- Thread starter
- #21
Maadui gani unaowazungumzia?
Maana sisi twajua ujinga, umaskini na maradhi ndio maadui zetu. Je, hawa ndio unaowazungumzia?
Kuna na wengine pia. Maadui siyo hao tu ulioorodhesha mkuu. Wa hapa pia hujulikana kama maadui wa ndani na wa nje.
Hawa si nadharia bali ni watu. Bin Adam kabisa. Machoni wako kama watu. Sheshe rohoni. Bora ya shetani.
Utawajua kwa silika zao.
Kwamba wamekereka mno kwa kuwa tumemzika marehemu wetu kwa amani au kuwa mwenzetu aliyekuwa katutoka amerejea?
Eboo! Binadamu wa namna gani hawa wenye kufanya tafrija binadamu wengine wanapotoana macho na roho pasipokuwa na sababu?
Hawa ndiyo wenye kukaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune.
Pumzika kwa amani Jabali la Muziki.