Uchaguzi 2020 Wito kwa Watanzania wenzangu tukiwemo sisi WanaJF, Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi chagua chama cha ukweli kwa maendeleo ya kweli

Wenye kuelewa tumekuelewa.
 
Nimekwambia wazanzibari mambo yameanza kwenda kombo kuanzia miaka ya 90 wakati wa mkapa sio kielimu tu hata kiuchumi
Kama ulikuwepo mjini maduka mengi kariakoo yalikua ya wazanzibari lakini mkapa kawamaliza
Kuna mambo mengi nchi hii behind the scenes
 
Kuna mambo mengine usitumie akili Sana
Kulikoni awamu hii shule za kiislamu zina''CHONWA'' moto kila kukicha halafu hakuna utafiti wala uchunguzi??
Hakuna mjengo Tanzania nzima yanapata majanga ya moto kuliko shule za kiislamu kulikoniii???
 

Kwenye kupiga kura, ukichagua chama ambacho sicho, ambacho sio chama cha ushindi, unakuwa umepoteza kura yako!.
Tukapige kura lakini tusipoteze kura zetu!.

Paskali
Hakuna kura inayopotea, kila kura inatuma ujumbe.
Ngoja nikufafanulie. Mtu aliyeshinda kwa asilimia 90 na yule aliyeshinda kwa asilimia 51 wote wameshinda; lakini huyo wa asilimia 51 lazima ajiulize sana kwa nini asilimia 49 hawakumpigia? Kama ni mtu makini atafanya utafiti na kuondoa changamoto ili uchaguzi unaofuata asilimia za ushindi ziongezeke - yaani wanaomkubali waongezeke.
Kura ambazo hazikumpigia mshindi hazikupotea bali zimemtumia ujumbe mhusika kuwa mahali fulani kuna jambo haliko sawa
 
Dkt Paschal wewe ni mwanahabari. Je wana habari mnataka uhuru wa habari? Asante
 
Paskali, Chama cha ushindi ni kipi?
 

Paskali uwe unaeleweka vizuri, je una maanisha​

....Tujitokeze Kwa Wingi Chagua Chama cha Ukweli Kwa Maendeleo ya Kweli? au unawasemea wale kule?​

 
Kweli kaka tusifanye Tena makosa tulioyafanya miaka mitano iliopita na kujukuta tukitawaliwa ki dikteta na kunyinwa uhuru hata wa kutoa mawazo
Kweli kaka tusifanye makosa tulioyafanya miaka mitano iliopita mpaka tunazoea mauaji yanayofaanywa na wasiojulikana
Kweli kaka tusifanye makosa tuliofanya miaka mitano hadi inafikia watu wanafilisiwa hivi
Kweli kaka tusifanye makosa ya kumchagua mtu katili anaekula hela za rambirambi za wahanga wa tetemeko la ardhi halafu badala hata pole anakuja kutuaibisha na kutudhalilisha kwa maneno ya dhihaka
Kweli kaka tusifanye makosa kuchagua mtu anaechukua korosho zetu kupitia jeshi lenye silaha za kivita
Kweli kaka tusifanye makosa kumchagua
Mtu atakaekua mbinafsi wa kujenga kiwanja cha ndege cha kimataifa kijijini wakati wananchi hapo kijijini hawana maji
Kweli kaka tusifanye makosa kumchagua mtu afungae na kutesa viongozi wa kidini eti ni magaidi
Kweli kaka tusikubali kuchagua mtu atakae mpa funguo za hazina mtoto wa dadake
Kweli kaka tusikubali kumchagua mtu atakae toa kandarasi zote kwa mume mwenza bila kutangaza zabuni
Kweli kaka tusifanye makosa kuchagua mtu anaeteua zaidi ya theluthi moja ya watendaji wa serikali kutoka kabila lake
Kweli kaka tusifanye makosa,,,,,,,,,,
Mambo mengi yametukuta miaka mitano hii
Tusifanye kosa
Piga kura ya ukombozi Linda kura
Takbirr
Allah Akbar
 
Tusidanganyike !Maendeleo ni Mchakato, yapo mengi aliyofanya Rais wetu na Tunajivunia kua na Rais Mazalendo na Mchapakazi kama Dr.Magufuli ..Tunaendelea Nae...!KURA KWA MAGUFULI
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
#ChaguaMagufuli
 
Ili aendelee kuwatesa mashekh wetu???
Wanafiki pekee watamchagua katili asie na huruma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…