Michael Scofield
JF-Expert Member
- Jul 30, 2011
- 1,225
- 473
Ni wimbo wa taifa ulivyotaka kunitia matatani au ni kilingala feki kilivyoniokoa.........?
Nilikuwa pande za mwisho wa reli kikazi, nikawa nimemtokea binti mmoja mzazi wake ni mwalimu mkuu katika shule mojawapo huko KG.
Tulikubaliana nimuibukie mida ya mchana ili twende lunch na maongezi zaidi.
Kufika maeneo ya shule nikaingia kichwa kichwa..! hamadi! nawakuta wanafunzi na walimu wamekusanyika wanaimba wimbo wa taifa, alafu kama kuna ugeni wa heshima hivi, kwani pembeni kulikuwa na askari wawili.
Mie haya ikanishika nikanyoosha kumbe kule nakoelekea hakuna njia ikanibidi kurudi na mara wimbo umeisha, Polisi na mwalimu mkuu wakanisimamisha na maswali mfululizo yakaanza.
Mwalimu akaanza "we kijana huna adabu kwa nini haueshimu wimbo wa taifa?"
Polisi nae " We kijana leo ndio utanieleza ni kwa nini haujui taratibu za nchi yako?"
Nikajua hawa nikibishana nao wataniharibia siku dawa ni kujifanya sijui kiswahili.
Kwa lafudhi ya kikongo wakati hata kikongo chenyewe sikijui, wala maana ya maneno nayoyatamka.
"Mobaya-boya ngana seyandoto, aloto na nzweli ya mandaa"
Askari " nini?"
Mie nikaendelea "Nakama la muki uliye tunangaa!"
Nikaona Mwalimu huyo anasepa zake huku askari akinitumbulia macho.
Nikampiga na la mwisho "Nakong'o ya lamukiya latunangaa, hakamatile sizyooo!"
Askari akafyonza "kumbe jitu lenyewe ni likimbizi"
Mie huyoooooooooo!