Wito: Chonde chonde, Tanzania ni zaidi mno ya yeyote

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
34,775
Reaction score
46,063
Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.

Tunaposhukuru kwa kila jambo hatuna budi kuyakubali yote yanayotusibu, mazuri na hata mabaya tusiyokuwa na uwezo nayo. Hata hivyo si kwa yale yaliyo ndani ya uwezo wetu.

Majuzi kati tumeondokewa na mzee wetu Rais mstaafu (RIP), jambo la kusikitisha sana, hatuna jinsi, bali kulikubali kama lilivyotusibu. Tushukuru kwa yote ikiwamo pia kwamba hatimaye tumempumzisha mzee wetu salama.

Kwa upande mwingine majuzi kati pia, mtanzania mwenzetu aliyefufuka kutoka katika wafu, alirejea nyumbani salama akipokelewa kwa nderemo na vifijo. Jambo la kheri kabisa. Kweli mola ndiye aliye mkuu sifa zote na utukufu zimrejee yeye.

Ajabu na kweli, amani na upendo vilivyotamalaki vilivyo kwenye matukio mawili haya, vimewaacha wengine na aibu, chuki, husuda na hata hasira kali isiyokuwa na sababu. Kwa hakika hawa ndiyo walio na adui zetu. Hawatutakii mema.

Tusiwaache watu wa namna hii (bila kujali walipo wala nafasi zao) bila ya kuwakemea.

Tuwapongeze wote ambao, (wakati maadui zetu wakitusubiria tutoane roho) walipata nafasi ya kutuwakilisha vilivyo katika matukio haya JKNIA, Uhuru au Lupaso.

Kwa hakika mliwatukilisha Watanzania wenzenu vilivyo na mmetutoa kimasomaso kweli kweli.

Washindwe maadui zetu na walegee!

Kwamba labda hukupata nafasi ya kufika? Hiyo siyo tatizo. Mazingira, nafasi, fursa, majukumu, nk hayawezi kuwa sawa kwetu sote na kwa wakati wote.

Nia njema na dhati yake ndiyo ulio msingi pekee muhimu kwetu sote, kama Watanzania. Kwa waungwana hayupo mmoja aliyefanya vyema zaidi katika haya kuliko mwingine. Hukufika kote, ulifika kumoja, ulifika kote, nk. Kongole kwako na shukurani nyingi kwa kutuwakilisha.

Kama nia ilikuwa mbaya, badilika mwenyewe. Vinginevyo wazalendo wenye moyo watakubadilisha!

Chonde chonde taifa hili ni zaidi mno ya mtu mmoja au kundi lolote liwalo lile.

Watu wasiotutakia mema na bila ya kuangalia makunyanzi yao ni muhimu sana kuwapa makavu na bila ya kupepesa macho.

Hivi vikundi vikundi vya watu vinavyojitokeza tokeza kwa nia ovu, visiachiwe kutuvuruga.

Katikati ya matukio mawili haya, bila ya haya wamejitokeza hata wenye kudai kuwa fulani hawezi kupata wadhifa fulani bila ya ridhaa yao. Eti bila hata kujali matokeo ya kura. Ajabu na kweli, wanasema ikibidi hata masanduku ya kura hukimbia nayo.

Si wa kuwafumbia macho hawa.

Bila kujali itikadi zetu na kwa umoja wetu, watu hawa ni wa kukemewa vilivyo. Chelewa chelewa utakuta mwana si wako. Kwa hakika wanakotaka kutupeleka siko.

Tanzania ni mali ya watanzania na kila mmoja wetu ana haki sawa. Hayupo yeyote aliye na haki zaidi katika lolote lihusulo ustawi wa nchi hii.

Washindwe na walegee.

Mungu ibariki Tanzania!
 
Nimerudia zaidi ya mara moja, iwapo wapinzani watahakikisha matokeo halali yanatangazwa popote, basi rais huyu ndio ataingiza nchi hii kwenye machafuko, akiamini yeye na watoa rushwa wa chama chake, ndio wana uhalali wa kukaa madarakani.
 
Utanzania wetu ni tunu isiyo na mfano.

Kusaidiana na kuwasaidia wote wanaoshindwa kuuona ukweli huo kwa hoja bila ya kujali makunyanzi, ni wa wajibu wa kila mtanzania na hasa aliye Mzalendo.

Tusiwaonee haya watu wanaohubiri shari badala ya utangamano, amani na maridhiano. Mtanzania ni mwenye kusamehe. Tusameheane na tuijenge nchi hii ukweli na haki viki tamalaki.

Misahafu inasema pasipo na kumung'unya maneno:

"Blessed are the peacemakers: for they shall be called the children of God. ... for they will be called sons of God."

Kinyume cha hapo kipo wazi.

Tunapojitanabaisha kuwa we are for the people na iwe hivyo kwa dhati kabisa na kwa vitendo.
 
Wa kuleta fyoko, Adililwe haswaa, Amani Kwanza!

Unaona umedhurumiwa, itafute haki yako kwenye Vyombo vinavyotoa haki
 
Kuna mtu mmoja amechafua hali ya hewa huko Kilwa.

Huyu ndo miongoni mwa wasioitakia mema Tanzania yetu kwa kukiuka matakwa ya katiba.

Mkuu ninaziona hisia zako na machungu ya wazi yaambatanayo na kauli yako. Sisi sote ni binadamu na waja wake maulana. Hakuna aliyemkamilifu 100%.

Kuvunjika kwa koleo siyo mwisho wa uhunzi. Na ni kwa kusameheana x7x70 ikibidi ndiko kutakako tuvusha sote salama kama taifa.

Kama binadamu wastarabu, tukubali kusameheana na kusahau (reconciliation).

Kuna huu uzi hapa:

Muda wa kuiponya nchi yetu ni sasa

Ninaamini uzi huu kwa hakika unatuhusu sana sasa labda kuliko wakati mwingine.

Tusipoyafanya haya sisi wenyewe sasa historia itakuwapo kutuhukumu.
 
Hahaha kuna kijiwe hapa wanaomba msiba mwingine wa kitaifa waomboleze mwezi mzima, wanasema wamechoka kelele, kulikuwa kumepoa sasa kaanza, sasa sijui nani afe.
 
Hahaha kuna kijiwe hapa wanaomba msiba mwingine wa kitaifa waomboleze mwezi mzima, wanasema wamechoka kelele, kulikuwa kumepoa sasa kaanza, sasa sijui nani afe.

Kwa hakika, kijiwe cha wachawi wenye kuombea misiba hakikuwapo Uhuru, JKNIA, Lupaso wala kokote, kuwawakilisha watanzania kwa dhati yao physically wala morally.

Wala kijiwe hicho hakipo hapa.

Hatuwezi kujidanganya kuwa kila kitu ni salama na kuwa maadui zetu waliochukizwa na salama na amani iliyotamalaki JKNIA, Uhuru na Lupaso chuki zao na hasira zao zimekwisha sasa.

Jitihada zao za kuchochea na kuhamasisha chuki na mihemuko isiyokuwa na tija ili tutumbukie kwenye misiba inapaswa kukemewa.

Kwa yaliyotokea katika sehemu tatu hizi ni ushahidi wa wazi kuwa watanzania walio wengi hawataki shari wala makabiliano.

Tunapomwachia mola yaliyoko nje ya uwezo wetu, hatuwezi kuwasabiria wao yaliyoko katika uwezo wetu kiasi cha kutuletea misiba, hata kwa kuwakemea tu.
 
Magufuli tutamkumbuka kwa mambo mengi sana baada ya urais wake.

Hatuwezi kujidanganya kuwa kila kitu kipo sawa bin sawia.

Hata hivyo, badala ya kusubiria kukumbukana kwa mengi peke yake, tunaweza kushirikiana sote kwa umoja wetu tukaja kukumbukana kwa mengi yaliyo mema.

Hakuna aliyemkamilifu. Misahafu inatufundisha kuwepo kwa mrejesho mbele za haki na sote kabisa kila mmoja kivyake vyake atawajibika.

Heri yao wapatanishi. Ole wao wenye kukaanga mbuyu.

Sote tuna wajibu hayupo wa kujitia utazamaji.

Anasema George Bush "You are either with us."

Tusiwe watazamaji wala wenye kukaanga mbuyu. Tukawa wapatanishi.
 
Baki na Bwege wenu

Kujikwaa si kuanguka mkuu. Mengine u ngosha na kiswahili nayo changamoto nyingine.

Tunapokubali kusamehe x7x70 tujiandae pia kujikwaa x7x70.

Tanzania ni moja lakini kuu kuliko sote.
 
Kujikwaa si kuanguka mkuu. Mengine u ngosha na kiswahili nayo changamoto nyingine.

Tunapokubali kusamehe x7x70 tujiandae pia kujikwaa x7x70.

Tanzania ni moja lakini kuu kuliko sote.
Kumfichia maovu mtu ni jinai kwakweli
 
Kumfichia maovu mtu ni jinai kwakweli

Tunaitishwa kusameheana.

Tunaitishwa hata kuwapenda adui zetu.

Hekima ni nyingi tulizonazo katika jamii zenye nguvu na uwezo wa kurejesha silaha alani.

Hatujafikia kwenye point of no return. Tusijiachie kutumbukia huko. Hayupo atakaye kuja kutugombelezea.

Tunaweza kuganga yajayo hasa kila upande ukiwadhibiti wakereketwa wao ambao aghalabu wasiendelee kuukaanga mbuyu na kuwaachia wengine kutafuna.
 
Kuna mtu mmoja amechafua hali ya hewa huko Kilwa.

Huyu ndo miongoni mwa wasioitakia mema Tanzania yetu kwa kukiuka matakwa ya katiba.
Na mapiga meza Dodoma yalipitisha sheria asishitakiwe kwa lolote hata kama anainajisi katiba atakavyo.
 
Maadui gani unaowazungumzia?

Maana sisi twajua ujinga, umaskini na maradhi ndio maadui zetu. Je, hawa ndio unaowazungumzia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…