1.
nawashukuru wapendwa, shairi mmelipenda,
nitaheshimu kufundwa, juu ya kulila tunda,
sitakinai kupondwa, nimeshazoea mlenda,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!
2.
nakushukuru kifrogu, vionjo kunitilia,
wachangamsha blogu, wengine wakimbilia
hata walio na sugu, somo litawaingia,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!
3.
wa pili ule ubeti, ni wazi pasi kiwingu,
kwa wima ama kuketi, utajua nini wingu,
fikira iliyo ya dhati, itaing'amua mbingu,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!
4.
paka jimi mchokozi, kweli nilikuwa bize,
mimi sijawa mpuuzi, yalojiri nisiwajuze,
bila ule udokozi, kazi nisizibakize,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!
5.
wote mloniwosia, tazingatia ushauri,
nisijebaki mkia, maisha kutahayari,
sitakuwa mmbea, kwa kila ilo habari,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!
6.
ni mengi yalitokea, na jibu kuchelewa,
shule ya ng'ambo tokea, mipango nililemewa,
baraka nizopokea, sio za kuambiwa,
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!
7.
harusi iko novemba, hapo sasa ni kamili,
nitavaa na kilemba, nitang'arisha na kandili,
mapambo nitajiremba, tena yale ya ukwel
mimi nawe Naimani ni kama wingu na mbingu!