Wito: CJ Prof. Ibrahim Juma, make a historia kwa Mahakama kutimiza wajibu wake kulinda haki. Tumia Suo Moto kui-check Serikali pia ruhusu Pro Bono

Umesahau ule mhimili ambao m mizizi yake iko chini zaidi?
 
Ki ukweli tumerudi nyuma katika utawala bora. Disgraceful leaders, inakera sana mambo mepesi wanatumia akili za dunia ya wapi sijui.
 
Nakubaliana na wewe, hasa tukianza na hoja namba 2
Huwa nashangaa watu wanaposema tusijadili kesi iliyopo mahakamani tutaharibu ushahidi na mwenendo, yaani ni kama vile mahakama huwa inasikiliza maoni ya wadau mtaani ndio ifikie maamuzi yake.

Hoja ya kwanza, ni kweli haiwezekani mahakama kuibuka tu na kutoa amri wakati hakuna kesi mbele yake, lakini mahakama ina uwezo wa kutumia sheria zilizopo kufuta kesi ambazo upelelezi wake haukamiliki. Badala ya kuwa majaji na mahakimu kuwa wakali na kushambulia serikali kwenye ruling ingekuwa inazifuta tu kwa mujibu wa sheria, hapo ingejionesha kuwa ipo huru tofauti na sasa ambapo ni kama inabariki huo uonezi.

Hapo kwa mfano wa mtu wa Mlele (remote area), ni kweli kabisa baadhi ya mahakimu wanazingua sana kujifanya hawapo maeneo hayo. Yaani wanamchukulia mtu katika kesi kwa mazingira ya Dar es Salaam. Ukishindwa kureason katika mambo obvious, hutaweza kureason katika mambo magumu kwenye hukumu zako.
 
Nje kidogo ya mada. Wahadhiri huwa wanazingua sana kuchezea maisha ya watu ili tu kuonesha ubabe wao.
Inaumiza sana, na ukifuata sheria walizozitunga wenyewe kutafuta haki yako unaonekana jeuri. Anachezea maisha kwa miaka 2 au 3 na anaona kawaida tu
 
Leo umelenga lila mtu aelewe .Pascal I must know you in personal huniangushagi toka 2012
 
Nimeshtuka mwanasheria kumuita mzungumzaji Mmoja kuwa ni kichaa. Ungeweza kuandika bila kuweka hilo neno.

Pro bono kwa katiba hii yetu na sheria hizi?

Mashauri yatakuwa mengi na serikali itaonekana haiwajibiki kwa wananchi hasa juu ya Ustawi wetu.

Unakumbuka hii

" imperial executive"

Hakuna wa kumdondosha isipokuwa kura ya maamuzi.

Pole kwa kusononeka juu ya nchi hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…