Ndio Salim alipata zahama kubwa sana 2005 na kuna sababu zake.
Tukumbuke huko nyuma Salum alituhumiwa na SMZ kushiriki mauaji ya Mzee Karume. Wakati akiwa mwakilishi UN alitakiwa aende Zanzibar kwa mahojiano na vyombo vya usalama Mwalimu Nyerere akamkingia kifua hasa Kutokana na yaliyowatokea wakina Mzee Hanga huko nyuma. Mwalimu alitaka vyombo vya usalama vya Zanzibar vifanye mahojiano na Salum hapa DAR na SMZ ikakataa. Tangu hapo katika macho ya SMZ ndugu Salim Ahmed Salim hajawahi kujisafisha kuhusu mauaji ya Mzee karume pamoja na kwamba SMZ ilikubali "yaishe". This is Salum's greatest political weakness.
Ndio maana 1985 baada ya Mzee Rashi Kawawa kukataa kumrithi Nyerere kwa sababu za kiafya pamoja na Nyerere kumtaka Salim aingie Ikulu wajumbe wa Kamati Kuu toka Zanzibar wakiongozwa na Marehemu Natepe
waliweka pingamizi kubwa sana. Pingamizi hili ndilo lililomuweka Mzee Mwinyi kwenye Urais 1985.
Ya 2005 wote tunayajua. pamoja na nguvu ya mtandao kumchafua Salum hilo halikuwa sababu muhimu sana. Sababu kubwa ni kwamba Salim hana support ya CCM kutoka Zanzibar. In other words he has no real consituency. Inasemekana kwamba karibu kura zote alizopata Salum kwenye mchakato wa Urais kwenye Halmashauri ya CCM zilitoka bara. Hata tukirudi nyuma kidogo wakati Makamu wa Rais Dr. Omar alipofariki ghafla wengi tulitegema Rais Mkapa amteue Dr. Salim (alisharudi toka OAU) kuwa makamu wake, lakini wapi? Kama angekuwa Mwalimu Nyerere angefanya lakini Mkapa hakuwa na ubavu huo.
Katika siasa za Tanzania na hasa Zanzibar, CCM kumteua Dr. Salim kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM ni kama ndoto za Alinacha! Na baada ya 2005 Salim analijua hilo.
Wakati mwingine jukwaa hili linakuwa kama klabu cha pombe! analysis zingine zinazotolewa hapa ni tepe tepe sana,kwa mfano si lazima iwe ccm au chama kingine chochote rais ajaye lazima akubalike zanzibar! vigezo vya hivi haviwezi kutupa rais bora! anayechaguliwa na rais wa jamhuri ya tanzania!
Pengine kubwa la kutizama na linalotuunganisha watanzania wote ni kama candidate anaiweza kazi! kwa maana ya uzoefu,uaminifu,hekima,ujuzi,uthabiti nk, bahati mbaya sana watanzania wengi wanaochangia hapajf wanaiona kazi hii kama rahisi tu!!! ndio maana wanasikika wengine wakisema aje kijana next time!
Lakini ukweli kabisa kwa sasa hakuna kijana iwe kwa wale walio ktk uongozi sasa au walio nje anaweza kuwa rais mzr wa tz! pengine wengi wanavutwa kwa kutaka kuiga tu, kutaka nchi zingine zenye marais vijana.kwa tz ni vigumu!kwa sababu structuire ya malezi katika familia zetu ni mbovu kabisa siku hizi!!! hazimjengi mtoto au kijana kuwa kiongozi mzuri!! zinamjenga kuwa mbinafsi,mpenda anasa,mchoyo,mbaguzi,mnafiki nk. kwa maana hiyo bado tunahitaji sana kuwa na vongozi wa umri kama wa salim,shein,mwandosya,sitta, nk kwenye nafasi ya urais na makamu ili kutunza tunu za taifa letu,AMANI,UTULIVU,KUHESHIMIANA,UPENDO nk.
Mifano ipo mingi lakin ni vzr tunapojadili watz wanaoweza kufanya hii kazi tuongozwe na sifa ya UWEZO na siyo kutanguliza uwepo wa mizengwe au cjui mtandao hiyo ni fanatism tu haina nguvu sasa hivi,lkn mwisho kabisa yupo mwenyezi Mungu nayye ana hesabu zake! our choise is not ABSOLUTE!! it can be changed!!