Wimbo wa Taifa Ulivyotaka Kunitia Matatani...!

Wimbo wa Taifa Ulivyotaka Kunitia Matatani...!

Michael Scofield

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2011
Posts
1,225
Reaction score
473
Ni wimbo wa taifa ulivyotaka kunitia matatani au ni kilingala feki kilivyoniokoa.........?
Nilikuwa pande za mwisho wa reli kikazi, nikawa nimemtokea binti mmoja mzazi wake ni mwalimu mkuu katika shule mojawapo huko KG.
Tulikubaliana nimuibukie mida ya mchana ili twende lunch na maongezi zaidi.
Kufika maeneo ya shule nikaingia kichwa kichwa..! hamadi! nawakuta wanafunzi na walimu wamekusanyika wanaimba wimbo wa taifa, alafu kama kuna ugeni wa heshima hivi, kwani pembeni kulikuwa na askari wawili.

Mie haya ikanishika nikanyoosha kumbe kule nakoelekea hakuna njia ikanibidi kurudi na mara wimbo umeisha, Polisi na mwalimu mkuu wakanisimamisha na maswali mfululizo yakaanza.
Mwalimu akaanza "we kijana huna adabu kwa nini haueshimu wimbo wa taifa?"
Polisi nae " We kijana leo ndio utanieleza ni kwa nini haujui taratibu za nchi yako?"

Nikajua hawa nikibishana nao wataniharibia siku dawa ni kujifanya sijui kiswahili.
Kwa lafudhi ya kikongo wakati hata kikongo chenyewe sikijui, wala maana ya maneno nayoyatamka.
"Mobaya-boya ngana seyandoto, aloto na nzweli ya mandaa"
Askari " nini?"
Mie nikaendelea "Nakama la muki uliye tunangaa!"

Nikaona Mwalimu huyo anasepa zake huku askari akinitumbulia macho.
Nikampiga na la mwisho "Nakong'o ya lamukiya latunangaa, hakamatile sizyooo!"
Askari akafyonza "kumbe jitu lenyewe ni likimbizi"
Mie huyoooooooooo!
 
hahaha, wewe umetudanganaya huwezi kukumbuka maneno uliyoongea kwakuwa ni yakutunga hapo kwa papo na hayapo sasa wewe umeyakumbuka vipi
 
hahaha, wewe umetudanganaya huwezi kukumbuka maneno uliyoongea kwakuwa ni yakutunga hapo kwa papo na hayapo sasa wewe umeyakumbuka vipi
Kwa taarifa yako haya maneno ni ya kwenye wimbo.
Tafuta wimbo mojawapo wa Madilu System ndio utakapojua nachokiamaanisha. Hizi nyimbo tulianza kuzisikiliza tangu miaka ya themanini, nyie siku hizi si mnasikiliza zakina Khalid Chokoraa.

Sio madeshee wote unaowasikia ni Wakongo, kuna wangine ni wamatumbi wa Mtwara....!

Hakianani, yaani Madiluu umenichekesha kweli kweli. Na jinsi Mwalimu alivyosepa, na hata askari alivyo kusheet eti mkimbizi, mimi mbavu sina!! Hebu nikumbushe maaana ya maneno haya:
1. Paradiso.
2, Nzere
3, Pie mboyo,
4. Apura.

Masongi hayo ya the late Madilu System huniacha hoi sana!! Pia nijibu eti ni kweli Madilu anahusishwa na kifo cha Gwiji-Rwambo Makiadi [Franco]? Je Zaiko Langa Langa wapo?? Mkali wao Nyoka Longo yupo?? Album yao ama CD yao ya recently inaitwaje Mkuu? Wewe naona mtaalamu sana maeneo hayo!! Wale watoto wa dot.com mlozoea manyimbo yenu yasiyo na mbele wala nyuma tafadhali msichafue ukurasa huu!! Just stay away from it!!
 
Mkuu si unakumbuka miaka ya 80, tulikuwa na kina Tabu ley, Mbilia bel, Franco, Pepe kale na wengine kibao!
Sasa masongi yao yalikuwa yashazoeleka kichwani.
Bendi zetu za hapa nchini, kurekodi kenya au redio Tanzania.
Alafu mkuu inshu ya Madilu kuhusishwa na kifo cha Franco hata na mimi nasikiasikia na ni kuhusu...................! namezea hapo.
 
Scofield ina maana ulimfuata mtoto wa shule au mwalimu? (kama njia ilikuwa inaishia hapo shule).
 
umetisha mkuu, vipi wande ku-arrest kwa kuishi nchini bila kibali
 
Back
Top Bottom