Tumsifu Benges
New Member
- Aug 14, 2022
- 1
- 0
UTANGULIZI
Neno Kiongozi limebebwa na neno ‘nafasi’ ambayo inakamilisha uwepo wa icho cheo yaani ‘’KIONGOZI’’
Ni vizuri kuelewa katika maisha tunayoishi leo kuna mwanzo wake vivyo hivyo kuna mwisho wake,kujikumbusha ni swala la muhimu sana hili nafasi zetu tunazopata duniani iwe ni kwenye mashirika binafsi au serikalini tujue uja na kupita na Mungu utupa akijua kuna jamii kubwa ya watu wake wanaotutegemea.
Ni desturi na mpango wa Mungu katika nafasi yoyote unayopewa wewe kama kiongozi ili kuongoza anakutazamia kwanza aweze kutimiza malengo ya hiyo nafasi pasipo kumbagua mtu yeyote yule huku ukifuata miiko ya hiyo na nafasi na sheria zilizowekwa.
Ndugu kiongozi kumbuka kila mtu ametokana na Mungu isipokuwa watu hawa uzaliwa kwenye familia tofauti tofauti hivyo Kiongozi kubagua watu wakati wa utoaji huduma sio mpango wa Mungu wala hao waliokuteua hivyo ni vyema kuzingatia miiko au sheria na miongozo ya kile anachotakiwa kukifanya kwa ushihi,uaminifu na ukamilifu.
Kiongozi wa leo amebadilika na kubadili utaratibu au maana ya halisi kuongoza na kutanguliza ubinafsi,uchoyo,ufisadi na tamaa,hivyo kupelekea tabaka la chini kupuuzwa,kuonewa na kuachwa sana nyuma kwenye mambo mbalimbali ambayo kimsingi yalitakiwa kutatuliwa na kushughulikiwa na huyo kiongozi hili lengo lililokusudiwa liweze kufikiwa,kutimia na kuleta ustawi kwa hao wanaongozwa.
Kumekuwepo na kupuuzwa sana kutoka kwenye mamlaka au nafasi mbalimbali katika taifa ambavyo kimsingi vinaendelea kusababisha watu wengi kuishi maisha ambayo kihalali yalitakiwa kubadilisha na misingi na utumishi mzuri wa hao viongozi wenyewe kwa kuweka sera zisizo kandamizi kwa kila nyanja.
Mfano kuna vijana wengi wamemaliza vyuo kwenye nchi mbalimbali lakini kutokana na ubinafsi ,tamaa na ufisadi wa viongozi wenye mamlaka nafasi zao wamekuwa wakipewa watu wengine kama familia ya kiongozi husika au kwa kupewa rushwa,hivyo kupelekea wakati mwingine nchi au taasisi kutokusonga katika swala zima la kutimiza malengo yaliyowekwa,hii inatokana na uwezo wa hao waliopendelewa kuwa ukilinganisha na nafasi wanazopewa hivyo kushindwa kusababisha mabadiliko badala yakekuendelea kusababisha maendeleo kudumaa.
Ili tuweze kumpata kiongozi bora na mwenye kutawala vyema na kuongoza wengine napendekeza ni vyema mambo yafuatayo yakaangaliwa kwanza kwa huyo mtu.
Kiongozi Mzalendo
Ninaweza kusema uzalendo ni ile hali ya kupenda unachokifanya,kupenda unawaongoza na kutopenda mtu mwingine akandamizwe kwa masilahi ya mtu mwingine.
Hili ni jambo la msingi sana ambalo kila kiongozi anatakiwa awe nalo kabla na baada ya kupewa nafasi yoyote au kuwaongoza wengine,kiongozi akiwa mzalendo ni rahisi sana kuridhika maana siku zote uzalendo utengeneza kitu kinaitwa ’HURUMA’’hivyo huyu kiongozi ataongoza ili aweze kutimiza wajibu wake kwa usahihi kabisa.
Kiongozi mwenye upendo
Ni desturi kwa mtu mwenye upendo kuumia pindi atakapoona mtu mwingine akionewa,akidhulumiwa na kunyimwa haki zake za msingi kwa masilahi ya watu au mtu mwingine,kiongozi au viongozi wengi wamekosa upendo kwenye nafasi zao hivyo kupelekea uonevu kwa wengine na kuwanyima haki zao za msingi kama kiongozi.
Viongozi wengi wamekuwa chanzo cha vurugu kwa sababu ya tamaa hivyo kuwafanya wanyoge kulia na kuumizwa na kudhulumiwa haki zao za msingi kwa masilahi yao wenyewe na vizazi vyao.
Hivyo napendekeza mamlaka zote zijitahidi sana kuwa na semina za mara kwa mara kwenye ngazi tofauti tofauti za kiutendaji haswa kwa viongozi ambao tiyari wapo kwenye hizo nafasi ili waweze kuelewa thamani na utu wa mtu mwingine katika kupata haki za msingi wakijua binadamu wote ni sawa,ikiwezekana kiwepo kipimo cha upendo kwa viongozi wanaopewa mamlaka ili wasiwe chanzo cha kuwagawa watu na kuleta dhuluma na manyanyaso kwa faida yao wenyewe.
Kiongozi mwajibikaji
Dhana ya uwajibikaji ni jambo la msingi pia linahitaji kuangaliwa sana kwa kila kiongozi anayepewa au kuaminiwa kuongoza wengine,uwajibikaji kwa viongozi wengi umepungua sana kutokana na kulizika na mamlaka walionayo.
Ni vyema kuwepo na kipimo cha uwajibika kwa kila kiongozi sawasawa na sehemu aliyopewa kuiongoza hii itasaidia wengi kuwahudumia watu wote katika kwa nafasi zao kwani akishindwa kuwajibika nafasi yake atapewa mwingine hivyo kuleta maendeleo ya haraka kwa watu na taifa kwa ujumla.
N.B. Ni muhimu kwa kiongozi kujifunza dhana nzima ya uwajibikaji kwa watu wote.
Kiongozi mwenye maono na nafasi yake.
Hii inaweza isiwe kitu kinachopewa kipaumbele sana kwa wenye mamlaka wakati wa uteuzi wa viongozi wengi ,lakini hili ni jambo la msingi sana kwa kila nafasi ambayo kiongozi anapewa kuiongoza au kusimamia.
kiongozi mwenye maono na nafasi yake mara zote umpelekea kuleta ushirikishi wa jamii nzima ya watu alionao ili kuweza kusababisha mageuzi ya karne na karne katika eneo alilopewa kuongoza,hii inapekea kuleta kwa Pamoja kila tabaka liwe la chini katikati au juu kushirikishwa hivyo kuchochea nguvu ya kufanya kazi kwa watu wote ambayo itapelekea mabadiliko chanya na yenye nguvu kwa jamii nzima ya eneo analoliongoza kiongozi husika.
Napendeza mamlaka zitenge vyuo maalum vya kufanya mafunzo kwa viongozi kabla hawajaingi kwenye majukumu yao wanayopangiwa kufanya ili hii zana ya uwajibikaji iweze kujengwa mwanzoni kabisa kabla hawajaingia kwenye majukumu yao.
Kiongozi mwenye kuheshimu haki za watu wake.
Haki ni kile kitendo cha kumpa mtu kile anachositahili pasipo kumfedhehesha au kumkandamiza kwa hali yoyote ile aliyonayo bali kwa kufuata taratibu na sheria zilizowekwa sambamba na kuzingatia haki za binadamu.
Katika uongozi kwenye ngazi mbalimbali viongozi wengi wamekosa hii sifa,watu wanaonewa,watu wanakandamizwa,watu wanadhulumiwa pia watu wanapuuzwa pasipo kupatiwa haki zao za msingi ikitokea ili uweze kupata haki yake inamlazimu mtu atoe chochote kitu hivyo kupelekea watu wengi kukosa haki zao za msingi.
Mfano; Mnamo mwaka jana mwezi wa kumi na moja nilipata kesi ya kubambikiwa ya wizi wa fedha taslimu million tano na nusu,inasikitisha sana mamla tunaziamini kwamba zitatusaidia ndo ilikuwa ya kwanza kunikandamiza mimi,ndugu msomaji wa andiko hili niliwekwa mahabusu kwa muda wa wiki nzima huku kukiwa na vitisho vya hapa pale kutoka kwa hao watoaji haki baadae iligundulika yule mtu alitoa pesa ili niweze kukamatwa,sasa wapo wengi sana wanaonewa kwasababu kama hizi na mamlaka husika zinaona nis awa tu haki za msingi za huyu mtu wa chini zikandamizwe ili mwenye nacho aweze kutimiza lengo lake’’ SIO SAWA’’.
Hivyo viongozi wenye kutenda haki wanatakiwa sana ili kuweza kuwafariji hawa ambao hawana chochote ili waweze kuishi kama binadamu wengine duniani.
HITIMISHO
Ndugu kiongozi nakushauri badilika leo kwanza mshukuru Mungu kwa nafasi aliyokupa kama kiongozi pia muogope Mungu kwa hiyo nafasi ukijua siku moja utaulizwa hesabu yake sawa na utumishi wako.

Upvote
0