GE2025 Wito wa mwisho: Askari Polisi msitolewe kafara… Wekeni Silaha zenu chini

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Mbona naona daliki tena kama huyu mama ataendelea aisee, maana wanaendelea kutangaza matokeo
 
Aliewashauli na kuwapa silaha hawa jama, sijui. Japo wengi wamekufa, ila kuna mama mmoja Tabata kisiwani kapigwa risasi kichwani, mbele ya mtoto wake wa kiume, tena mmoja tu. Mama,alikuwa muuza mkaa(Nasema alikuwa, kwa sababu kutokana na hali ilivyo, sidhani kama kuna uwezekano wa kupata msaada, na lisasi kichwani, bila usafili wala huduma).


Hawa vijana wanaouliwa ndugu na wazazi, mnadhani watareact vipi? Kikubwa tu busara itumike.
 
Hapana,Ubungo hapa sahiz mabomu ya machozi yanaunguruma hatari
Aaah, kumbe bado vimwananchi viko barabarani? Duh kwa kweli vimeamua! Poti wangu Mr. Njaa yuko wapi na kujikomba kwake kwa mazeri?
 
Angalau Gen-Z wa Dar wamewaheshimisha wanaume wa Dar. Sasa hivi sitarajii tena zile kauli za wanaume wa Dar wanakimbizwa na Panya Road!
 
Yaani sioni namna gani na katika ulimwengu gani wanawarudisha Watanzania majumbani maishayaendelee
 
Yaani sioni namna gani na katika ulimwengu gani wanawarudisha Watanzania majumbani maishayaendelee
Kutatokea machafuko kila siku, nchi haitatawalika. Kuweza kutawala itabidi waifanye Tanzania kama Korea ya Magharibi, Police state. Ila kwa Tanzania ilivyo haitawezekana.

Kwahiyo wanaweza kusogeza mbele kidogo anguko lao kwa siku, wiki, miezi kadhaa. Lakini 100% anguko lao linakuja hivi karibuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…