Wito wa kura ya maamuzi kuhusu marekebisho kwenye katiba: vita vipya vya team Ruto vs Team Raila

Wito wa kura ya maamuzi kuhusu marekebisho kwenye katiba: vita vipya vya team Ruto vs Team Raila

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
Kimewaka na hivi karibuni kitaeleweka. Mgogoro kati ya Naibu rais William Kipchirchir Samoei Arap Ruto na Rt. Honorable Raila Amollo Odinga kuhusu kura ya maamuzi mwakani umeanza kuibua hisia chungu nzima. Hii ni baada ya mswada ulotayarishwa na mbunge wa Ndia George Kariuki kuhusu kura ya maamuzi ya kurekebisha katiba ili County zipunguzwe hadi 12 na maseneta wapunguzwe hadi 24 na baadhi ya marekebisho mengine kwenye bunge. Raila anaunga mkono kura ya maamuzi mwakani kama walivokubaliana na rais Uhuru baada ya ile 'handshake' yao. Naibu rais naye anapinga vikali kura hiyo ya maamuzi, mawazo yenu wakuu. https://www.standardmedia.co.ke/art...rendum-calls-jolt-the-2022-political-equation
 
toka mwanzo ilikuwa inajulikana kuwa mkikuyu ata msinitch mkalenjini. Unyangau bado upo kazini
 
toka mwanzo ilikuwa inajulikana kuwa mkikuyu ata msinitch mkalenjini. Unyangau bado upo kazini
Acha kukurupuka, toa ukabila wako hapa, wabunge karibia wote kutoka Ml. Kenya wanamuunga mkono Naibu rais Ruto kuhusu kura ya maamuzi hiyo. Kaa kando tafadhali uwape nafasi wanaoelewa kinachoendelea wajadili haya masuala bila ya hizi pumba zako za kawaida.
 
Acha kukurupuka, toa ukabila wako hapa, wabunge karibia wote kutoka Ml. Kenya wanamuunga mkono Naibu rais Ruto kuhusu kura ya maoni hiyo. Kaa kando tafadhali uwape nafasi wanaoelewa kinachoendelea wajadili haya masuala bila ya hizi pumba zako za kawaida.
sasa kama anajua hayo yote thtead umefungua ya nini?? Wakikuyu mna msinitch Ruto
 
Hii shida yote imeletwa Na kitu inaitwa JUBILEE.
Kenya tuko hapa juu ya hawa vijana wawili ,bure kabisa.
Nlijua hakuna kitu wanaweza since 2013.
 
sasa kama anajua hayo yote thtead umefungua ya nini?? Wakikuyu mna msinitch Ruto
Hili ni jukwaa la Kenya News and Politics, kama ulitarajia nikuombe ruhusa utangoja sana. Hapa tunaongea kuhusu marekebisho kwenye katiba ya KENYA, ili tupunguze idadi za County, wabunge, maseneta na madiwani. Kama haijakupendeza pita kule.
 
Tatizo hujui hata hasara yakupunguza county.
 
Wakikuyu jamii waliolaaniwa kwa usaliti
 
Hii shida yote imeletwa Na kitu inaitwa JUBILEE.Kenya tuko hapa juu ya hawa vijana wawili ,bure kabisa.Nlijua hakuna kitu wanaweza since 2013.
Jombaa hii ni kuhusu marekebisho kwenye katiba ya 2010, kabla ya Jubilee au UhuRuto kuingia ikulu. Wengi wataingiza siasa za 2022 lakini nadhani hii ndio chance yetu kubwa ya kupunguza County, wabunge, maseneta na madiwani na kupunguza pia gharama ya mishahara yao.
 
Katiba haikua caste on stone kwamba haiwezi kuboreshwa zaidi, ni muhmu sana kuwa na mdahalo wa kitaifa wa kuhusu hili, japo pia musiiweke ikae kama ushindani baina ya Ruto na Raila maana hapo watu wataunga au kupinga kwa misingi ya mahaba yao kwa viongozi badala ya kutumia muda kutafakari.
 
Hili ni jukwaa la Kenya News and Politics, kama ulitarajia nikuombe ruhusa utangoja sana. Hapa tunaongea kuhusu marekebisho kwenye katiba ya KENYA, ili tupunguze idadi za County, wabunge, maseneta na madiwani. Kama haijakupendeza pita kule.
Hivi, kwanini kupunguzwa kwa Counties na Senators inaonekana kama mwiba kwa Ruto? Je, atapoteza nini na Raila atafaidika vipi? Ukinijibu hayo naweza kuuona mwisho wa mgogoro huu...

Hata hivyo, ni bora Counties zipunguzwe ili kubana matumizi maana ni kama walijitengenezea sehemu ya ulaji na kuwapa nafasi jamaa zao...
 
Katiba haikua caste on stone kwamba haiwezi kuboreshwa zaidi, ni muhmu sana kuwa na mdahalo wa kitaifa wa kuhusu hili, japo pia musiiweke ikae kama ushindani baina ya Ruto na Raila maana hapo watu wataunga au kupinga kwa misingi ya mahaba yao kwa viongozi badala ya kutumia muda kutafakari.
Kwa mtazamo wako unadhani unaunga mkono upande upi (bila kujali kama ni shabiki wa Raaila au Ruto), kwa faida na mustakabali wa Kenya?...
 
Kupunguzwa kwa county na maseneta kumeletaje hiyo confrotation ya team raila vs ruto.Enlighten us tusiojua.
Ruto na timu yake wanapinga hili, nadhani kwasababu tu lilikuwa ni wazo la Raila na Uhuru kwa pamoja bila ya kuwajumuisha wao, siunawajua tu wanasiasa? Mimi naunga mkono hoja ya kura hiyo kwasababu nadhani wanalolifanya rais Uhuru na Raila ni kufanikisha mabadiliko mazuri bila kujali kama itavuruga siasa za uchaguzi wa 2022. Ruto keshaanza kulialia, sawa tu na waliokuwa wafuasi wa Raila kwenye NASA. The dynamics are changing fast.
 
Wakikuyu jamii waliolaaniwa kwa usaliti
Usaliti na ukikuyu unahusiana kivipi na mchakato wa kurekebisha katiba kwa manufaa ya taifa letu
tukufu la Kenya. Viongozi wa mlima Kenya tayari wameshagawanyika wenyewe kwa wenyewe wengi wao wakimuunga mkono Ruto. Kwahivyo hata maoni yako ya kikabila hayana msingi wowote ule.
Tatizo hujui hata hasara yakupunguza county.
Hasara ama faida? Akili zako zimetafunwa sio bure.
 
Hivi, kwanini kupunguzwa kwa Counties na Senators inaonekana kama mwiba kwa Ruto? Je, atapoteza nini na Raila atafaidika vipi? Ukinijibu hayo naweza kuuona mwisho wa mgogoro huu...Hata hivyo, ni bora Counties zipunguzwe ili kubana matumizi maana ni kama walijitengenezea sehemu ya ulaji na kuwapa nafasi jamaa zao...
Kweli kabisa Counties zikipunguzwa tutakuwa tumebana matumizi kwa njia kubwa sana. Naibu rais William Ruto na viongozi wanaomuunga mkono wanapinga hayo, sio kwa sababu zozote zile za kimsingi, ni ubabe wa kisiasa tu. Msikize hapa alipokuwa kule Pwani jana akilalamika vikali kuhusu Raila na anavokivuruga chama cha Jubilee.
 
Kwa mtazamo wako unadhani unaunga mkono upande upi (bila kujali kama ni shabiki wa Raaila au Ruto), kwa faida na mustakabali wa Kenya?...

Mtazamo wangu ni kwamba katiba tuliyo nayo ni bora sana, tena nzuri yenye mambo muhimu ambayo yametuwezesha kupiga hatua kijamii na kiuchumi. Lakini hata hivyo, inayo mapungufu ambayo yanahitaji kuangaliwa upya na kujadiliwa kwa mapana na kila Mkenya.
Hivyo bila kuegemea upande wowote wa kisiasa, mimi nashauri mdahalo uwe wa kulijadili hili, tuangalie wapi pa kurekebisha na kama patahitaji kura ya maoni, basi ifanywe tu.
Lakini tukianza misimamo ya vyama au kuendeshwa na mahaba yetu kwa viongozi, basi tutaharibu kitu kizuri. Maana kuna atakayepinga kisa kiongozi wake amepnga, na mwengine ataunga mkono kwa kufuata mkumbo bila kusoma hata kurasa moja.
 
Kimewaka na hivi karibuni kitaeleweka. Mgogoro kati ya Naibu rais William Samoei Kipchirchir Arap Ruto na Rt. Honarable Raila Amollo Odinga kuhusu kura ya maoni mwakani umeanza kuibua hisia chungu nzima. Hii ni baada ya mswada ulotayarishwa na mbunge wa Ndia George Kariuki kuhusu kura ya maoni ya kurekebisha katiba ili County zipunguzwe hadi 12 na maseneta wapunguzwe hadi 24 na baadhi ya marekebisho mengine kwenye bunge. Raila anaunga mkono kura ya maoni mwakani kama walivokubaliana na rais Uhuru baada ya ile 'handshake' yao. Naibu rais naye anapinga vikali kura hiyo ya maoni, mawazo yenu wakuu. Revealed: How referendum calls jolt the 2022 political equation
pingli-nywee uko upande gani? Marekebisho yafanyike au la?
 
MK254, tuwe wakweli, itakuwa vigumu sana kuepuka hizi siasa za kibabe kwenye mchakato wowote kuhusu katiba. Nakumbuka Mwai Kibaki na serikali yake walivobwagwa chini kwenye ile kura ya kwanza ya maamuzi kuhusu katiba mpya. Baadaye kidogo wakaja wakaungana Kibaki, Raila na Uhuru na wakapiga kampeni za kufa mtu na wakenya wakakubali katiba mpya kwa asilimia zaidi ya tisini. Kinachonishangaza ni kwanini William Ruto kila mara huwa yupo upande wa upinzani ikifika ni kwenye masuala ya kikatiba. Ikumbukwe kwamba hata hii katiba tunayoitumia kwa sasa Ruto alikuwa kiongozi wa mrengo ulioipinga vikali. Huu mchakato ni wa kisiasa, kura zitapigwa na kila mwanasiasa anataka aoneshe ushawisi wake kuhusu kura zitakavopigwa. Cha muhimu ni kila mkenya afanye maamuzi yake kibinafsi.
 
Back
Top Bottom