Wito kwa Salim Ahmed Salim - Mpinge Kikwete 2010

Kosa kubwa mnalofanya kwenye ushauri wenu ni kumshauri agombee kupitia CCM wakati mnajua kwamba hataenda popote. Can you guys come out of box and think of a life without CCM? Yaani nyie watu hili limbwata la CCM hali-expire tu?

Sasa wewe mkuu na mwalimu wangu unaleta maada nyingine hapa kweli akiamuwa kugombea CHADEMA atapita kweli?? kama Zitto tu hata ktk mchakato wa uchaguzi ilishindikana duu kweli haya makuu!!

Hivi ni lipi nusu shari kati ccm walilomfanyia Mzee salim kwa kumchafua ktk kampeni lakini kagombea na lile la Zitto kutoruhusiwa kutogombea kabisa ktk CHADEMA na bado kuchafuliwa kukawa pale pale.?

Mimi naona wote na wewe ukiwemo tuanglie nje ya box pia.
 
wabongo maneno mengi na woga mwingi,eti upinzani haujakua nani kasema, sasa hela wanayotumia viongozi wetu ni mchezo,,magari mazuri, suti,,,,,wakati hata workshop zinazowahusu moja kwa moja wananchi hasa wakulima kama ile ya kilimo kwanza anaenda mkuu wa wilaya,,,,bora hata afisa kilimo wa wilaya.............watz ubwege utatuua.......na akili zetu hazina akili...............tunabaki kulaumu tu,,,wakt viongozi wanajineemesha kwa jasho letu,,,,,,hasa kodi zetu........mtu yuko bush vimiji vidogo eti aliipie kodi ya nyumba aliyojenga mwenyewe,akinunua mafuta ya koloboi alipie VAT.........jamani viongozi waonee huruma wananchi,,,,matumbo yenu hayajai.?
 
Mkuu,

Unawaongelea kina nani hawa?


SMZ wameapa kuwa mtu yeyote kutokea pemba asiwe Rais ,huku wakimwaga sumu dhidi watu wenye asili kutokea huko,imefika hata viongozi wa ngazi za juu watu wengi kutoka bara sasa nao wapandia Baniwagoni hilo la chuki , ukweli unauma lakini huo ndio ukweli , kwa kuwa SMZ ndio waliokama mpini katika Mungano na serekali ya kikwete *(Bara)imekamata makali, imeifanya SMZ kuwa na nguvu kubwa kuhusiana na mambo ya Mungano wanaridhiwa kwa kila wanalolitaka liwe kwa hofu ya kuwa wasije wakanika ukweli wa Mungano na kuvurugika ,wakati bara wamesha tamka Mungano ulindwe kwa hali yoyote ,sasa kumtaka Salim kugombea Urais wa TZ ni mtihani kwa serekali ya Kikwete na hatama ya Mungano unaolidwa kwa hali yeyote ile .
 

Nafikiri Babylon umeelewa - Muungano - ndio unaoipa SMZ kiburi cha kukataa mambo mengi yalo na manufaa kwa Taifa la Kitanzania - ikiwa kuna kitu wanachokipinga hutishia kuvunja Muungano na hapo SMT hugwaya - kuna siri gani ya kuwangangania?
 
Kwani Salim amewahi kuchukua maamuzi gani magumu katika uongozi wake ambayo tunaweza kuyaweka kwenye kipimo cha mizani ya uongozi na kusema alionesha mfano?
 
Mi ninaona tujaribu viongozi wapya.

Mtoto Tanzania ana miaka 40 na lakini bado UMEME ni Tatizo.
 
Mi ninaona tujaribu viongozi wapya.

Mbona tunao wengi tunaowajaribu..

Nchimbi, Masha, Ngeleja, Kamala, Malima etc

Na wengine wapo njiani waja kama kina Jerry Slaa, Kinjeketile Ngombale, Hussein Bashe, Nape Nnauye. Maina Owino, ect...

Na kama Urais nao umekuwa wa KUJARIBU nadhani tunaoyaona sasa bado hayatoshi.....tujiandae na makubwa zaidi

omarilyas
 
Hivi wakuu kuna yoyote humu ambae alifuatilia uchaguzi wa Japan?

Uchaguzi wa Japan ulihusu kubadili mfumo uliokuwepo kwa miaka 50 kwa kuchagua chama kingine ambacho kiliundwa na watu wa aina ya Salim A. Salim.

Salim A. Salim ana sifa zote za kuibadili Tanzania na kuindeleza kiukweli, na ndio maana anajaribu kutoka hilo dukuduku lake.

Ana "vision" (niliiona pale MOD wakti akiwa waziri), "exposure"- ameona mifumo mbalimbali duniani inavyoendesha nchi na mengine mengi tu.

Kwa kifupi ni mtu wa kimataifa.
 

Mkuu,

Kwa haya ulosema, nakupa 9/10
 
ni afadhali agombee amuondoe JK kwa sababu amekosa muelekeo na ameshindwa kutawala hisia za wa TZ.Wajameni tumpige JK chini kwa pamoja kwa wale wanaoitakia nchi yetu mema.Jk kasababisha chi iwe na makundi na umoja wa kitaifa kuanguka
 
Mungu akiendelea kumpa Afya njema, JK bado ataendela kuwa Rais wetu hadi 2015.

Mungu Ibariki Tanzania

Kidumu Chama Cha Mapinduzi.
 
Mi ninaona tujaribu viongozi wapya.

Mtoto Tanzania ana miaka 40 na lakini bado UMEME ni Tatizo.

mtizame vizuri...ana ndevu mpaka miguuni..si mtoto tena huyu ni mtu mzima na mvi moja moja zimeshaanza kuonekana...amedumaa huyu, ana matatizo makubwa sana ambayo ufumbuzi wake haujulikani utatoka wapi, labda muujiza.. toka azaliwe hatambai, hasimami, hatembei, haongei anasua sua tu..a 40 yrs old baby!
 

JK je, hakuchefui?? kwanini midanganyika hatupendi kuambiana ukweli?? tunapenda sana kuzunguka mibuyu na kusifia watu kwa unafiki wetu kwa kuwa tu tunafuata itikadi fulani! Ni lazima tukubali kutokubaliana, watu hatufanani, na akuambiaye ukweli anakutakia mema!!

Tumeshupalia mitandao tu kwa kuwa inatushibisha matumbo yetu na kutukinga dhidi ya sheria za nchi. Kila mtu ana uhuru wa ku-contest for the presidency of this country .... hakuna mwenye mkataba na kuweka marais wa nchi hii .... na kama wapo, believe me ... there is a day watakuja umbuka na kubakia uchi .... if not for the ballot power, then mass power will do!

Namkubali yeyote atakaye contest for presidency ...awe anatoka CCM au Upinzani .. i wont mind ... so long as hana dots za mtandao coz hawa jamaa wametubaka sana na inatosha!

wana CCM na wasio wana CCM... tuacheni mawazo mgando!!!!!!!!!!
 
hawa ndio walioambiwa na kikwete tuwaache wapumzike......salim kashika cheo kikubwa kabisa barani africa sote tunajua....anataka nini zaidi,mi nadhani tumwache tu apumzike.....
 
Ni kweli Salim ni kiongozi mzuri. Lakini kwa siasa za Tanzania hilo halipo. Si unajua ccm ni vipindi viwili kuwa raisi? Mpaka amalize miaka 10 huyu ndio ccm italazimika kutafuta mwingine, hapo ndipo kina Salim wataweza kusikika. Hata kama wewe unaona anfluku, mtandao wake unaona anang'ara. Piga ua ilhali kamaliza mitano ni lazima mitano mingine. Hiyo ndiyo ccm ya leo Bongo.
 

Kweli mkuu Leka,

Lakini umesikia yaliyompata mkulu Mwanza? ni uchovu au ni ugonjwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…