Wito kwa watanzania wote: Ili CCM na serikali zake wajue hatuwataki, 2025 wote tususie uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi

Wito kwa watanzania wote: Ili CCM na serikali zake wajue hatuwataki, 2025 wote tususie uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi

Ni miaka 63 sasa CCM ipo madarakani. Kimsingi hakuna maendeleo ya msingi waliyotuletea, isipokuwa kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilileta usanii wa kisiasa na kiuchumi na hatimaye kuturudisha nyuma decades.Wanayojisifia kwamba ni maendeleo si lolote kabisa ukilinganisha na rasilimali nyingi tulizo nazo. Tuamke Watanzania.

Comrade Magufuli katika awamu yake moja alijitahitahidi kubadilisha taswira ya Tanzania kwa kutuletea maendeleo, lakini juhudi zake zilifishwa prematurely, inasikitisha sana.

Kwa jinsi hali ilivyo ya kisiasa nchini mwetu, hatuna jinsi yeyote ambayo kama Watanzania tunaweza kujinasua kwenye mkwamo tulio nao sasa.Katiba haiheshimiwi kabisa na sioni uwezekano wa Bunge au hata wana siasa kutusaidia.

Mwito wangu kama Mtanzania ni huu, kama mpaka 2025 tusipokuwa na Katiba mpya, wala Tume Huru ya Uchaguzi, siku ya uchaguzi wote tubaki nyumbani.Sisi wananchi ndio tunaowapa wanasiasa legitimacy ya kutawala, kama wasipotupa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tubaki nyumbani,simply tuwanyime legitimacy ya kututawala.It is now or never, tushirikiane wote.

kuhusu suala la kuiondoa ccm kwenye ballot papers hilo sahauni narudia tena sahauni,unless kuwe na katiba mpya tena ile itokanayo na warioba na tume huru ya uchaguzi vitu ambayo huwezi ona ccm inakubali kuvifanya.

Wananchi ndio wakuiondoa ccm madarakani kwanza wasusie uchaguzi hapa napo na wasiwasi ccm kuhonga mamluki wake wakapige kura kisha wanazi multiply hata mara 1000[emoji28], ili ionekane wananchi wengi wamepiga kura.

Ccm sio chama cha siasa ni genge la wahuni na mafisadi.
 
Sawa,sisi tukae nyumbani,mbona maruhani hayaonekani?Tusipokwenda watajistukia mkuu,na uovu wao utakuwa dhahiri.
Kuna watanzania wajinga ndugu, ccm wakiwapa tu kanga wanabebwa kwenye magari wanaenda lupiga kura, kwa unadhani huwa wanafanyaje kwenye mikutano yao? Wanagawa ef tano tan9 na wanasomba kwa malori
 
Mimi binafsi sipigi kura tena chini ya tume ya CCM
 
Me huwa siwaelewagi mnaolilia tume huru ya uchaguz et sijui katiba mpya, hivi unahisi hayo yatabadilisha nini ikiwa watu ni wale wale?

Hiyo tume huru ya uchaguzi watashindwa nini kuihonga hela ili watoe matokeo wanayoyataka?

Jirani zetu Kenya hapo uchaguzi wao uliopita ulisimamiwa na tume huru, je wamepata walichotegemea?

Sijui katiba mpya, je yaliyopo kwenye katiba ya sasa yanasimamiwa?

Ishu ni viongozi hawana uchungu na watanzania na ni wabinafsi na issue sio katiba mpya wala tume huru

Sent using Jamii Forums mobile app
haya tufanyejee weka mbinu...
 
Mtaishia kugongwa virungu na police muishie kuwa walemavu halafu mje na kauli ya Mungu atatulipia.

Ukishajitambua kwenye maisha pigania maendeleo ya familia yako hayo mengine unayoona hayawezekani yaache yakupite tu

Sent using Jamii Forums mobile app

Wazee wetu wangekuwa waoga kama wewe yamkini tusipata Uhuru tungeendelea kutawaliwa na mkoloni .?!
 
Ni miaka 63 sasa CCM ipo madarakani. Kimsingi hakuna maendeleo ya msingi waliyotuletea, isipokuwa kuturudisha nyuma kimaendeleo.

Kila serikali iliyoingia madarakani ilileta usanii wa kisiasa na kiuchumi na hatimaye kuturudisha nyuma decades.Wanayojisifia kwamba ni maendeleo si lolote kabisa ukilinganisha na rasilimali nyingi tulizo nazo. Tuamke Watanzania.

Comrade Magufuli katika awamu yake moja alijitahitahidi kubadilisha taswira ya Tanzania kwa kutuletea maendeleo, lakini juhudi zake zilifishwa prematurely, inasikitisha sana.

Kwa jinsi hali ilivyo ya kisiasa nchini mwetu, hatuna jinsi yeyote ambayo kama Watanzania tunaweza kujinasua kwenye mkwamo tulio nao sasa.Katiba haiheshimiwi kabisa na sioni uwezekano wa Bunge au hata wana siasa kutusaidia.

Mwito wangu kama Mtanzania ni huu, kama mpaka 2025 tusipokuwa na Katiba mpya, wala Tume Huru ya Uchaguzi, siku ya uchaguzi wote tubaki nyumbani.Sisi wananchi ndio tunaowapa wanasiasa legitimacy ya kutawala, kama wasipotupa Katiba mpya na Tume Huru ya Uchaguzi tubaki nyumbani,simply tuwanyime legitimacy ya kututawala.It is now or never, tushirikiane wote.
Wazee wa buku saba na wale wazee wa vitenge, kofia na t-shirts hawawez gomea maan tyr wamepewa mzigo wa hayo niliyoainisha hapo juu!!
 
CCM peke yake ndio itatuvusha watanzania dhidi ya madui watatu namini wazalendo wanajua
 
CCM wanajijua wameshachokwa.Kuwasusia uchaguzi ni kuwawashia "Green Light" waendelee kutawala,ni sawa na kumkabidhi fisi bucha,manake wanajijua kwenye ballot box/sanduku la kura hawatoboi.Mimi nafikiri labda ungeshauri tuingie kwenye uchaguzi kwa kulinda kura zetu.Ni ngumu kushinda uchaguzi wa raisi kwa jinsi mambo yalivyolakini angalau ubungo watakuwepo wawakilishi wa wananchi toka upinzani ambao watawasha moto na wabunge wa CCM waonekane hawana lolote mbele ya wananchi.Ni mwisho wa siku,miaka inavyokwendda,CCM watamwaga manyanga tu.Sababu ya kukosa support ya wananchi walio wengi 🤔
 
CCM peke yake ndio itatuvusha watanzania dhidi ya madui watatu namini wazalendo wanajua
Wewe ni li-CCM lazima useme huu upuuzi.Hata hivyo ifike mahali muone aibu kwa uovu mnatufanyia Watanzania.it seems mmejivua ubinadamu kabisa,tunawaona ni binadamu wenzetu kumbe sio.
 
Sasa hivi Umeme hakuna mateso wanapata wote walio sisiemu, wapinzani na wasio wanachama wa chama chochote cha siasa.
 
Regardless of the political membership status all suffer the consequences of lack of electricity supply.
 
Unaenda kupiga kura na anayehesabu kura ni mmoja wa wagombea.Hiyo siku tafuta jambo la muhimu la kufanya ila sio huo upuuzi wa kura
 
Back
Top Bottom