Mkuu toka lini ukaona mkuu wa shirikisho la mpira akajiuzuru kisa timu imefungwa?
Hapa wakulalamikiwa ni wachezaji , hata angekuwa Morinho hii timu kufungwa ingefungwa tu.
Wapeleke maombi FIFA wasipangiwe mechi yoyote ndani ya miaka miwili ili wajitazame kwanza
Nadhani issue si kujiuzuru anatakiwa aoneshe kuchukizwa na matokeo haya na achukue hatua Amfukuze huyu Kocha mara moja amrudishe Kim Poulsen haraka sana aichukue timu kujiandaa na mechi ya Nigeria na kwa Kim itakuwa kazi rahisi maana sehemu kubwa ya wachezaji wenye viwango vya kuchezea Taifa Stars kipindi hiki kawatengeneza yeye.
Wametuaibisha vya kutosha njee ya mipaka ....sasa basi kikosi kiandaliwe upya na hakuna ulazima wa kumleta kocha kutoka njee watafute mvawa apewe majukum,Na hata hawa wachezaji wetu sidhani kama kuwalaum ni dawa hawa wamezidiwa uwezo.Kikosi kisukwe upya hili ndio muhimu na tujitoe kwenye mashindano ya kimataifa kama miaka 2 hivi tujipange ama sivyo tutakuwa mabingwa wa kutoa point kwa wenzetu
Kama sio 20%Nahisi Malinzi anakula 10% mshahara wa Nooij
Kudadadeki Malinzi cjui kwann alimfukuza KIM aisee. Naamini saivi national team ingekuwa inajiamini sana na ingetoa upinzani stahiki kwa wapinzani.
Kocha wa Mwisho kuifundisha Stars alikuwa Marcio Maximo
Mkuu upo sahihi, kipindi Maximo anainoa taifa starz kila mtanzania alikuwa na hamasa ya kuishangilia timu ya taifa,Sina uhakika....ila ukweli ni kwamba maximo alileta mwamko wa watu kuipenda timu yetu...Kim alikuwa anaweka misingi ya soka...na mazao yalianza kuonekana...Timu ilikuwa inaeleweka.....ilikua unaweza kuitegemea kushinda