Wito: Watanzania Tuwasaidie Wakenya

Wito: Watanzania Tuwasaidie Wakenya

Hivi misaada ambayo serikali yenu iliwomba mumefikisha ngapi, maana nawajua kwa ubahili wenu mtakausha sana, labda Wahindi na Waarabu ndio watatoa hiyo misaada.
Mtani, serikali yetu tunaijua inaomba msaada just kujazilizia.ila ikiwa siku kuna uhitaji mkubwa wa haja, lazima kila mwananchi atajitoa kwa chochote.

Kwa hiyo mtani ni kusema hutaki chakula chetu ama?
 
Chakula chenu tukikihitaji tutaagiza maana mahela tunayo ya kumwaga, kwa sasa tumekomaa kwenye kupima maelfu ya watu kwa siku ili turudi kwenye hali ya kawaida ikiwemo kuwarejesha watoto shuleni, hivi mbona mumeshindwa kupima watu mpaka kunao Watanzania wanatuibukia huku kila tukiwapima wanakutwa na Corona, ina maana huko mnaogelea kwa kirusi, sema tu kwa neema ya Mungu mpo mpo tu siku zinaenda.
Naona hata Zanzibar mumewapelekea kirusi kwa fujo.
 
Moyoni unaipenda Tz

Sent using Jamii Forums mobile app

Naipenda Afrika, kwanza vitoto vya hili bara vyote vina msambwada, hamna bara nyingine utapata utamu wa nyama choma kwa ugali na wanawake wenye maumbo ya kupendeza kama humu, hivyo hamna taifa ninalochukia Afrika, labda sema nachukia tu tabia ya baadhi ya Waafrika, unakuta kwa mfano Watanzania ni wanafiki kwa kiwango cha lami, anakuamkia shikamoo, muda wote anakuita mkuu, ila ukigeuza kidogo tu atakusema vibaya kwa kila atakayemskliza.
Kwetu hapa, mtu akiwa na tatizo na wewe, anakuambia papo hapo bila kuremba.
 
Waache ubishi kwanza...

Ni kama vile Bhakresa alivyojitolea chakula nchini Rwanda...

Cc: mahondaw
 
Naipenda Afrika, kwanza vitoto vya hili bara vyote vina msambwada, hamna bara nyingine utapata utamu wa nyama choma kwa ugali na wanawake wenye maumbo ya kupendeza kama humu, hivyo hamna taifa ninalochukia Afrika, labda sema nachukia tu tabia ya baadhi ya Waafrika, unakuta kwa mfano Watanzania ni wanafiki kwa kiwango cha lami, anakuamkia shikamoo, muda wote anakuita mkuu, ila ukigeuza kidogo tu atakusema vibaya kwa kila atakayemskliza.
Kwetu hapa, mtu akiwa na tatizo na wewe, anakuambia papo hapo bila kuremba.
Unaipenda sana Tz bhana wewe fara, wacha porojo mob.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaipenda sana Tz bhana wewe fara, wacha porojo mob.

Sent using Jamii Forums mobile app

Yeah! Kupandishana mizuka na nyie humu JF hunisaidia kudumisha uandishi wa Kiswahili, maana kwa kweli hapa Kenya huwa hatuandikiani kwa Kiswahili kabisa, hehehe!! Hivyo huwa nasaka hoja ya kuwatibua ili mtiririke kama nzige, na kama kawaida huwa hamkawii, subiri nitinge kwenye jukwaa lenu la siasa nikatafute hoja ya kuileta huku.
 
Wakenya hamuandikiani kiswahili sababu majority yenu ni brainwashed.
Mnaishia kuandikiana sheng na english, sheng for diminishing swahili, english for looking down on swahili.
Whilst if your leaders joined hands, swahili would be stronger than it is now.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakenya hamuandikiani kiswahili sababu majority yenu ni brainwashed.
Mnaishia kuandikiana sheng na english, sheng for diminishing swahili, english for looking down on swahili.
Whilst if your leaders joined hands, swahili would be stronger than it is now.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuandikiana kwa Kiswahili ni mtihani maana chenyewe bado sana kwenye mambo mengi, ni kizuri tu kwenye kutupiana umbea lakini ukihitaji kukitumia kikazi huwa balaa.
Hata Tanzania nimeishi na kuona kinavyowapa tabu wataalam ofisini, unakuta email wanaandikiana kwa kingereza, hata reports zote inabidi ziandaliwe kwa kingereza.
Nilikua napata tabu sana, report nimeandaa kwa kingereza, inasomeka freshi halafu naambiwa lazima itafsiriwe, naingia gharama za kuhakikisha nakala ya kiswahili, tatizo unakuta hakuna anayejishughulisha kuisoma.
 
Back
Top Bottom