Witness from the front line: Hili zoezi la sensa mlioko juu msiporekebisha haya kwa haraka tegemeeni taarifa mbovu kuwahi kutokea

Witness from the front line: Hili zoezi la sensa mlioko juu msiporekebisha haya kwa haraka tegemeeni taarifa mbovu kuwahi kutokea

Hawatakusikiliza coz wanakazana kulamba keki ya sensa huku makarani wakipewa wali maharage yanayonuka.

Kuna sehemu wamelipwa sh 200,000 tu siku ya 15 leo huku wakilala guest houses na kujtegemea chakula cha jioni.

Kile kibibi kinasisitiza eti uzalendo mbele. Hawajui magumu tupatayo wala roho ya huruma kale kabibi hakana.

Hapa ni punda afe mzigo ufike. Mzigo utafikaje wakati punda kafa?
Hii comment imenichekesha sana. Kwa hiyo mzigo hauwezi kufika ikiwa punda amekufa?
 
Mambo kama haya wawe wanaacha siasa , baadh ya wakufunzi Kwa kweli ni janga , huyu anakwambia ukiwa unatafuta majira nukta zungusha tablet , mwingine anakwambia inabd utulie usitingishike, mwingine anakwambia zima Kwanza location , mwingine anasema boost na internet , huyu anasema huruhusiwi kuwa na simu au kuweka laini kwenye tablet , yaan ni vurugu tupu sa sjui hyo internet unaipataje
Ili upate hiyo gps, internet ya simu ndio inatumika? Namaanisha muda wote internet inatakiwa kuwa ON?
 
Tatizo ni moja tuu, hivyo vishikwambi vinatumia offline map, waandaaji wa hili zoezi wangeweka programu yenye kutumia data badala ya offline map.
Upande wa Map ndo mizinguo, ningependa sana nitumie simu yangu kuliko kishikwambi maana kwa simu inapiga kazi saafi kabisa maana nawasha data all time na zote zinasoma ndani ya EA.
 
Ili upate hiyo gps, internet ya simu ndio inatumika? Namaanisha muda wote internet inatakiwa kuwa ON?
Sijui kuhusu huo mfumo wao, ila kuna Mifumo ambayo Coordinates unapata ukiwa offline, infact ndio mfumo unaotakiwa kutumika sababu si sehemu zote utapata internet, hasa zile remote areas.
 
Tatizo ni moja tuu, hivyo vishikwambi vinatumia offline map, waandaaji wa hili zoezi wangeweka programu yenye kutumia data badala ya offline map.
Upande wa Map ndo mizinguo, ningependa sana nitumie simu yangu kuliko kishikwambi maana kwa simu inapiga kazi saafi kabisa maana nawasha data all time na zote zinasoma ndani ya EA.
Hapana, umefikiria sehemu ambazo huwezi kupata internet huyu karani atapata wapi hizo coordinates? Mfumo wa kuchukua coordinates offline ni sahihi wauboreshe tu kuondoa ugumu au changamoto za kuipata.
 
Sijui kuhusu huo mfumo wao, ila kuna Mifumo ambayo Coordinates unapata ukiwa offline, infact ndio mfumo unaotakiwa kutumika sababu si sehemu zote utapata internet, hasa zile remote areas.
Ndio nataka nijue huko ili nione jinsi gani zoezi litakuwa gumu
 
Hawatakusikiliza coz wanakazana kulamba keki ya sensa huku makarani wakipewa wali maharage yanayonuka.

Kuna sehemu wamelipwa sh 200,000 tu siku ya 15 leo huku wakilala guest houses na kujtegemea chakula cha jioni.

Kile kibibi kinasisitiza eti uzalendo mbele. Hawajui magumu tupatayo wala roho ya huruma kale kabibi hakana.

Hapa ni punda afe mzigo ufike. Mzigo utafikaje wakati punda kafa?
Siyo sehemu moja, bali karibia nchi nzima wametoa laki mbili tu! Huku watu wanatumia gharama kubwa kila siku kwa ajili ya kujikimu. Pia nashindwa kuelewa hawa viongozi wetu walioko maofisini wanatumia akili zipi....hili zoezi litatumia pesa nyingi sana pasipo sababu..ilikuwa ni suala la kukaa na wenyeviti wa vitongoji na wa mitaa, wakelezwa taarifa ambazo serikali inahitaji alafu wakapewa muda hata wiki moja au mbili na alafu wakawapa hata posho kidogo sana. Nina uhakika wenyeviti hawa wangeleta taarifa sahihi kwa zaidi ya asilimia 100% na wala kusingekuwepo na uhitaji wa vishikwambi, sijui GPS .. ... zoezi lingekuwa bora sana.
 
Kwa namna sensa inavyoendeshwa nchi hii, ni mradi wa upigaji. Tuna wajumbe wa kazi gani kama hawajui idadi ya kaya zilizopo kwenye maeneo yao pamoja na idadi ya watu kwa kila kaya?

Badala ya kutumia billions of taxpayers ' money, kwanini wasingepewa wajumbe wa nyumba kumi hii kazi wakaifanya taratibu hata kwa miezi kadhaa huku wakipewa posho?

Wizi mtupu!
Watu kujua kwingi!!!

Huyo mjumbe anajua sensa ni nini hata au kujua idadi ya watu kwenye kitongoji chake tu ndo inatosha

Acheni ujuaji sensa ina taratibu zake na namna yake maalumu ya kukusanya taarifa mbalimbali (tena nyingi kweli kweli) na ndio maana watu wanakula semina kwa takriban theluthi ya mwezi
 
Wewe ni mzalendo ila kwa bahati mbaya hawatakusikiliza sababu lengo la serikali yetu si ufanisi wa kazi bali kumaliza kazi, data zingine wataenda kuzipika na kuzichekecha wenyewe huko. Umeeleza kwa namna ambayo hata sisi ambao hatuko huko tumeelewa na tumezielewa changamoto na hakika si za kupuuza. Kama mtu yuko familiar na mambo ya data atamuelewa vizuri mleta uzi.

Lengo la teknolojia ni kurahisisha kazi, iweje hili liwe gumu huko? Hilo li application wamelitoa wapi, wao walipolifanyia mazoezi hawakuona hizo errors? Hawana consultant mwenye uzoefu na mambo ya data? Serikali inaweza kupoteza pesa nyingi sababu ya uzembe wa watu kama hawa waliopewa jukumu la kusimamia zoezi zima.
Kabisa, jamaa ametoa alert ya jambo jema sana na Mungu ambariki kwa hilo.
Upikaji hapo lazima uwepo sababu:
1. itakuwa vigumu pia kuanza kumuhoji tena mtu ambaye ulishamuhoji kwa masaa mawili.....ataona anasumbuliwa
2. Wengi wa makarani wenyewe ni hawa vijana ambao wasio na ajira ambao kurahisisha mambo ni sifa yao kuu (rejea anuani za makazi)
 
Mungu mwenyewe alisema hakuna kuhesabiwa nyie zaeni tu huku mkimtegemea yeye.
 
Wakat wa wa vita ya pili ya dunia moja ya Siri kubwa Kwa USA na washirika wake kupata ushindi ni kuwasikiliza waliokuwa front line yaani kwenye uwanja wa mapambano , na maoni Yao yalisikilizwa moja Kwa moja na high command na kufanyiwa kazi haraka iwezekanavyo bila mtu wa Kati kuleta siasa ...!! Waliokuwa kwenye battle zone Walitoa taarifa kuhusu Hali ya mapigano , intensity , wapi palipopungua , silaha gani miyeyusho na silaha za namna gani ziboreshwe , haya maoni ni katika idara zote za kijeshi kuanzia jeshi la ardhini ( marine) jeshi la majini (US navy) , na jeshi la anga (Airforce) , Marekani ilianza vita kama underdog Ila ikamaliza ikiwa superior and most feard nation.

Aliyeko front anajua exactly the horror of war...!! Kutomsikiliza Kwa sababu iwayo yoyte ile ni kuhalalisha kushindwa.

Back to the topic , Mimi ni karani wa Sensa , katika mchakato mzima wa zoezi hili karani ndo mtu wa mhimu zaidi kuliko wote , yeye ndo anashuhudia Kwa usahihi what is real going on na kipi ni sahihi na wapi pa kurekebisha ,

Nipongeze serikali Kwa kuja na idea Bora zaidi ya kuendesha zoezi hili na Kwa kweli likifanikiwa hata Kwa 80% serikali itakuwa imekula bingo , aliyeleta mchakato Kwa idea hii nampa salute ,

Hata hvyo mchakato ni costful , Kwa haraka more than 600tsh billion zitaperish away kwenye huu mchakato , hela nyingi Kwa nchi hii ya kimaskini ...

In reality zoezi ni gumu hasa , linahtaji angalau semi skilled workers with high commitment , Viongozi wa ngazi za juu wamehamasisha Kwa nguvu zote huku mzigo mzito akiangushiwa karani , ...

Kwa maoni yangu makarani wengi mbali na kufanya kazi ya kuchosha bado Wana moyo wa kufanya na mwitikio ni mkubwa , tatizo ni matumizi ya software ya CS entry kwenye tablet , hii ni changamoto kubwa sana

Baada ya kufanya mazoezi changamoto hii imeonekana kuwa ni deadliest na itaharibu mchakato mzima kama haitafanyiwa kazi , nasema haya Kwa moyo wa kizalendo kabisa , makarani tulileta taarifa na tatizo kubwa karbu Kwa makarani wote ni hii software hasa matumizi ya ramani na uwepo wa GPS.

Imagine karani umetembea Kwa moyo mmoja mpak kwenye Kaya fulan mlimani , umefika unammkuta mama anafua akakupokea Kwa moyo mmoja akaacha kazi yake, ukatazama ramani ukajihakikisha GPS inasoma kwenye ramani , ukafungua dodoso la Kwanza , akaanza kukupa taarifa za waliolala kwenye Kaya ambao ni 12 , takriban masaa mawili umekaa naye akikupa taarifa , umemaliza unatafuta majira unapata , unasave unajikuta imesave nje ya ramani , .....!! Kwa mjibu wa Sensa hyo kazi yote inakuwa ni useless ,unatakiwa uende Kwa msimamizi ufute kazi yote akutumie mchakato upya na uende tena kwenye Kaya hyo uanze mahojiano upya ,

Cahangamoto zaidi inakuja kama Kwa sku nzima umehoji kaya 10 , na kaya 9 zote majira nukta (GPS ) yamesoma ndani ya ramani na moja imesave nje ya ramani Kwa mfumo wao wa software , hzo kazi zote zinakuwa invalid inabdi ufute kazi zote uwekewe kazi upya na uende ukarudie mahojiano upya kwenye Kaya zote , na endapo itatokea the same scenario , itabd ufute tena uanze upya .. ni kazi ngumu na ya kuchosha hasa kipindi hiki cha kiangazi , na kimbembe ni kuwa maeneo mengi karani ni mmoja Kwa kila kitongoji , ni mzigo mzito sana...ni uzalendo tuu utakaofanikisha hili zoez and not otherwise

Nawaambia live hakuna karani atakubali kufanya such kind of fucking process , tegemeeni data za kupikwa na zoezi Zima litapoteza maana ...

Tulileta mrejesho tukiwa na option Bora za kuboresha mana lengo ni kufanikisha , nikashangaa IT wa wilaya anajibu shit bila kujua Kwa undani hyo critical condition huku akitutisha makarani , ....

Kwa Sisi ambao tuko kwenye battle field tukawaambia wakubwa wetu kuwa huko juu ma IT wa Taifa wakeshe kuhakikisha wanaboresha hyo application ili iwe na option zifuatazo :-

1. Wakati ninahoji Kaya basi kuwe na signal kwenye tablet kama dot hvi au whatever yenye rangi ya kijani ili kuni-alert kuwa GPS inasoma ndani ya 3 meters kutoka pale nilipo...na kama sivyo ionyeshe rangi nyekundu kunitahadharisha kuwa GPS inasoma wrong place hvyo nifanye mchakato wa kuiweka Sawa

2. Option ya pili , in case ikatokea Kaya moja nimesave nje ya ramani , na Kaya zingine let say Kaya 10 zimesave ndani ya ramani basi kuwe na option ya kuiweka pending hyo Kaya moja , ili zingine niweze kuzituma alaf iliyozingua hyo moja ndo nirud badala ya kuzifuta zote na kuanza upya ....

Cha Kushangaza IT alisema tusitegemee option za namna hzo Bali tuongeze umakini,
Changamoto iliyopo ili GPS isome mahali uliopo unahtaji ufate step zaidi ya tano , hapo bado accuracy yake ni 70 % bado lolote laweza kutokea , na pia ni ngumu kufanya kazi kuanzia asubh mpak jioni ukafanya Kwa usahihi , kuna kujisahau ukapata error hyo , Yani hakuna option ya kurekebisha hyo moja, bali data zote zinakuwa nullified ....

Kama Hali ikiendelea hv , nini makarani wataenda kufanya , nimeenda let say Kaya X , nimehoji nikaambiwa wanakaya wamelalal 13 , nikajikunja kizalendo karbu hata masaa 2 au 3 kupata data Kwa usahihi , zen ikasave nje ya Raman , kurud tena Kwa mwanakwaya Yule umuachishe tena kazi yake ni bonge la nouma , nitakachokifanya nafuta hyo kazi sahihi , badala yake naenda kwenye hyo kaya nasimamia nje getini , napika data , ili nisichoke najiandikia watu 2 wamelala pale , ili nisave nitoke , na hzo tayar zinakuwa data ambazo ni invalid ...

Na hii kwenye mazoez watu wamefanya Sana , dada mmoja kahoji Kaya ya Kwanza ikasoma ndani ya ramani , nakahoji ya pili ikasoma nje , ikabd afute msimamizi amwekee kazi na Raman upya , akahoji tena moja ikakubali nyingine ikasoma nje , dada alitaman kulia , akaenda Kwa msimamiz akafutiwa kazi na kuweka ramani upya , dada alichokifanya akaenda sehemu akapika data , zikasoma ndani ya ramani akaleta Kwa msimamizi akapokea akatuma makao makuu data ambazo ni invalid ....

Mlioko juu jitahdini hili tatizo mlitatue , la sivyo huko kwenye viyoyozi , hao viongozi walioko huku wanawadanganya kuwa zoezi lipo poa but in reality ,ni disaster inaenda kutokea .....
View attachment 2323556
Kuna maswali niliwahi kumuuliza Kamishna wa Sensa mama Anne Makinda. Swali lilikuwa usahihi wa taarifa kuwiana na teknolojia iyakayotumika. Nikitaka kufahamu ufahamu wa wakusanya taarifa.

Nakumbuka niliwahi kushiriki zoezi la pilote la anuani za makazi ambapo mimi nilikuwa layman lakini kwenye zoeI maafisa wa Manispaa waliingia mitini kwa sababu ya kushindwa kuelewa wanafanya njni.

Ukweli ni kwamba. Wangekusanya taarifa mannual huku wakiwa na GPRS device kuweka pin ya kila kaya na kujaza coordinates kwenye data sheet.

Kisha waajiri waingiza data ambao watajaza datasheets na kuunganisha coordinates kwenye server


Mungu awasaidie kwa kweli. Na sijui malipo itakuwaje
 
Tatizo ni moja tuu, hivyo vishikwambi vinatumia offline map, waandaaji wa hili zoezi wangeweka programu yenye kutumia data badala ya offline map.
Upande wa Map ndo mizinguo, ningependa sana nitumie simu yangu kuliko kishikwambi maana kwa simu inapiga kazi saafi kabisa maana nawasha data all time na zote zinasoma ndani ya EA.
Hiyo ndiyo isiyotakiwa sasa! Kumbuka intaneti inatumika kuboost tu ili ramani isomeke (ifunguke) basi baada ya hapo unahitajika kufunga data... tatizo hamsomi hata miongozo halafu mkiharibikiwa mnakuja kulialia hapa
 
Mi nafikri muwe na alternative. Kidigitali ikifeli mnaswitch analogy. Yani shkwambi likizingua unachukua kabrasha lako unajaza. The only way forward
 
UV CCM waliojazana humo tunatarajia hayo yakupika data yatokee ..enewei hata hivo hakuna wa kujali chochote kwenye nchi hii...pika data chukua chako maisha mengine yaendelee..Hilo li application nasikia NI la marekani..
 
thubutu! IT wa Bongo hawana huwezo huo,
ni system za ki-paskitani izo, so kuomba marekebisho mpaka yafanyike ni miezi kadhaa ipite
Kumbe ndio maana unawaletea shida watumiaji wa mfumo maana mfumo unabidi utengenezwe kuendana mazingira ya eneo husika na pia kwa kua mfumo unatengenezwa na team ya programmers/developers inabidi ufanyiwe testing kadhaa kila hatua ya uundwaji wa mfumo inabidi ufanyiwe majaribio kuthibitisha kua unafanya kazi bila kuleta shida kwa mtumiaji na hio team ijiridhishe kua mfumo upo sawa hauleti errors/bugs zozote au mfumo hauna complications zozote kwa mtumiaji yaani utamrahisishia mtumiaji kuifanya kazi yake pasina kutumia nguvu na akili mingi na pia team ijithibitishie kua mfumo hauna shida yoyote kabla haujakabidhiwa kwa mteja/mtumiaji husika kwamba unafanya kazi kwenye mazingira yawayo yoyote ya mtumiaji/mteja pasina kuleta shida yoyote, swali km mfumo umetengenezwa na ma IT wa Pakistani from scratch (code after code) na unahusu mazingira ya Pakistan je! Wakati mfumo unatengenezwa ulifanyiwa testing (majaribio) aidha na ma IT wa bongo au wa Pakstan kwamba kwenye mazingira ya bongo huo mfumo unaweza kufanya kazi bila kunaleta errors zozote kwenye haya mazingira au ndio wuacha tu tununue tutajua mbele ya safari?

Nawasilisha..
 
Mkuu hyo Kaya ina wanakaya 30 , maswali Kwa kila mwanakaya ni Kati ya 70-100 kulingana na umri , jinsia na shughuli za kiuchumi , na ili upate data Kwa Usahihi hapo itakulazimu ukae masaa si chini ya matatu mpak ma nne , na hap umekabidhiwa kitongoji kizima na sku za kuhesabu ni sita tuu
Vitongoji wangewaza fanya kazi hii kwa ufanisi zaidi. Nyie mngeenda chukua taarifa kwao.
 
Back
Top Bottom