mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Nawasihi sana viongozi wetu kumtanguliza Mungu mbele katika vita dhidi ya corona. Msimwonee Mungu haya katika jambo hili. Usalama tulionao tofauti na mataifa mengine siri yake ni kwamba Rais wetu wa wakati huo alikuwa anaitisha maombi na kuhamasisha watu kumwomba na kumtanguliza Mungu mbele.
Kwanini tunaonea aibu ukweli huu? Haigharimu chochote kwa viongozi wetu kuomba watu wamwombe Mungu. Kuomba maombi haina maana kuwa tahadhari nyingine zisichukuliwe. Tusitake kuwafurahisha mabeberu kwa gharama ya kumweka Mungu pembeni kama Taifa.
Kwaakili ya kawaida hakuna mtu anayeweza kuchukua tahadhari ya kutosha kumzidi waziri mkuu wa Uingereza au Trump? Hao pamoja na tahadhari kubwa walipata corona. Hapo ndio ujue kuwa si kwa uweza wala kwa nguvu bali kwa neema ya Mungu leo hii Tanzania tuko salama! Viongozi wetu mna dhamana kubwa sana mbele za Mungu kwa jinsi mnavyotuongoza katika vita hii.
Sikilizeni dhamiri zenu wala si kuogopeshwa na vitisho vya mabeberu. Tunawaamini mtatuongoza vizuri kama tulivyoanza kwa kumtanguliza Mungu. Msipotusimamia vizuri Mungu ataidai damu ya watanzania katika mikono yenu.
Jipeni moyo, simameni imara na Mungu atawasaidia. Kumwomba na kumtanguliza Mungu mbele ndiyo jambo la msingi na mengine ya tahadhari ndipo yafuate. Vinginevyo tukitanguliza akili zetu na tahadhari zingine hazitakuwa na msaada. Hizo zingine zinakuwa na maana tu kama Mungu ametangulizwa mbele.