Kw akuwa kuna loophole kwamba Mteule wa Rais hawajibiki kwa mtu yeyote mpaka kwa Rais mwenyewe tu so wateule hawa wanavunja sheria sababu wana Kinga moja kwa moja kutoka kwa mteuaji.
Sasa basi ikiwa Mahakama mamlaka yake haitoki moja kwa moja kwa rais pekee akina Makonda et al wasingekuwa wanadharau wito wa mahakama na kufanya wanayotaka.
Huo ni mfano tu ktk mingi.
Njia tunazopata viongozi wengi ni kwa njia ya Uchaguzi sasa tazama uovu na uvunjaji sheria unaofanyika wakati wa Uchaguzi huku aliyewatuma wafanye hivyo ni Mgombea ambaye bado yuko madarakani na ndiye kawateua hao wavunja sheria ili aliyewateua wamlinde kwenye Ushindi wa mezani.
Hizi loopholes ndio ubovu wa katiba yenyewe.
Tumeona Ripoti ya CAG ilivyoivua nguo serikali. Lakini Dr Tulia Ackson kwa kuogopa kuaibisha Mama akaamua kuitupilia mbali yasije kumkuta Yale ya Ndugai....
Hakuna hata moja kati ya uliyoyaeleza hapa ninalokataa, umeandika ukweli mtupu hapo.
Lakini, pamoja na ukweli huu, mimi naamini, dawa sahihi kabisa ya kuwakomesha hawa watu wa CCM ni wananchi wenyewe, na siyo lazima iwe Katiba Mpya.
Tukipata watu wa kutosha, watakaokuwa tayari kukataa uhalifu, CCM hawawezi kufanya uhalifu wao waliozoea kuufanya.
Huhitaji raia milioni kumi, wote kuwa mstari wa mbele kukataa uhujumu huu. Tukipata watu kuanzia laki tano tu, walioelimishwa vizuri, na kuelewa wajibu wao wa kuzuia uhalifu, hapatatokea uhalifu kamwe.
Hawa wakishapatikana, hapo ndipo utakapotambua kuwa kumbe waTanzania wengi wamechoshwa na haya madudu wafanyayo CCM, kwa maana utaona nchi nzima inalipuka kukataa kuharibiwa kwa kura. zao.
Sasa kazi ipo tu hapo pa kuwapa elimu, na kuwaandaa hawa watu wa mwanzo wawe tayari kwa kila hali kutimiza wajibu wao.
Hii ndiyo kazi tunayo waomba CHADEMA waisimamie, kuweka mikakati na kuratibu juhudi zote za kufanikisha zoezi hili.
Nchi hii haiwezi kukosa watu laki tano waliotayari kulinda sheria ili uhalifu usifanywe dhidi ya wananchi.
Hata vyombo vya dola sivioni vkishiriki kuwaumiza wananchi hawa wanaolinda maslahi ya nchi.
Hata CCM wenyewe wataona aibu ya kufanya uhalifu wao. Sasa hivi hakuna anayenyanyua kidole, ndiyo maana wanafanya ionekane kama ni hali ya kawaida tu.