Wito kwa WanaJF: JF Member anapokufa, je, tuanze kuonesha solidarity yetu kama msiba wa Regia, au tuache tu kila mtu na bahati yake na hadhi yake?


Taabu tozo za miamala ambazo wengine time kula yamini kuwa Mwigulu ataisoma
 
Hili ni wazo zuri lakini pia inaweza kuwa ni fursa kwa wenye nia ovu.....anonymity ndio inayofanya JF iwe yenye kuogofya.......

Nadhani kukiwekwa utaratibu mzuri juu ya hili jambo kila mmoja atanufaika na hili na kujiona wa thamani kuwa mwana JF na kuwavutia wengine kuwa member wa JF......
 
Nakubaliana na hili wazo,uongozi wa jf ufanye kitu ambacho kitaonesha utekelezaji wake
Hiv mnaposemaga uongoz wa jamii forums huwa mna refer kitu gan!? Au wakurugenz na technical stsffs hapo? ( as i assume), Isn't programming (and other admnstrative stuffs) a burden enough hapo JF mpaka mjitie kwenye mambo mengine ambayo ni ya users ambao kwa ma group yao kwa kadiri ya wanavyojuana ndio haswa wanatakiwa kushughulikiana!??
 
Mimi naunga mkono wazo, na R.I.P mrumi mungu Amjalie pepo ya JANATULFIRDOUS. AMEEN
 
Mkuu uongozi ndo utupe uelekeo na namna ya ufanyikaji wa hili Jambo,humu wengi tunatumia false names,je ikitokea Mimi naanzisha uhamasishaji wa mchango wa msiba wa member wa jf mtaniamini?

Hapa ndo tunataka uongozi utoe mwongozo mkuu
 
Wazo ni zuri lakini lisiwe ndio sera ya JF
Kwenye initial stage ni rahisi sana kuwa na mfuko husika, lakini kadiri unavyokua mambo yatabadilika na kuhitaji management kamili
Je kutakuwa na viingilio?
Je michango itakuwa kwa wiki au kwa mwezi?
Tutachanga kiasi gani?
Taratibu zitakuwaje?
Ambaye hajawahi kuchanga akifa tutafanyaje?
Mtu akichelewa kuchanga/akipitisha mchango afanyweje?

LET LOVE LEAD!
Kuna ambao watategea kuchanga kwa kudhani wao sio sehemu muhimu ya JF
Kuna ambao hawatachanga kwa Kudhani tu michango itatumika ndivyo sivyo
Marehemu anaweza kukosa support ya wengine kwa kudhani tu kuna mfuko wa michango
Management ya pesa huwa inasumbua sana..badala ya kutuunganisha kwa upendo inaweza kutuletea mgawanyiko mkubwa na tukafarakana sana!

USHAURI WANGU
Kifo ni jambo la dharura.. Kwasasa ni vema tukabaki na utaratibu huu huu wa kupeana taarifa na kutoa michango ya hiari kutokana na kuguswa, kupitia mawasiano yasiyoacha Shaka ya ndugu ama rafiki Ana jamaa wa karibu na kuchukulia kila msiba Kama kesi inayojitegemea!
 
Si jambo la kupendeza kwa hakika,
Mgt ya JF hebu tuweni na jambo pindi mambo haya yanapotokea. Na kwa mchango wa Min. 1,000 wakuu mfikirie pia mwanajukwaa yyt anapopoteza matathalani Wazazi, watoto au mwenza. JF hatujashindwa kufanya haya isipokuwa coordination ndo changamoto. RIP warumi

TUAMKE, TUTENDE.
 
Naona haya kwenye magrupu ya WhatsApp ya watu wanaofahamiana kabisa inavyokuwa ngumu kutekelezeka. Sembuse hapa ambapo hatujuani kabisa?

Mi nadhani liwe jambo la hiari kwa watakoguswa. Namba inatolewa watu wanachanga...

Tatizo naloliona hapa, nikituma hela kwa mchangishaji, mara paap anaona jina la mtumaji ni mimi niliyekuwa natukanana naye jamvini, kumbe ni bosi wake kazini.... Lahaula lakwata! Kumbe bosi yuko JF anamwaga pumba kichizi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…