Elections 2010 With 70% Voters' turnout, Slaa Wins; Less than that Kikwete Wins - My Prediction:


MK hiyo ya kura kuibiwa i agree with you have a look at this


Mkuu wengine tuwachovu sana wa IT, nadhani unamaanisha hizo website zote zinashea IP code moja!!!! Please naomba utoe maelezo ya ziada
 
Mkuu wengine tuwachovu sana wa IT, nadhani unamaanisha hizo website zote zinashea IP code moja!!!! Please naomba utoe maelezo ya ziada


Website zote zimekuwa hosted katika server moja,kwanini server inayo host NEC ndio inayo host jkikwete2010.com, Hapa nina wasiwasi sana ukijaribu ku-ping all the above sites eg ping nec.go.tz, kisha jmkikwete.com the same ip address ina reply ina maana lolote laweza kufanyika
 
Not more than 2 hours. I believe we can afford that. Uwezo tunao. Sababu tunayo. Tuweke NIA sasa

Mimi ningeshauri uhakikishe Jumapili unawahi mapema kwenye kituo cha kupigia kura ili uweze kuitumia haki yako vizuri kuchagua kiongozi anayefaa
 
Mzee Mwanakijiji
Heshima kwako
Tunashukuru kwa uchambuzi wako, naomba kama upo karibu na viongozi wetu, tumwombe Dr Slaa, jumamosi awe hewani japo kidogo ata dakika mbili -tatu kuondoa huu wasiwasi wa wizi wa kura ili watu wajitokeze kupiga kura. Binafsi sina shaka na nimejiandaa iyo jumapili kwenda kumpigia kura.
 

With this naoba nimhakikishie MKJJ kuwa wizi wa kura upo!!! Hakuna cha systems or nduguye na systems!!!
 
Ni miezi miwili sasa watanzania tumekuwa tukisikiliza sera za vyama tofauti. Ni hivi karibuni watanzania watafikia kufanya maamuzi magumu ya kubadilisha uongozi wa serikali kwa kuajiri kiongozi mwingine tofauti na JK kupitia sanduku la kura.

Kama Mwanakijiji alivyosema hapo juu kuwa haya matumaini ya maamuzi magumu hayawezi kufanyika kama wapenda mageuzi hawatajitokeza kwa wingi kufanya hayo maamuzi magumu kuchukuwa nafasi na historia ya nchi yetu. Nina hakika kuna baadhi wa wananchi watakuwa wamejiandikisha kupiga kura lakini siku hiyo waweza kujisikia wavivu au wagonjwa na kushindwa kwenda kupiga kura. Ningependa kuchukuwa nafasi hii kuwaomba watanzania wenzangu kuhakikisha kuwa hakuna mtu anachezea hiyo nafasi lulu kwa Taifa letu.

Tuhakikishe tunahamasisha wenzetu wajitokeze siku hiyo kupiga kura. Kama kuna wale ambao wanaona kuwa watashindwa kufika kwenye kituo cha kupigia kura kwa sababu za ugonjwa, unaweza kumuomba hata jirani yako akusindikize ili utimize kufanya haya mabadiliko.
Kwa walioko jijini Dar, ukishindwa kwenda kupiga kura kwa sababu ya ugonjwa......tuwasiliane kwa email indumeyene@jamiiforums.com ili nikupe namba ya simu na kuweza kupata huduma ya usafiri kwenda kwenye kituo chako cha kupigia kura.
MAAMUZI MAGUMU NA YA KWELI YANAHITAJIKA SASA, NAKUPENDA TANZANIA.
 

Mkuu kama hizo website zote ziko kwenye server moja, it is likely database ya NEC iko serviced na mwenye server!! Sasa hapa ndo ile maneno ya kuchakachua daftari inakuja vizuri!!! Wizi utafanyika katika daftari, watakuwa wamefanyia kazi maeneo yote ambapo CHADEMA wana nguvu, and so kuondoa possible voters!!! Or something!!!

I predict kutakuwa na matatizo makubwa on sunday ktk vituo vingi!!! They know for sure kwa uhalali hali ni mbaya kwao!! Cha msing tujitokeze kwa wingi!!!!
 
My intitial prediction was 40, 30, 30 being Kikwete, Slaa and then Lipumba. However the Lipumba's vote could go JK's way like about !0% an then 5 % to Slaa. Then with slim marging Mkwere atarudia ufalme. hata kwa ile 40, 30, 30 bado Mkwere angeshinda kisa mabadiliko ya katiba ya Mshindi kashinda na si uwiano wa kura;Senksi to Nkapa!
 

Hilo likifanyika ni jema. Lakini, je inakuwaje pale ambapo watu wakaanzisha vurugu za ki Green guard ili pavurugike na watu wale kichapo ndo wapeleke kura wilayani? Mie naamini kwamba hapo ndipo mahali wanapopenyeza hizo kura zao feki, na by the time mnafika wilayani, maboks kibao feki yamejazwa!
 

I agree, but I predict JK wins by more 70%. In addition to scooping Lipumba's votes as you rightly put it JK is likely to benefit from the newly recruited CCM young voters. My prediction is drawn from the fact that opposition parties were surprized by irregular increment of about 3 million potential voters relative to 2005 elections. My guts tell me that the majority of the 3 million potential voters are likely to belong to CCM. My prediction.
 

Huu ni mtazamo wako.
Labda nikupe intro ndogo tu ya sie tunaoshinda vijijini. Hamasa ya watu wa vijijini (ambako wapigakura ni wengi kuliko sisi wa mjini) kuhusu uchaguzi wa mwaka huu ni kubwa sana na kuna uwezekano mdogo sana wa JK kushinda kwa maeneo ya vijijini.
 
Nipo katika CCM wengi nao wanasema watampigia kura Dr Slaa na pia nilikuwa sehemu kama Dodoma ambaye miaka mingi sana ilikuwa chini ya CCM ila kipindi hiki watu wamemka sana na pia na Mungu saidia Slaa atakuwa Rais wetu mpya
 
Nakubaliana kabisa na wewe kwamba ni muhimu sana sote tukaenda kupiga kura maana hiyo ni hatua ya kwanza muhimu kuliko zote katika kuleta mabadiliko katika mfumo wowote wa kidemokrasia.
But honestly Mwanakijiji, unafikiri kama Dr. Slaa atashinda, dola hii yenye kuunganishwa na chama tawala katika mambo karibu yote, itakubali kuruhusu mapenzi ya wananchi yatimie bila upinzani wowote?
 


Bandungu Wild Card na The Good mnaweza kuwa mko sawa, ila nimeshindwa kuelewa mnatumia kigezo gani kunihakikisha kuwa Watanzania hata wafanywe nini hawawezi kuwa na mawazo mbadala.

Kumbuka kampeni za afya, elimu au matangazo ya biashara ya kuuza vocha, sabuni, soda, kondomu, bia nk hayana tofauti na kampeni za siasa. Kama kungekuwa hakuna nafasi ya kubadili mtizamo, msimamo au mwenendo wa walengwa hakuna mtu angeweka msisitizo kwenye kampeni/matangazo.

Kuamini pamoja na mapinduzi yote ya teknolojia bado Watanzania ni wale wa 1995, ni kupotosha ukweli kwani voda, tigo, radio na TV stations zingeshafunga virago
 
Pumba tupu, when did Tanzania have 70% of voters voting?
 
wow... I'm just thinking..
No, Mzee Mwanakijiji! It is the other way round! It was low voter turnout that helped CHADEMA got the votes they garnered! Wanaoipenda CCM ndiyo wengi hawakwenda kupiga kura. It is CCM members who are normally complacent and don't turn out in big numbers to vote, especially women and the aged. "CCM tutashinda tu hata nisipokwenda kupiga kura", they would say. But show me vijana wa CHADEMA ambao this time around hawakwenda kupiga kura? Wakisaidiwa na wasaliti wenye vinyongo BINAFSI ndani ya CCM (siyo walioichoka CCM). Complacency hii ya wanaCCM kutokwenda kupiga kura, na mahali pengine siyo complacency bali vitisho na hila za wapinzani dhidi ya wanawake na wazee wa CCM, (of course na usaliti) vikitafutiwa dawa na CCM, come 2015 wapinzani watashangaa! Wabunge wao watakuwa wachache Bungeni kuliko ilivyokuwa 2005 - 2010.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…