GE2025 Wito kwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama: Simameni na Wananchi tarehe 29 Oktoba, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Sote tunafahamu kuwa Taifa letu hivi sasa linaangamizwa kwa kutisha na rushwa kubwa zinazofanywa na Wanasiasa na familia zao bila kusahau Viongozi wachache wa Serikali na vyombo ya Ulinzi na Usalama.

Haya yanafanyika huku Watanzania wengi wakikosa huduma bora za msingi kama Maji safi na salama, madawa hospitalini, makazi bora na salama, muindombinu bora ya barabara pamoja na elimu safi na salama kwenye mazingira bora na salama.

Haya yote yanafanyika huku Watanzania wengi wakiwa wanalipwa viinua mgongo vidogo sana baada ya kustaafu vinavyowafanya waishi maisha magumu sana baada ya kustaafu.

Haya yanafanyika huku Watanzania wengi wakikosa hata bima za afya kwao na familia zao hali inayowafanya wengi kukosa matibabu ya msingi.

Haya yanafanyika huku mamia ya vijana wakiwa hawana kazi na kuishia kutumiwa na Wanasiasa kama chawa kwa kupewa ujira wa dharau wa 5000 hadi 10000 na tisheti za chama ambazo note hizo zimetokana na pesa zilizoibwa na wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi. Pesa zilizopaswa kutumika kutoa huduma bora kwa wananchi wa kawaida.

Haya yanafanyika huku Watanzania wanaosimama kupinga maovu haya wakitekwa, kupotezwa na kuuwawa kana kwamba ni wanyama tu wa porini wasio na haki yeyote.

Kwa hali ilivyo navisihi sana vyombo ya ulinzi na usalama kusimama imara hiyo siku ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba 2025 kwa kuwa upande wa wananchi walioamua kupinga matendo haya mabaya yanayofanywa dhidi yao.

Mwaka 2024 katika maandamano ya Wanafunzi na Wananchi nchini Bangladesh, Mkuu wa Majeshi wa Nchi hiyo Generali Uz Zaman alikataa kupokea amri ya aliye kuwa kiongozi wa Nchi hiyo Sheikh Hasina ya kuuwa Waandamanaji waliokuwa wanapinga Ufisadi wa Serikali yake. Hatimaye Serikali ya Sheikh Hasina liondolewa na Wananchi na sasa Taifa la Bangladesh limeanza mwanzo mpya.

Wito wangu kwa Vyombo ya Ulinzi na Usalama, tarehe 29 Oktoba 2025x simameni na wananchi maana yanayopiganiwa na Wananchi yakifanikiwa yatawasaidia nyie, ndugu zenu na hadi vizazi vyenu. Ni mambo yatakayolifaidisha Taifa letu lote.
 
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama ambao wanajipimia keki ya taifa watapata wapi busara ya kusimama na kina Pangupakavutiamchuzi?
 
Askari wanaowaongoza ndo wanatumwa kwenda field kupambana na Wananchi.

Askari hawa wengi wao ndio wanaoathirika pakubwa na rushwa kubwa na ndogo zinazofanywa na Viongozi wa Juu wa Taifa hili hasa Wanasiasa na wengineo wote.

Wito huu ni kwa Askari wote kujitambua na kufanya maamuzi sahihi kwa ajili ya kesho yetu Watanzania wote.
 
Issue ni kwamba askari wataahidiwa au kupewa Hela ndegu sana na hivyo watakuwa vipifo lakini baada ya kuzitumia na kuisha watakumbuka na kujuta sana.

Imagine waalimu hupewa laki1 au 50k wanaiba matokeo hapo mwalimu anajiona mjanja sana masikini ya Mungu maisha atakayopitia baada ya siku tati ni Siri yake mke wake na Watoto tu
 
Coordination ya askari wa chini inafanywa na hao bloated commanders. Labda miongoni mwao apatikane Ibrahim Traoré!
 
Issue ni kwamba askari wataahidiwa au kupewa Hela ndegu sana na hivyo watakuwa vipifo lakini baada ya kuzitumia na kuisha watakumbuka na kujuta sana.

Imagine waalimu hupewa laki1 au 50k wanaiba matokeo hapo mwalimu anajiona mjanja sana masikini ya Mungu maisha atakayopitia baada ya siku tati ni Siri yake mke wake na Watoto tu
Hello ndefu itakusaidia nini wakati Wanasiasa wanafisadi kodi za Wananchi kukufanya uishi maisha ya kimasikini baada ya kustaafu?
 
Hayo Huwa wanayajutia baada ya uchaguzi nakwambia ukweli hakuna mwalimu anayehongwa zaidia 200k Kuna kura! Ni 50-100k tu hapo anajiona ana akili sana na kuwatambia wenzake kumbe kichwani ni mavi ya nyoka tu
 
Hao unaowaita wakuu wa vyombo vya usalama wakobize kumfurahisha boss wao ili wakistaafu wahongwe ubalozi au ukuu wa mkoa
 
Sote tunafahamu kuwa Taifa letu hivi sasa linaangamizwa kwa kutisha na rushwa kubwa zinazofanywa na Wanasiasa na familia zao bila kusahau Viongozi wachache wa Serikali na vyombo ya Ulinzi na Usalama.

Haya yanafanyika huku Watanzania wengi wakikosa huduma bora za msingi kama Maji safi na salama, madawa hospitalini, makazi bora na salama, muindombinu bora ya barabara pamoja na elimu safi na salama kwenye mazingira bora na salama.

Haya yote yanafanyika huku Watanzania wengi wakiwa wanalipwa viinua mgongo vidogo sana baada ya kustaafu vinavyowafanya waishi maisha magumu sana baada ya kustaafu.

Haya yanafanyika huku Watanzania wengi wakikosa hata bima za afya kwao na familia zao hali inayowafanya wengi kukosa matibabu ya msingi.

Haya yanafanyika huku mamia ya vijana wakiwa hawana kazi na kuishia kutumiwa na Wanasiasa kama chawa kwa kupewa ujira wa dharau wa 5000 hadi 10000 na tisheti za chama ambazo note hizo zimetokana na pesa zilizoibwa na wanasiasa wa Chama cha Mapinduzi. Pesa zilizopaswa kutumika kutoa huduma bora kwa wananchi wa kawaida.

Haya yanafanyika huku Watanzania wanaosimama kupinga maovu haya wakitekwa, kupotezwa na kuuwawa kana kwamba ni wanyama tu wa porini wasio na haki yeyote.

Kwa hali ilivyo navisihi sana vyombo ya ulinzi na usalama kusimama imara hiyo siku ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba 2025 kwa kuwa upande wa wananchi walioamua kupinga matendo haya mabaya yanayofanywa dhidi yao.

Mwaka 2024 katika maandamano ya Wanafunzi na Wananchi nchini Bangladesh, Mkuu wa Majeshi wa Nchi hiyo Generali Uz Zaman alikataa kupokea amri ya aliye kuwa kiongozi wa Nchi hiyo Sheikh Hasina ya kuuwa Waandamanaji waliokuwa wanapinga Ufisadi wa Serikali yake. Hatimaye Serikali ya Sheikh Hasina liondolewa na Wananchi na sasa Taifa la Bangladesh limeanza mwanzo mpya.

Wito wangu kwa Vyombo ya Ulinzi na Usalama, tarehe 29 Oktoba 2025x simameni na wananchi maana yanayopiganiwa na Wananchi yakifanikiwa yatawasaidia nyie, ndugu zenu na hadi vizazi vyenu. Ni mambo yatakayolifaidisha Taifa letu lote.
Wasipo tekeleza agizo lako mkuu Mungu atatekeleza kusimama nao,
Leo mtu mtu mmoja akaniambi 29/ October ,cha kwanza atasimama juu ya jengo kuu kuliko yote kwa urefu akiwa kifua wazi na kupunga moja ya vazi lake kabla ya mengine anayo fikiri ,hapa ndo nikajua safari hii watz hawatanii ,wameamua aisee
 
WWasiposimama na Wananchi hata Mungu atawashangaa maana kinachopiganiwa na Wananchi ni cha kuwanufaisha Watanzania wote kuanzia wao, ndugu zao hadi familia zao.

Hali iliyopo sasa wanaolitesa hili Taifa ni Wanasiasa hasa Chama cha Mapinduzi.

Wakisimama upande wa Wananchi wanasiasa watatia adabu na Wananchi na matakwa yao yataheshimiwa kweli.
 
Asante sana Kapteni Tesha. Mungu akulinde

Jeshi la Wananchi lisimame na Wananchi hiyo Oktoba 29 kusitisha huu udhalimu wa CCM
 
JWTZ simameni na Kapteni Tesha.

Likomboeni Taifa dhidi ya huu udhalimu na dhidi ya hawa madhalimu
IMG-20251004-WA0008.jpg
 
Back
Top Bottom