Wimbo wa Taifa ufupishwe

Wimbo wa Taifa ufupishwe

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Time management, tuokoe muda wa kuimba wimbo mrefu bila sababu.

Afrika (AU) ina wimbo wake, SADC ina wimbo wake na East Africa ina wimbo wake pia hivyo Tanzania hatuna sababu ya kurudia kuimba wimbo wa kuiombea Africa kwenye wimbo wetu.

Kufanya hivi ni kurudia bila sababu kile kinachofanywa na Wimbo wa African Union na kusababisha wimbo wetu kuwa mrefu bila sababu.

Nashauri kile kipande cha Mungu ibariki Afrika tuachane nacho kwenye wimbo wetu wa Taifa ili kibakie kipande cha Mungu ibariki Tanzania ili mambo mengine yabakie kwenye nyimbo za EA, SADC na AU ambazo pia tunahusika nazo.
 
Na bendera ipunguzwe rangi! Toa rangi ya blue maana tayari bahari inaonekana kwenye ramani!

Unganisha Mwanza, Geita, kagera, shinyanga, simiyu ita KANDA YA ZIWA Dar, lindi,Mtwara, Moro na pwani yenyewe ita MWAMBAO WA PWANI.

Bungeni kuwe na wawakilishi wa Kanda tu!

Aaah! Yote haya tuyaweke kwenye kundi Moja! KATIBA MPYA YENYE MENO!
 
Na bendera ipunguzwe rangi! Toa rangi ya blue maana tayari bahari inaonekana kwenye ramani!

Unganisha Mwanza, Geita, kagera, shinyanga, simiyu ita KANDA YA ZIWA... Dar, lindi,Mtwara, Moro na pwani yenyewe ita MWAMBAO WA PWANI...

Bungeni kuwe na wawakilishi wa Kanda tu!

Aaah... Yote haya tuyaweke kwenye kundi Moja! KATIBA MPYA YENYE MENO!

Rangi ya blue iachwe maana imeshaanza kuwa kama ndio nembo ya taifa. Air Tanzania, national team, udart, etc. Tutoe rangi ya kijani na njano maana zinafanana na club moja ya mpira hapa nchini iliyopoteza mwelekeo. Ni aibu kuwa na rangi zao kwenye bendera. Rangi nyeusi pia itolewe haina maana sana, bara zima ni watu weusi tu 😂😂
 
Na bendera ipunguzwe rangi! Toa rangi ya blue maana tayari bahari inaonekana kwenye ramani!

Unganisha Mwanza, Geita, kagera, shinyanga, simiyu ita KANDA YA ZIWA... Dar, lindi,Mtwara, Moro na pwani yenyewe ita MWAMBAO WA PWANI...

Bungeni kuwe na wawakilishi wa Kanda tu!

Aaah... Yote haya tuyaweke kwenye kundi Moja! KATIBA MPYA YENYE MENO!
Hahahaha[emoji2][emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Hata mimi huwa napata tabu pale unapokuwa unamuombea mshindani wako katika jambo flani. Mfano unachuana game na Kenya kufuzu kombe la dunia unaanza kumuomba Mungu aibariki Afrika na baadaye unaomba aibariki Tz, maanake utakuwa umemuombea pia mshindani wako ambaye yeye dua yake kajiombea pekeyake. Hapo baraka kwa Kenya zitakuwa 2 kwako 1 hivo uwezekano wa mpinzani wako kubarikiwa ni mkubwa zaidi.

Naunga hoja mkono, tufute ubeti wa kwanza au tuutumie kulingana na muktadha wa tukio lililo mbele yake.
 
Vaaaa barakoaa kwanzaaaaaaaa. Umenawamikonoooooooooooooooo
 
Mimi nina maoni tofauti kidogo nadhani kuna haja ya kuongeza ubeti wa kupigania uzalendo.. Waafrika wengi hatuna uzalendo na bara letu
 
Mawaziri wakongwe waliotumika ni KINGUNGE NGOMBALE MWIRU NA GEORGE HURUMA MKUCHIKA STEVEN MASATU WASSIRA
 
Kuna Muingereza mmoja aliwahi kusema ukitaka kuzijua Nchi za Kiafrika wewe sikiliza nyimbo zao za Taifa tu matatizo yao yote wanayaimba humo huku wakimuomba Mungu awasaidie lakini kiukweli ni wao na uporaji wao ndio tatizo.
 
Kanuni ya maombi ni kuwaombea wengine kabla ya kujiombea wewe mwenyewe. Hayo ndio maombi yenye nguvu.Mungu hapendi ubinafsi km alivyo mwanadamu.
Nitaifa gani lina wimbo wa aina hii? Ndio maana uzalendo wetu unalegalega sana. Unaanza kwa kuimbea Afrika kisha ndo uiombee nchi yako. Waliotunga wimbo tuwashukuru lakini sio vibaya tukifanya mabadiliko kidogo. Kama ikishindikana kukiondoa kipande cha Mungu ibariki Afrika basi wimbo uanze na Mungu ibariki Tanzania kisha ndiyo Mungu ibariki Afrika, Huwezi kuanza kwa kumuombea jirani kabla ya kujiombea mwenyewe.
 
Time management, tuokoe muda wa kuimba wimbo mrefu bila sababu.

Afrika (AU) ina wimbo wake, SADC ina wimbo wake na East Africa ina wimbo wake pia hivyo Tanzania hatuna sababu ya kurudia kuimba wimbo wa kuiombea Africa kwenye wimbo wetu. Kufanya hivi ni kurudia bila sababu kile kinachofanywa na Wimbo wa African Union na kusababisha wimbo wetu kuwa mrefu bila sababu...
Ni kweli halafu hicho kipande cha Mungu ibariki Afrika, wabariki viongozi wake, kina dosari, tunamwomba Mungu kuwabariki viongozi ambao ni majizi na wauaji kwa nia ya kujitajirisha wao.

Kuna members walishauri wimbo sahihi uwe ule wa Tazama ramani utaona nchi nzuri... ambao kimsingi ni mzuri na maudhui yake ni nzuri
 
Back
Top Bottom