Wimbo wa Seduce Me wa Ally Kiba ni "Copy & Paste"??

Wimbo wa Seduce Me wa Ally Kiba ni "Copy & Paste"??

Wimbo huu ndo amekopi na kupesti wa Ali Kiba. Kawakamate wajinga!
Ebu tuanzie hapa, kama wewe umeupata nasi titajie aliyeuimba nasi tuufuate ktk youtube au mtandaoni!
Wabongo bana,
Kweli ukitaka kuwaficha kitu kiweke kwenye maandishi.
Hiyo comment uliyoi-quote kwenye para ya mwisho nimemalizia hivi

"Sijaelewa hasa kaimba nani huo wimbo, wala kati ya huyo muimbaji na Ally Kiba ni nani hasa alianza kuimba. Pengine mkiusikiliza wimbo huo mnaweza kuuelewa umeimbwa na nani na kuanzia hapo tutajua nani alianza kuuimba."

Natumai kwa ku-quote kwako kote hukuona hiki kipengele. Rudia tena kusoma kisha uje u-comment
 
Nimekuelewa, tuwekee link basi twende huko wenyewe!
 
Nimekuelewa, tuwekee link basi twende huko wenyewe!
Mie nimefowadiwa tu kwenye Whatsapp mkuu wangu,
Alienifowadia nae kafowadiwa ndio akaniuliza nani kaimba,
Sasa kwakua hapa JF kuna watu wajuzi wa kila aina ndio nikasema nilete hapa kuuliza kaka yangu,
Ila sijui hata kama huu ndio kopi/cover au wa Kiba, wala mie sio timu Kiba wala timu Diamond, mie nlileta hapa ili tusaidiane
 
Mimi ni Ni shabiki wa diamond lakini kwa ujinga huu wa kuleta link isiyo tupeleka kwenye wimbo/account ya aliye imba wimbo huo unao sema ali kakopi ni kujishushia hadhi.

ILA JAMBO MOJA LINANISHANGAZA KWANINI KIBA ASIKANUSHE HABARI HIZI YEYE MWENYEWE?
Yule hapendi kujibu vitu hovyo
 
Wadau Kwema??

Kwa sasa Ally Kiba anatingisha na wimbo wake alioutoa hivi karibuni wa Seduce Me. Wimbo huo kwa sasa ni 'hit Song" kiasi kwamba popote unapopigwa basi watu wengi huonekana kuufurahia na kuusifia.

Sasa basi leo katika pitapita zangu huku na kule nikakutana na wimbo unaofanana na huo kuanzia "beats" mpaka "melody" yake, tofauti inakuja kwenye lugha ya Kiengereza iliyotumika pamoja na maana ya maneno yaliyotiumika labda.

Sijaelewa hasa kaimba nani huo wimbo, wala kati ya huyo muimbaji na Ally Kiba ni nani hasa alianza kuimba. Pengine mkiusikiliza wimbo huo mnaweza kuuelewa umeimbwa na nani na kuanzia hapo tutajua nani alianza kuuimba.

Utuambie huo wimbo umeutoa wapi
 
Back
Top Bottom