Wito: Chonde chonde, Tanzania ni zaidi mno ya yeyote

Maadui gani unaowazungumzia?

Maana sisi twajua ujinga, umaskini na maradhi ndio maadui zetu. Je, hawa ndio unaowazungumzia?

Kuna na wengine pia. Maadui siyo hao tu ulioorodhesha mkuu. Wa hapa pia hujulikana kama maadui wa ndani na wa nje.

Hawa si nadharia bali ni watu. Bin Adam kabisa. Machoni wako kama watu. Sheshe rohoni. Bora ya shetani.

Utawajua kwa silika zao.

Kwamba wamekereka mno kwa kuwa tumemzika marehemu wetu kwa amani au kuwa mwenzetu aliyekuwa katutoka amerejea?

Eboo! Binadamu wa namna gani hawa wenye kufanya tafrija binadamu wengine wanapotoana macho na roho pasipokuwa na sababu?

Hawa ndiyo wenye kukaanga mbuyu na kuwaachia wenye meno watafune.

Pumzika kwa amani Jabali la Muziki.
 
Na kumfukuza kazi Mwampamba kwa kutongoza wake za watu.

Usitake ncheke.

Lazima kukubali hali yetu inaweza kuwa ni tete zaidi.

Inawezekana kuwa tumeshafika mbali sana kama si kufika kwenye talaka rejea kabisa.

Hata hivyo one extra mile bandugu. Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Silaha tuzirejeshe alani, turudishe majeshi nyuma tujaribu tena kwa njia nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…