Wito kwa Malinzi ajiuzulu

tanzania mchezo wetu bao tu, mpira tuwaachie wenyewe.
 

Kumfukuza kochha sio ishu...Ishu ni yeye mwenyewe aondoke...Watu wapya waingie na new thinking.....Kumtimua kocha na kumuacha malinzi ni sawa na kuweka mvinyo mpya kwenye chupa ya zamani
 

hizi ndio bangi malinzi ndio anacheza je tanzania mashindano hayo tumewahi kufanya vizuri mara ngapi
 
Kila mzungu anaweza kuwa kocha wa taifa star hata michezo ameisoma kwenye gazeti naomba mechi ijayo tufungwe goli 7-10
 
Kwa TFF hii na chaguo lao (kocha huyu Nooij) tutafungwa... na nasema tufungwe tu... maana hakuna namna nyingine.
 
nyie si ndio mlimsifia sana wakati anachaguliwa, endeleeni kuugulia maumivu ya vipigo kila siku.

siku hizi sitaki hata kujua stars kacheza na nani sembuse matokeo yake.

Njoo huku tushabikie TWANGA PEPETA
 
Kila mzungu anaweza kuwa kocha wa taifa star hata michezo ameisoma kwenye gazeti naomba mechi ijayo tufungwe goli 7-10

7-10 tu, mimi nataka 1-100
 
mi sioni sababu ya kujiuzulu ila walaumiwe wale waliomchagua wengine hata kabla ya kuchaguliwa tulijua hawezi kuleta mafanikio kwani historia yake ya uongozi inajieleza toka akiwa yanga
 

Mkuu, kwa tanzania kujiuzulu ni ndoto, hata mtu awe muuaji, atagoma tu... uwajibikaji sio lugha yetu

Kuanzia kwenye family hadi ikulu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…