Pre GE2025 Wito kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama: Msiogope, simameni na Wananchi, CCM wanatupeleka pabaya!

Pre GE2025 Wito kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama: Msiogope, simameni na Wananchi, CCM wanatupeleka pabaya!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Shida gani? Lini walikuwa wanapata Raha? 😁😁😁😁😁

Kwamba Wakuu wanapata shida au siyo? 😂😂
Kwa hiyo kumbe na weww unajua wanapata shida ikowemo Bima za chini zisizotibu magonjwa makubwa na pensheni za mbuzi wakati CCM wanapitisha Sheria ya kutunzana Viongozi wa kisiasa na wenza wao
 
Nyie ndo walinzi wa taifa hili. Sio CCM

Nafahamu mnaona kwa namna gani CCM wanalipeleka Taifa hili pabaya.

Nafahamu mnajua namna ya Viongozi wa CCM wanavyolifisadi hili Taifa kwa wizi wa kutisha na matumizi mabaya ya kodi za wananchi huku wakitaka watukuzwe at the expense ya kodi za wananchi.

Najua mnaona wanavyoiba fedha za wananchi kupitia tenda za miradi mbalimbali huku miradi yenyewe ikijengwa chini ya kiwango.

Najua mnaona wanavyoongeza gharama za miradi inayotumia fedha za wananchi ili waibe hela kwa faida zao na kugharamia wizi wa uchaguzi. Mfano overpricing ya viwanja vya michezo vinavyoendelea kujengwa huko Dodoma, Arusha na hapa Dar es Salaam.

Nafahamu mnajua namna taifa hili lilivyofikia kwenye hatari ya kuwa failed state kutokana na kikundi cha watu wachache hasa CCM kujimilisha Taifa hili. Wanateuana watu wasio na uwezo kwa sababu tu ya kujuana na uchawa.

Najua mnafahamu chaguzi za Taifa hili sio chaguzi kama chaguzi ila ni maigizo yanayofanyika ili kuwahadaa wananchi. Viongozi wanaopatikana kupitia chaguzi hizo sio Viongozi waliochaguliwa kweli na wananchi na uthibitisho ni Maneno ya makada na Viongozi wa CCM wenyewe. Rejeeni Hotuba ya Nape kuhusu wanavyoshinda uchaguzi alipokuwa Kagera na ile hotuba ya aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido walivyoelezea kuikweli namna CCM wanavyonajisi chaguzi za nchi hii kupitia Tume hii ya Uchaguzi ambayo ni vibaraka wa CCM.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Nafahamu mnaona namna uchawa unavyoliangamiza taifa na kodi za wananchi zinavyotumika kutengeneza watu wajinga wanaoitwa machawa kuwarubuni Watanzania.


Najua mnafahamu kuwa haya yote yanafanywa na CCM kwa sababu moja tu. Nchi hii ina Katiba mbovu inayowawezesha kufanikisha markings yote haya bila kufanywa chochote na wala kuhojiwa na yeyote.

Najua mnajua kuwa leo hii mkiamua kusimama na Wananchi, Taifa letu litafanikiwa kupata Katiba Bora ambayo itaweka mifumo imara na kuondoa uwekezano wa nchi yetu kufikia hapa tulipofikia kuelekea kuwa failed state.

Najua mnafahamu kuwa kiukweli CCM si chochote si lolote bila nyie. Na kiburi chao ni kwa sababu tu mmefumbia macho ujinga wao.

Ombi langu kwenu,
Sasa simameni na Wananchi. Msiruhusu CCM waibe uchaguzi, mairuhusu CCM waendeleze udhalimu wao maana udhalimu wao unaenda kuliangamiza hili taifa.

Nyie ndo walinzi wa hili Taifa na CCM wakikaa kando haitawaathili wala kuwapunguzia chochote ila italihakikishia hili Taifa uimara na mafanikio ya uhakika kwa wananchi wake kwa miaka mingi ijayo.

Nawaomba tena. Simameni na Wananchi na kataeni kutumiwa na CCM.
Kazini kuna kazi
 

Attachments

  • 3049818-bea797ab6cbc71c96b0e8f1726a165b5.mp4
    55.4 MB
Hapana!

CCM wameshalifikisha hili taifa pabaya sana. Tuviombe vyombo hivi viliokoe hili Taifa kwa kusimama upande wa wananchi.
Juzi nilipokuwa natizama jinsi Assad alivyokimbia nchi..ndipo nikaamini kuwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakizima data Huwa wanaamka wakiwa wamechelewa sana!
Uzalendo wa kweli uko JWTZ...kama huamini rejea Salamu za CDF mbele ya Mh.Rais siku Ile..!
 
Juzi nilipokuwa natizama jinsi Assad alivyokimbia nchi..ndipo nikaamini kuwa wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wakizima data Huwa wanaamka wakiwa wamechelewa sana!
Uzalendo wa kweli uko JWTZ...kama huamini rejea Salamu za CDF mbele ya Mh.Rais siku Ile..!
Wanasiasa na vyama vyao bila vyombo vya usalama si lolote si chochote.
 
Acha kuwadharau vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

CCM ni wajinga wanaoishi kwa propaganda, uongo na vitisho visivyo maana.

Wana kipi cha kuvifanya vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vikisema hapana juu ya udhalimu wao kwa mfano?
Sijavidharu mkuu naviheshimu sana, ila sijui ni kwanini vinaigwaya sana Ccm.

We angalia DPW walivyojitwalia kilaini bandari zetu, angalia wamasai walivyofurushwa kwenye makazi yao ya asili na pia angalia watawala wanavyofuja rasilimali za taifa.

Yote hayo yanafanyika huku idara zote za ulinzi zimeweka mikia tumboni kama mbwa aliyeona chatu.
 
Back
Top Bottom