Wito wa mpito kwa DPP: Wakili aliyemwandaa ACP Kingai aondolewe jopo la Mashtaka la akina Mbowe

Wito wa mpito kwa DPP: Wakili aliyemwandaa ACP Kingai aondolewe jopo la Mashtaka la akina Mbowe

Wakili wa Serikali; unayatambuaje Maelezo yako?
Shahidi; nayatambua kwa mwandiko wangu, sahihi ya Adam na sahihi yangu

Ameihakikishia mahakama mbele ya Mtukufu Jaji kwamba yale maelezo ni yake mwenyewe (ACP Kingai; mkamataji)!
yake ndiyo si likuwa anamhoji mtuhumiwa anaandika na mtuhumiwa anasaini kwamba kilichoandikwa ni sawa sasa hapo kosa liko wapi? mbowe anaenda kula mvua za kutosha gaidi mkubwa mbwa huyu
 
Means maelezo Yale aliyatunga mwenyewe from his head or cooked from his head ànd not from the suspect. Do you mean that?
 
yake ndiyo si likuwa anamhoji mtuhumiwa anaandika na mtuhumiwa anasaini kwamba kilichoandikwa ni sawa sasa hapo kosa liko wapi? mbowe anaenda kula mvua za kutosha gaidi mkubwa mbwa huyu
Mbwa maaaaaaàa yako not Mbowe
 
Means maelezo Yale aliyatunga mwenyewe from his head or cooked from his head ànd not from the suspect. Do you mean that?
syo kweli maelezo alitoa mtuhumiwa yakakndikwa na akasaini huyo haruki hapo maelezo yake hayo mtuhumiwa maana alisaini
 
Tuache yote ila hilo la dawa la kulevya ni aibu kubwa; Hivi serikali inawetegemeaje hawa watu wakati wanawavua nguo Hivi kila siku?
... in short apart from ugaidi na uhujumu uchumi walikuwa wamepanga pia kuwabambika dawa za kulevya (kesi nzito nzito za maisha au 30 yrs) ili wakichomoa kwenye shtaka hili wanaswe kwenye shtaka lingine. Nadhani mwandaa script (charge sheet) alikuja kusahau kuingiza dawa za kulevya given the urgency and the prevailing pressure!
 
syo kweli maelezo alitoa mtuhumiwa yakakndikwa na akasaini huyo haruki hapo maelezo yake hayo mtuhumiwa maana alisaini
Soma alivyoulizwa na wakili wa serikali. Wakili framed a wrong question, a misleading one for the anticipated response
 
Jana nilikuwepo Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi. Sikwenda pale kwa minajiri ya kuhudhuria kesi ya akina Mbowe. Nilikwenda kufuatilia mambo ya mwanangu anayesoma pale Law School of Tanzania. Kwakuwa nilimaliza kilichonipeleka mapema na niliwaona hata marafiki zangu wakijumuika kuhudhuria kesi ya akina Mbowe, niliamua kujumuika nao. Ni katika viunga hivyohivyo vya Law School of Tanzania.

Jana, upande wa Mashtaka (Jamhuri) ilianza kuleta mashahidi. Shahidi wa kwanza, na nilishajua na kumtegemea, akawa ni ACP Ramadhani Kingai ambaye kwasasa ni RPC wa Kinondoni. Kama shahidi wa kwanza na wa muhimu wa Jamhuri, Kingai alieleza mengi kwenye kesi ya msingi na hata kwenye kesi ndogo iliyoibuka baada ya mapingamizi yaliyotolewa na upande wa Utetezi uliokuwa ukiongozwa na Wakili Msomi Kibatala.

Katika uga wa kisheria, shahidi yeyote huandaliwa na Wakili anayemleta mahakamani. Kuandaliwa si kufundishwa cha kusema ila ni kuunda mtiririko na mueleweko wa ushahidi wa shahidi husika. Pia, maadalizi hujumuisha upembuzi wa kipi cha kuanza; kipi cha kumalizia; kipi cha kusemwa na kipi cha kutokusema mahakamani kwenye kesi husika. Hata ACP Kingai aliandaliwa na Wakili au Mawakili wa Jopo la Mashtaka.

Kuna mambo ya wazi kabisa ambayo yameleta mkanganyiko badala ya muunganiko kwenye ushahidi wa Kingai. Mkanganyiko usio na tija. Kuhusu mtiririko wa matukio; kilichotokea na kilichofanyika na polisi. Nitatoa mifano michache kwakuwa mambo yenye mkanganyiko yalikuwa mengi mno. Kwanza, Kingai hakutaja kwenye ushahidi wake kuhusu watuhumiwa kufikishwa kituo cha Polisi Mbweni. Aliishia kusema walifikishwa Central Dar. Kwanini hakuandaliwa kuhusu hilo?

Pili, Kingai amesema kuwa watuhumiwa walikutwa na bastola moja na risasi tatu. Ni tofauti na Hati ya Mashtaka inayotaja risasi moja. Tatu, amezungumzia watuhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya. Kwanini hakuandaliwa kuacha kuzungumzia kitu kisicho sehemu ya mashtaka ya akina Mbowe? Nne, Kingai amesema kuwa alipokuwa akiongoza timu ya upelelezi na ukamataji alikuwa Regional Criminal Officer (RCO) wa Arusha. Hakuandaliwa kueleza kwanini alifanyia kazi mikoa ya wengine kwenye ma-RCO na askari wengine?

Au Kingai naye alikuwa Sabaya wa pili? Tena, Kingai ameeleza kuwa kuna mashahidi walichukuliwa maelezo yao Moshi. Hapohapo akasema watuhumiwa walichukuliwa maelezo yao Dar es Salaam kwakuwa ndiko jalada lilipokuwa limefunguliwa. Kwanini wahusika wa jambo moja watofautishwe mahali pa kuchukuliwa maelezo yao? Hapa pia hakuandaliwa vyema. Kingai amefanya kadiri ya uwezo wake kuelezea. Lakini, hakuandaliwa vyema.

Halafu, kama mkamataji hakupaswa kushiriki kwenye kuwachukua maelezo washtakiwa. Hivi Wakili aliyemwandaa hakulijua hata hilo? Maana Kingai amekuwa akirudiarudia mahakamani kuwa aliwachukua maelezo washtakiwa ambao yeye mwenyewe ndiye aliyewakamata. Kufanya hivyo si kuandika stori yake mwenyewe anayetaka wengine waiamini na kumpongeza kwa uandishi wa stori tamu kuwahusu washtakiwa?

DPP Mwakitalu, chukua hatua mapema. Ondoa Wakili au Mawakili waliomuandaa Kingai. Kama Kingai amejikanyaga vile, watakaofuata wataanika madudu mapya na yakutisha zaidi.

Chief Hangaya, nasi tuanze kampeni chamani?

Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam
Mkitaka kutunga uongo ni lazima waongo wote mkusanyike pamoja sehemu moja, hamuwezi kutunga uongo kwa kutumia simu ambazo nazo zimechanganyikiwa kwa uongo wa kila aina na ni kila siku.
Madawa ya kulevya yameingizwa ili kukazia uwezo wa kukata miti kuanzia Dar mpaka Mbeya, kwani bila bangi hauwezi hata kufika Kimara.
 
... in short apart from ugaidi na uhujumu uchumi walikuwa wamepanga pia kuwabambika dawa za kulevya (kesi nzito nzito za maisha au 30 yrs) ili wakichomoa kwenye shtaka hili wanaswe kwenye shtaka lingine. Nadhani mwandaa script (charge sheet) alikuja kusahau kuingiza dawa za kulevya given the urgency and the prevailing pressure!

Unasahauje jaman? Hii nchi ngumu sana
 
Mzee mipango ya dhulma huwa haifanikiwi hata huyo kingai angekesha kusoma makabrasha ya ushahidi angechemka tuu.
 
yake ndiyo si likuwa anamhoji mtuhumiwa anaandika na mtuhumiwa anasaini kwamba kilichoandikwa ni sawa sasa hapo kosa liko wapi? mbowe anaenda kula mvua za kutosha gaidi mkubwa mbwa huyu
Mijadala ya great thinkers nakushauri uwe unasoma tu bila kuchangia kitu. Maana hapo ndipo unapochemka kuuficha ujinga wako....

Yani hata logic ndogo tu kwenye hoja ya jamaa hujaielewa? Kwani shuleni ulienda kusomea ujinga?
 
Back
Top Bottom