakaa natafakari tuzo 7 alizopata Diamond, ukweli ni kwamba My Number One imempa Diamond mafanikio sana ameweza pata tuzo hizo kwa sababu ya ya huo wimbo, pia ameweza kuvuka boda na kupata baadhi ya collabo na wasanii wakubwa Afrika kwa sababu ya nyimbo hiyo.
Je Diana anajisikia vipi kuona mafanikio hayo kupitia wimbo ambao anadai ni wimbo wake?, Diana mwenyewe aliwahi kuhojiwa na Saida Mwilima akasema nililia sana sikutoka nje kwa wiki kazaa naomba mniache.
Je Diamond nae anajisikia vizuri kuona dhuluma hiyo aliyofanya?.
Mjini mipangoo akilii vijijiiniii
Mbona hili suala lipo wazi kabisa na lilithibitishwa na producer wa hiyo beat. Huyo dada hakuipenda hiyo beat, na Diamond alipoitaka huyo dada alipewa taarifa na akaridhia beat ichukuliwe. Haikuwa wimbo bali ni beat tu. Huyo dada hayo ni maneno ya mkosaji.
Bora kauimba diamond, wengine hata wakipewa waigize hawataweza, huyu dogo anajua kuimba na kubuni c kama H.bb anayekatikakatika ovyo kwenye stage bila mpangilio. Dogo keep it up.
Davido ndio mwanamuziki mkubwa Africa????? Kina salif keita, femi kuti, youssour tuwaitaje?? Acha upuuzi wewe