Witness from the front line: Hili zoezi la sensa mlioko juu msiporekebisha haya kwa haraka tegemeeni taarifa mbovu kuwahi kutokea

Nikupongeze mkuu,ila changamoto ya gps kusoma nje ya eneo fanya hivi kwanza fungua ramani husika na angalia gps ambayo inatambulisha kishkwambi chako kama kiko ndani ya EA/eneo lakuhesabia then nenda kwenye location kwa sekunde 3 bila kuachia chagua location service then google accuracy weka off baada ya hapo rudi kwenye kazi haiwezi kuhama tena
 
TOKA WANILE KICHWA NA KUPEANA NAFASI KWA KUJUANA NA SI VIGEZO TOKA HIYO SIKU NAMUOMBA MUNGU ZOEZI LISIFANIKIWE
 
Absolutely, na pia naskia wametoa mwongozo endapo ikatokea by mistake moja ikasave nje unatuma hvyo hvyo zote , nafkr wataleta mrejesho badae nini kifanyike
 
Umejihangaisha bure kumwandikia makala/waraka huyu... nimwemwambia aje inbox kama kweli ana tatizo la ramani lakini hajathubutu na ni bora ameshtuka maana ningemuumbua tu
 
Hii akili sijui ya wapi wandugu!?

Yaani mkajua sensa ni kujua namba ya watu tu
 
Mkeo na wengi kama yeye ni vichwa maji hawasikilizi (hawaelewi) mafundisho ya darassani halafu wakirudi nyumbani wanataka msaada kwa watu ambao hamkwepo kwenye mafunzo... kinachofuata ni lawama na kejeli
 
Unajua hizi Garmin GPS, kama hamjapata latest version basi ujue error yake ni mita 2 mpaka 3. Na kama unavyosema lazima uiwashe ukiwa eneo la wazi nje, mfano mkifika kwenye nyumba pale mlangoni kwa nje ili iweze kudaka walau satellites zaidi ya 4 ndiyo utapata correct readings. Kwa case ya msituni pia kuna Garmin gps version ambayo iko vizuri na inakupa error ya mita 2 hata ukiwa chini ya miti. Pia kuna smartphones zenye GPS nzuri na zenye error mpaka nusu mita.
 
Ili upate hiyo gps, internet ya simu ndio inatumika? Namaanisha muda wote internet inatakiwa kuwa ON?
Iko hivi GPS ni kifaa (global positioning system) ambacho Kazi yake ni kuchukua points za eneo husika (coordinates). Kwa mfano ukienda msituni na gari au bodaboda ukaiacha na kuamua kutembea humo porini kwa mguu wakati wa kurudi unaweza kupotea na usijue gari mmeacha wapi. Hivyo ukiwa na gps pale ulipoacha gari unabonyeza kama vile unavyoweka alarm kwenye simu halafu unasevu kwa hiyo GPS. Sasa wakati wa kurudi hiyo GPS inakuongoza mpaka ulipoacha gari. GPS hutumia betri ndogo kama za rimoti na wala haihitaji internet. Lakini kuna smartphones ambazo zina GPS au kama hazujawekwa unaweza ku downloads... Mfano unaweza kuset kwenye simu yako kwamba kila ukipiga picha inachukua na coordinates za eneo husika moja kwa moja. Ndiyo maana naona kuna mapungufu kwenye mfumo wao wanaotumia kwa sababu wangeweza kabisa kupiga picha ya kaya husika na at the same time wakapata gps location ya hiyo kaya (coordinates).
 
Mkuu unaweza kutengeneza map kwenye computer halafu baadae ukai upload kwenye hizo tablets na wakatumia bila internet. Wakitegemea internet watachemsha kwenye maeneo yasiyo na mtandao
 
Soma tena nilichouliza. Hao wanatumia tablet ambayo ndani yake ndio Kuna mifumo ikiwemo hiyo ya gps, ndio nauliza wanatumia internet?
 
Mkuu unaweza kutengeneza map kwenye computer halafu baadae ukai upload kwenye hizo tablets na wakatumia bila internet. Wakitegemea internet watachemsha kwenye maeneo yasiyo na mtandao
Unatoa ufafanuzi wa jambo ambalo hujalielewa.
 
We kijana pika data ,kula posho endelea na mambo mengine unajichosha bure
Anapikaje data wakati anatakiwa kuchukua coordinate kwenye kila kaya?? Apike coordinate?? [emoji12] [emoji12]
 
Nchi ishapikwa na viongozi muda mrefu sasa ni muda wa wananchi kwenda kupakuliwa!
 
Mi nafikri muwe na alternative. Kidigitali ikifeli mnaswitch analogy. Yani shkwambi likizingua unachukua kabrasha lako unajaza. The only way forward
Vipi coordinates za kaya atazipataje bila kutumia gps iliyoko kwenye Tablets?
 
Mkuu techniques za kufanya sensa ni the same world wide... Hivyo kama Pakistan walitengeneza huo mfumo na wametumia kwenye sensa huko kwao au kwa nchi nyingine, probably za Afrika au Asia, mbona haina shida kabisa? Imagine mpaka jezi tuu za Simba na Yanga tunatengenezea nje ya nchi [emoji23] [emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…