Witness from the front line: Hili zoezi la sensa mlioko juu msiporekebisha haya kwa haraka tegemeeni taarifa mbovu kuwahi kutokea

Hii comment imenichekesha sana. Kwa hiyo mzigo hauwezi kufika ikiwa punda amekufa?
 
Ili upate hiyo gps, internet ya simu ndio inatumika? Namaanisha muda wote internet inatakiwa kuwa ON?
 
Tatizo ni moja tuu, hivyo vishikwambi vinatumia offline map, waandaaji wa hili zoezi wangeweka programu yenye kutumia data badala ya offline map.
Upande wa Map ndo mizinguo, ningependa sana nitumie simu yangu kuliko kishikwambi maana kwa simu inapiga kazi saafi kabisa maana nawasha data all time na zote zinasoma ndani ya EA.
 
Ili upate hiyo gps, internet ya simu ndio inatumika? Namaanisha muda wote internet inatakiwa kuwa ON?
Sijui kuhusu huo mfumo wao, ila kuna Mifumo ambayo Coordinates unapata ukiwa offline, infact ndio mfumo unaotakiwa kutumika sababu si sehemu zote utapata internet, hasa zile remote areas.
 
Hapana, umefikiria sehemu ambazo huwezi kupata internet huyu karani atapata wapi hizo coordinates? Mfumo wa kuchukua coordinates offline ni sahihi wauboreshe tu kuondoa ugumu au changamoto za kuipata.
 
Sijui kuhusu huo mfumo wao, ila kuna Mifumo ambayo Coordinates unapata ukiwa offline, infact ndio mfumo unaotakiwa kutumika sababu si sehemu zote utapata internet, hasa zile remote areas.
Ndio nataka nijue huko ili nione jinsi gani zoezi litakuwa gumu
 
Siyo sehemu moja, bali karibia nchi nzima wametoa laki mbili tu! Huku watu wanatumia gharama kubwa kila siku kwa ajili ya kujikimu. Pia nashindwa kuelewa hawa viongozi wetu walioko maofisini wanatumia akili zipi....hili zoezi litatumia pesa nyingi sana pasipo sababu..ilikuwa ni suala la kukaa na wenyeviti wa vitongoji na wa mitaa, wakelezwa taarifa ambazo serikali inahitaji alafu wakapewa muda hata wiki moja au mbili na alafu wakawapa hata posho kidogo sana. Nina uhakika wenyeviti hawa wangeleta taarifa sahihi kwa zaidi ya asilimia 100% na wala kusingekuwepo na uhitaji wa vishikwambi, sijui GPS .. ... zoezi lingekuwa bora sana.
 
Watu kujua kwingi!!!

Huyo mjumbe anajua sensa ni nini hata au kujua idadi ya watu kwenye kitongoji chake tu ndo inatosha

Acheni ujuaji sensa ina taratibu zake na namna yake maalumu ya kukusanya taarifa mbalimbali (tena nyingi kweli kweli) na ndio maana watu wanakula semina kwa takriban theluthi ya mwezi
 
Kabisa, jamaa ametoa alert ya jambo jema sana na Mungu ambariki kwa hilo.
Upikaji hapo lazima uwepo sababu:
1. itakuwa vigumu pia kuanza kumuhoji tena mtu ambaye ulishamuhoji kwa masaa mawili.....ataona anasumbuliwa
2. Wengi wa makarani wenyewe ni hawa vijana ambao wasio na ajira ambao kurahisisha mambo ni sifa yao kuu (rejea anuani za makazi)
 
Mungu mwenyewe alisema hakuna kuhesabiwa nyie zaeni tu huku mkimtegemea yeye.
 
Kuna maswali niliwahi kumuuliza Kamishna wa Sensa mama Anne Makinda. Swali lilikuwa usahihi wa taarifa kuwiana na teknolojia iyakayotumika. Nikitaka kufahamu ufahamu wa wakusanya taarifa.

Nakumbuka niliwahi kushiriki zoezi la pilote la anuani za makazi ambapo mimi nilikuwa layman lakini kwenye zoeI maafisa wa Manispaa waliingia mitini kwa sababu ya kushindwa kuelewa wanafanya njni.

Ukweli ni kwamba. Wangekusanya taarifa mannual huku wakiwa na GPRS device kuweka pin ya kila kaya na kujaza coordinates kwenye data sheet.

Kisha waajiri waingiza data ambao watajaza datasheets na kuunganisha coordinates kwenye server


Mungu awasaidie kwa kweli. Na sijui malipo itakuwaje
 
Hiyo ndiyo isiyotakiwa sasa! Kumbuka intaneti inatumika kuboost tu ili ramani isomeke (ifunguke) basi baada ya hapo unahitajika kufunga data... tatizo hamsomi hata miongozo halafu mkiharibikiwa mnakuja kulialia hapa
 
mfumo umetengenezwa from scratch na IT wa hapa hapa bongo au umetengenezwa na IT wa nje ya nchi (umenunuliwa kutoka nje ya nchi)?
thubutu! IT wa Bongo hawana uwezo huo,
ni system za ki-paskitani izo, so kuomba marekebisho mpaka yafanyike ni miezi kadhaa ipite
 
Mi nafikri muwe na alternative. Kidigitali ikifeli mnaswitch analogy. Yani shkwambi likizingua unachukua kabrasha lako unajaza. The only way forward
 
UV CCM waliojazana humo tunatarajia hayo yakupika data yatokee ..enewei hata hivo hakuna wa kujali chochote kwenye nchi hii...pika data chukua chako maisha mengine yaendelee..Hilo li application nasikia NI la marekani..
 
thubutu! IT wa Bongo hawana huwezo huo,
ni system za ki-paskitani izo, so kuomba marekebisho mpaka yafanyike ni miezi kadhaa ipite
Kumbe ndio maana unawaletea shida watumiaji wa mfumo maana mfumo unabidi utengenezwe kuendana mazingira ya eneo husika na pia kwa kua mfumo unatengenezwa na team ya programmers/developers inabidi ufanyiwe testing kadhaa kila hatua ya uundwaji wa mfumo inabidi ufanyiwe majaribio kuthibitisha kua unafanya kazi bila kuleta shida kwa mtumiaji na hio team ijiridhishe kua mfumo upo sawa hauleti errors/bugs zozote au mfumo hauna complications zozote kwa mtumiaji yaani utamrahisishia mtumiaji kuifanya kazi yake pasina kutumia nguvu na akili mingi na pia team ijithibitishie kua mfumo hauna shida yoyote kabla haujakabidhiwa kwa mteja/mtumiaji husika kwamba unafanya kazi kwenye mazingira yawayo yoyote ya mtumiaji/mteja pasina kuleta shida yoyote, swali km mfumo umetengenezwa na ma IT wa Pakistani from scratch (code after code) na unahusu mazingira ya Pakistan je! Wakati mfumo unatengenezwa ulifanyiwa testing (majaribio) aidha na ma IT wa bongo au wa Pakstan kwamba kwenye mazingira ya bongo huo mfumo unaweza kufanya kazi bila kunaleta errors zozote kwenye haya mazingira au ndio wuacha tu tununue tutajua mbele ya safari?

Nawasilisha..
 
Vitongoji wangewaza fanya kazi hii kwa ufanisi zaidi. Nyie mngeenda chukua taarifa kwao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…