Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Kila jambo baya lilikuwa na mwanzo mdogo, lakini wahusika hawakuushughulikia mwanzo, na baadaye wakaangamia au wakalazimika kutumia gharama kubwa kuokoa Taifa au jamii yao.
Tanzania hii ya leo, pamoja na matatizo mengi tuliyo nayo, umoja wetu usiozingatia dini, kabila au eneo mtu atokalo ni jasho na jitihada nyingi za muasisi wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere (Mwenyezi Mungu Umjalie Pumziko Jema la Milele).
Baada ya jitihada hizi za watangulizi wako, Rais Samia usikubali kuingia kwenye historia mbaya kuwa wewe ulikuwa mtawala wa kwanza kuruhusu mambo yanayopalilia chuki na ugaidi wa kidini.
Kuna mtu ameingia nchini, mtu huyu ni mhalifu, nchini kwake India amepigwa marufuku kuonekana na anatafutwa kwa kuhamasisha ugaidi. Mataifa mengi Duniani, yamempiga marufuku kuonekana katika mataifa yao kutokana na mafundisho yake hatari kwa usalama wa Dunia.
Mtu huyu anayedaiwa kuendesha midahalo ya kidini ni mtu ambaye amesikika mara kadhaa katika mihadhara yake akitamka kuwa waislam wote wanatakiwa kuwa magaidi dhidi ya wale aliowaita ni maadui wa uislam.
Hivi kweli waislam wa Tanzania wamekosa watu wa kuwafundisha watu kuhusiana na imani yao mpaka aletwe mtu ambaye anatafutwa kwa uhalifu na mafunfisho ya uovu?
Rais ingilia kati, usiruhusu watu wahalifu kuja kupandiza mbegu za chuki na ugaidi nchini mwetu. Kinachopandwa leo na watu waovu kama huyo mhubiri, matunda yake yatakuwa kuvisumbua vizazi vyetu vya baadaye.
Dini haifanyiwi mdahalo wala mashindano, dini hufundishwa na kuhubiriwa.
Samia, wewe ni muislam, na huyu mhubiri mhalifu anayetafutwa, ni muislam, ukiruhusu haya mambo ya kidini yanayokiuka misingi ya utengamano wa Taifa letu, inaweza kuleta tafsiri mbaya kwa watu wengine. Usikubali hilo litokee, litakuathiri sana wewe binafsi na Taifa letu.
Mshikamano wetu, umpja wetu, vinatakiwa kulindwa kwa nguvu zote.