Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,264
Nyakati kama hizi haziepukiki. Taifa linazeeka na linahitaji Reforms. Kama waasisi wa Reforms walidhani itabakia kwenye tafsiri zao, basi walikosea sana. Reforms ni OVERHAUL. Hakuna cha Ceteris paribus. Mabadiliko yasipowagusa ni kazi bure. Sio suala la mvinyo mpya, chupa ya zamani.
Hata baadhi ya wanyama na wadudu wakifikia hatua fulani ya ukuaji (uzee) katika maisha yao, hujivua magamba na kuwa vijana tena. Taifa letu limefikia hapo. Huu ni wito kwa watu wote, na hasa viongozi, tuache gamba lijivue kwa njia ya asili. Kinyume na hapo ni kuchunana ngozi tu na kubakia na madonda, majeraha, makovu, na hata vifo.
KWA WATU WA DINI/IMANI
Zimezuka chokochoko za kutosha kwa muda mfupi sana kiasi hatuelewi ni nani yuko nyuma yake. Viongozi wa dini wanaongea hadi mapovu yanawatoka na hakuna wa kukemea. Wanaongea vitisho! Ifike mahali kauli za kutishana zikome. UKRISTO NA UISLAM ni imani zinazobebana. Wala wasijidanganye eti itafika siku tutapigana kisa DINI zetu, haipo! Tutashikana mashati kwa masuala mengine kama siasa na uchumi.
Serikali kama ina mkono wake hapo ijiondoe mara moja, maana inadhalilisha baadhi ya watu wanaotumika kwenye suala hili.
KWA VIONGOZI WA KISIASA
ifike mahali siasa isiwe ndio suala la kufa na kupona. Kuna njia zingine za kuendesha maisha. Siasa isiwafaye mkajiona kuwa walemavu wa fikra, kiasi kwamba bila MAMLAKA yako huwezi kupenya nguvu ya soko. Huwezi kupata tenda. Huwezi negotiations. Huwezi kuwa humble. Mmeifanya siasa kuwa ni chaka la kujilimbikizia mali, na viriba vyenu ni elastic (vinatanuka tu) to infinity - yani havijai na ndio maana mnajilimbikizia tu.
kamba mlizofungwa shingoni hazina ukomo wa urefu. Zinavutika tu kwa kadiri unavyogoea kutafuta malisho, hivyo mnajikuta mnaingia hata kaika maeneo ambayo hamkustahili. Siasa imewafanya muwe kupe na chawa (parasites). Mmekuwa viwavi. Mnakula na kunya papo hapo kuanzia mwanzo wa maisha yenu hadi mwisho wake. Hii yote inawafanya muwe dhaifu sana kimantiki na hodari sana katika "kujitafutia". Hayo yote yamedhihirika kuanzia mwezi wa kumi mwaka huu.
Mmetengeneza uraibu wa kutisha kwenye siasa huku mkihukumu waraibu wengine katika mawanda mengine. Lenu hamlioni. Kuanzia ngazi ya juu kabisa (urais) hadi utendaji wa mitaa imekuwa tatizo. Tusitake kuamini kuwa "bila mimi" mambo hayaendi. Mjifunze kwa waajiriwa pale wanapopewa likizo za mwaka kuwa wanakumbushwa hata wasipokuwepo kazi zitaendelea kufanyika. Igeni mfano huo. Mapengo huzibika. Tena ya kisiasa ndio usiseme. "Mwili" unaandaliwa mochwari na huku kuna mtu anapima suti kwa fundi. Siku ya mazishi anakuja kuhakikisha kuwa umeenda kweli futi sita chini kisha anaenda kugonga cheers na kesho yake anakaimu nafasi yako. Hivyo wanasiasa msijione kuwa mko maalum sana.
Mfano hai ni uteuzi na utenguzi uliofanyika juzi hapa kwenye "baraza la mawaziri". Kuna mtu asubuhi alitoka na walinzi na jioni akarudi na dereva tu. Hii inatupa picha kuwa kazi yenu msiione ni ya kufa na kupona kiasi cha kusigina haki za wengine. Acheni kutoa matamko yenye kuibua chuki na hasira mkidhani mnamfurahisha mtu fulani. Angalieni taifa hili kwa mapana yake (Bara na visiwani).
VYOMBO VYA DOLA
Mnao wajibu mkubwa kwa umma na si kwa mtu mmoja. Viapo vyenu inabidi vitizamwe upya. Teuzi zenu inabidi zitizamwe upya. Mtitizamo yenu inabidi itizamwe upya. Ujasiri wenu inabidi uwe ni kwa maslahi mapana ya umma. Nyie ni RAIA kama wengine. Huwa mnajidanganya kwenye viunga vyenu kuwa sio raia. Sisi ndio mnatuita raia. Hizo dhana pengine zinawafanya muwe na imani kuwa mko juu ya "Raia". raia ni citizens, na citizens ni wananchi ambao ndio hao raia. Kutumika kwenu kwenye vyombo vya dola na kimamlaka haiwafanyi muwe aliens.
Wakuu wa vyombo epukeni kuwatumia walioko chini yenu kutekeleza amri ambazo mbeleni zitakuja kuleta madhara. Msio na vyeo jitahidini sana kutumia busara na hekima pale mnapopokea amri za wakubwa wenu. Najua ni ngumu ila kwa umoja wenu mnaweza kufanya mabadiliko. Polisi ni ndugu zetu. Nina ndugu wa damu ambao ni polisi.. Nina marafiki wazuri ambao ni polisi. Very humble hadi unajiuliza huyu kwenye hii kazi kafuata nini.
Najua wahudumu wa dola huwa mnalishwa upepo kuwa nyie ni watu MAALUM sana. Ni kweli mna umaalum wenu ila hauwaondolei uraia wenu. Usiwaondolee pia utu wenu. Msiewe sifa kwa maslahi ya wachache. Sikilizeni shida za wananchi kwa mapana. Wahalifu kweli wapewe stahili zao na raia wema nao wapate haki zao. Mna jicho na dhana ya kimtazama kila raia kuwa ni mhalifu mtarajiwa. Na mtuhumiwa kama mhalifu kamili. Sisi sote ni watanzania na tunapambania taifa hili toka kona tofauti kwa nia moja.
VYAMA VYA SIASA
Kuna chama kimekuwa madarakani kwa miongo sasa kiasi kwamba imefika hatua kimejimilikisha taifa hili. Kauli ya juzi ya mwenezi kuwa anatoa kauli rasmi kuwa chama kinaisimamia serikali na sio serikali kukisimamia chama sidhani kama ni sahihi. Ni suala la mjadala mpana hapa. La kuzingatia ni kwamba vyama navyo visijiaminishe na visiaminishe umma kuwa bila wao mambo hayaendi. Walijaribu kukaa kando na kuona vile mambo hayaendi? Hakula lisilowezekana. Maadam tumetaka kuwepo nasiasa, basi siasa na iwe ndio msingi wa uongozi bora kama vile HAKI ilivyo msingi wa AMANI.
Ifike wakati vyama vibadilishane uongozi kama watu wenye busara. La muhimu pawe na ILANI YA KITAIFA ambayo haitaangalia chama bali maslahi mapana ya umma. Serikali ndio iwe na mamlaka na sio chama. Hii dhana ya chama kushika hatamu ndio imetufikisha hapa. Serikali ndio kila kitu maana siasa na wanasiasa huja na kupita. Chama kushika hatamu ndio huzaa matamshi ya kibabe yenye mrengo wa kudhuru kila chenye kuleta "upinzani".
Vyama vya siasa vipunguzwe nguvu. Chama kisiwe na mamlaka ya kuisimamia serikali bali serikali ijisimamie, maana katika mihimili ya Dola hakuna chama pale, bali wanachama wa vyama mbalimbali na wasio na vyama pia.
MAANDAMANO
Maandamano imekuwa ni mwiba sana kwa serikali zetu. Wala sio kwa serikali bali mwiba kwa vyama vya siasa ambavyo vinaamini kuwa vina mamlaka ya kutoa amri kwa serikali na serikali ikatii. Chama kibakie kama mzazi ambaye baada ya wakati fulani anakosa mamlaka kamili juu ya yule aliyemzaa. Maandamano ni haki ya kikatiba. Polisi kwa intelijensia zao wahakikishe kuwa maadamano hayo yanafanyika kwa staha na si vingine.
MWISHO
Tunatamani kuona Taifa la wawajibikaji. Raia wawajibikaji, lakini raia wenye dhamana ya uongozi wawajibikaji. Anayevunja amani kwa kauli na matendo apate stahili yake. Anayetumia dhamana kutenda visivyo naye apate stahihi zake.
Mwisho kabisa, ile tume ya maridhiano kama wadau wengi walivyotoa maoni yao, haijakidhi viwango. Ilipaswa kuwa tume ambayo imeundwa na chanzo ambacho hakina maslahi ya moja kwa moja na serikali hii na uteuzi wake. Hatuwezi kupata maridhiano ambayo yataleta ahueni kwa pande zote.
Hatutaki tena kuona umwagikaji damu, hata tone moja kisa madaraka.
Mungu bariki Taifa letu Tanzania 🙏