Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Tunaposhukuru kwa kila jambo hatuna budi kuyakubali yote yanayotusibu, mazuri na hata mabaya tusiyokuwa na uwezo nayo. Hata hivyo si kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wetu.
Majuzi kati tumeondokewa na mzee wetu Rais mstaafu (RIP), jambo la kusikitisha sana, hatuna jinsi, bali kulikubali kama lilivyotusibu. Tushukuru kwa yote ikiwamo pia kwamba hatimaye tumempumzisha mzee wetu salama.
Kwa upande mwingine majuzi kati pia, mtanzania mwenzetu aliyefufuka kutoka katika wafu, alirejea nyumbani salama akipokelewa kwa nderemo na vifijo. Jambo la kheri kabisa. Kweli mola ndiye aliye mkuu sifa zote na utukufu zimrejee yeye.
Ajabu na kweli, amani na upendo vilivyotamalaki vilivyo kwenye matukio mawili haya, vimewaacha wengine na aibu, chuki, husuda na hata hasira kali isiyokuwa na sababu. Kwa hakika hawa ndiyo walio na adui zetu. Hawatutakii mema.
Tusiwaache watu wa namna hii (bila kujali walipo wala nafasi zao) bila ya kuwakemea.
Tuwapongeze wote ambao, (wakati maadui zetu wakitusubiria tutoane roho) walipata nafasi ya kutuwakilisha vilivyo katika matukio haya JKNIA, Uhuru au Lupaso.
Kwa hakika mliwatukilisha Watanzania wenzenu vilivyo na mmetutoa kimasomaso kweli kweli.
Washindwe maadui zetu na walegee!
Kwamba labda hukupata nafasi ya kufika? Hiyo siyo tatizo. Mazingira, nafasi, fursa, majukumu, nk hayawezi kuwa sawa kwetu sote na kwa wakati wote.
Nia njema na dhati yake ndiyo ulio msingi pekee muhimu kwetu sote, kama Watanzania. Kwa waungwana hayupo mmoja aliyefanya vyema zaidi katika haya kuliko mwingine. Hukufika kote, ulifika kumoja, ulifika kote, nk. Kongole kwako na shukurani nyingi kwa kutuwakilisha.
Kama nia ilikuwa mbaya, badilika mwenyewe. Vinginevyo wazalendo wenye moyo watakubadilisha!
Chonde chonde taifa hili ni zaidi mno ya mtu mmoja au kundi lolote liwalo lile.
Watu wasiotutakia mema na bila ya kuangalia makunyanzi yao ni muhimu sana kuwapa makavu na bila ya kupepesa macho.
Hivi vikundi vikundi vya watu vinavyojitokeza tokeza kwa nia ovu, visiachiwe kutuvuruga.
Katikati ya matukio mawili haya, bila ya haya wamejitokeza hata wenye kudai kuwa fulani hawezi kupata wadhifa fulani bila ya ridhaa yao. Eti bila hata kujali matokeo ya kura. Ajabu na kweli, wanasema ikibidi hata masanduku ya kura hukimbia nayo.
Si wa kuwafumbia macho hawa.
Bila kujali itikadi zetu na kwa umoja wetu, watu hawa ni wa kukemewa vilivyo. Chelewa chelewa utakuta mwana si wako. Kwa hakika wanakotaka kutupeleka siko.
Tanzania ni mali ya watanzania na kila mmoja wetu ana haki sawa. Hayupo yeyote aliye na haki zaidi katika lolote lihusulo ustawi wa nchi hii.
Washindwe na walegee.
Mungu ibariki Tanzania!