Wivu ni ugonjwa, na wahusika ni watu wakaribu siku zote

Wivu ni ugonjwa, na wahusika ni watu wakaribu siku zote

Mayor Quimby

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2021
Posts
4,950
Reaction score
10,977
Kindetawili

Tega:

Mayor Quimby ana roho mbaya sana.

Waulize sasa watu wanao mjua huyo Mayor..

Katika watu 100 ukibahatisha mmoja ndio anamajua huyo Mayor na anatakwabia yupo tofauti na anavyoongelewa.

Wakati huo huo utakutana na watu 1000 ambao awajawahi kumuona ila wanajua mafanikio yake.

Hao watu 1000 kutokana na habari za wengine watakwambia Max ni mtu mmbaya kutokana na hadithi za watu wengine.

Sasa unaweza shindanisha utetezi wa mtu mmoja anae mjua max na watu 1000 wasiomjua Mayor kwa kusikia na wanaosema mtu ni mtu wa ovyo kwa kusikia tu.

Sijapata kuona watanzania wana wivu aisee na chuki.

Lengo la mada ni kwa wewe msomaji kama una tabia za chuki na wivu jitazame.
 
Hii mada aiwezi pata mchango

Ukweli huwa unauma ndio tabia za watanzania

Yaani wivu, watu awajiamini

Ubora wake au amani yake ni kumtukana mwingine.

Kama sio JF basi mtaani

Yaani watanzania tuna wivu mpaka mtu unajiuliza vipi.

Hiki kitu ni cha kukaa na kujiuliza wengi wetu; tatizo ni nini.
 
Kasheshe sasa ilipo kuna siku bwana Mayor anaweza jitokea zake kwenda bar kujipumzikia kutoa stress zake.

Kufika bar anakutana na mmoja ya wale watu 1000 asiowajua wenye chuki nae kwa hadithi za third party; halafu pimbi anamletea fujo.

Hao ndio baadhi ya watanzania; unabaki unajiuliza mjomba kabla sijakupasulia chupa ya kichwa mbona atujuani.

Kuna baadhi ya watanzania wana matatizo kwakweli ambayo mie nimekosa majibu; labda wenzetu mnayaelewa.
 
Tatizo waTanzania sasahivi tumelala bia na nyama choma raha tu. Wewe kibwengo wa nchi gani usie lala?.🤣
Nipo kwangu Iringa (Ipogolo) nawaza tu.

Ni kwanini kuna watu wanawafuata watu wasio wajua; na wakifika moja kwa moja wanawachukulia poa kwa hadithi walizo okota kwengine.

Niamini kama umewahi kuishi na watu nchi zingine ni watanzania tu ndio wenye hizi tabia za kuwavaa watu kwa hadithi za wengine (to be specific wengi wao ni watu wa kutoka familia duni).

Kwanini hili kundi la hawa watu duni wanadhani wana uhalali wakuwafuata watu wasio wajua na wahusika wanatakiwa kuongea nao.

Ni kama ulaya kuna ndugu zangu waliopo kwa miaka mingi wanashangaa na wao kuna watanzanis waliofika huko ambao hawana miaka 15 na zaidi wana hizo tabia.

Watu wanabaki vipi unamvaa mtu usiemjua au kutambulishwa kwake rasmi na mtu mwingine wa karibu yake.

Yaani watanzania wanaweza mvaa tu mtu wasiemjua from no where; halafu wanachukulia poa. Hakuna jamii nyingine yoyote ipo hivyo, ata kwa bongo huo sio utaratibu wa mitaa ye kishuani popote ndani ya mikoa ya Tanzania.

We vipi, wengine wao ulaya unakuta wamesukuma vikete; sitaki kusema washikaji zangu wa kijamaika na kibongo uhuni.

Unajiuliza wabongo vipi mbona wanavaa watu wasio wajua kama wana wajua.
 
Aisee! imekuaje tena Meku?
Kuna shida mahala kwenye jamii yetu na atutaki mjadala wa kuongelea sababu zake.

Lakini wivu ni tatizo kwenye jamii yetu.

Sasa unategemea uonewe wivu walau na watu mnaojuana.

Kwa watanzania unawezakutana na jealousy za ovyo ukijuliza huyu nae katokea wapi, jamaa humjui, amgombei nafasi ya kazi, ujawahi zuia maendeleo yake; lakini rijitu lina chuki tu na wewe.

Haya ni kwa mtaani tu wala sio kuhusu watu maarufu. Watanzania mitaani tuna matatizo ya wivu ya kupindukia kuanzia ndani ya familia zetu na ndugu wa tumbo moja achilia mbali watu baki.

Tuna matatizo gani lazima tuulizane huo ndio ukweli yaani ata ndugu mnachekeana unafiki mkifika umri wa kutafuta maisha kwa familia nyingi sana. Huo ndio ukweli wetu,

Ndio najiuliza kwanini tupo ivyo
 
Napenda sana mchezo wa "draft", hivyo naenda katika vijiwe ambako mchezo huo unachezwa. Ukitaka uongee vizuri na watu wa hapo, yakupasa usiongee mambo ambayo yataashiria umestarabika; ongea mambo yanayoashiria kuwa wewe ni mtu wa hovyo hovyo tu, hapo watafurahi na kuwa rafiki yao. Lakini wakigundua kuwa wewe ni mtu makini, watakuchukia mno na kukutenga. Yote hii inatokana na chuki na wivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Nashangaa waliofurahi Dkt. Dorothy Gwajima kuondolewa Wizara ya Afya
 
Tatizo waTanzania sasahivi tumelala bia na nyama choma raha tu. Wewe kibwengo wa nchi gani usie lala?.🤣
Ukiamka nahitaji kujulishwa kwanini watu wa mbali wapigane kuona usongi mbele.

Wanafaidika vipi na kukwama.

Hii topic tusiikwepe wivu upo na aukwepeki. Tunashindana na marafiki kufanikiwa (bila ya kuzuiana), class mates na hata ndugu.

Lakini kwanini wewe badala ya kushindana kwa mafanikio, unakubali kushindwa. Baada ya hapo unaanza majungu.

Na chanzo cha majungu ni watu wa karibu sawa, shida zaidi ni rijitu usilolijua na lenyewe kuwa na ugomvi na wewe.

We vipi mjomba
 
Napenda sana mchezo wa "draft", hivyo naenda katika vijiwe ambako mchezo huo unachezwa. Ukitaka uongee vizuri na watu wa hapo, yakupasa usiongee mambo ambayo yataashiria umestarabika; ongea mambo yanayoashiria kuwa wewe ni mtu wa hovyo hovyo tu, hapo watafurahi na kuwa rafiki yao. Lakini wakigundua kuwa wewe ni mtu makini, watakuchukia mno na kukutenga. Yote hii inatokana na chuki na wivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakini tunaishi kwenye hii jamii.

Mwanzo nilidhani ni familia yetu tu ni yenye shida, mpaka nilipo nisikia story za wengine.

Sasa ndugu shida kwa baadhi ya familia nyingi, maisha yenyewe nayo yanataka mbinu; halafu unakutana na jitu nalo from no where linakuanzishia from nowhere unabaki unajiuliza we vipi kulikoni.

Hayo matatizo yake si awepelekee ndugu zake
 

Nashangaa waliofurahi Dkt. Dorothy Gwajima kuondolewa Wizara ya Afya
Hii siyo mada ya Dorothy Gwajima tujadili maisha yetu ya kila siku watanzania.

Usitake kusema wewe huna ndugu ambae mafanikio yanamkera.

Kama ndugu awatoshi ujakutana na mijitu mtaani ambayo huijui kabisa imenuna tu kwa mafanikio yako mpaka ukajiuliza huyu nae vipi. Sasa shida zake we umechangia vipi.
 
Napenda sana mchezo wa "draft", hivyo naenda katika vijiwe ambako mchezo huo unachezwa. Ukitaka uongee vizuri na watu wa hapo, yakupasa usiongee mambo ambayo yataashiria umestarabika; ongea mambo yanayoashiria kuwa wewe ni mtu wa hovyo hovyo tu, hapo watafurahi na kuwa rafiki yao. Lakini wakigundua kuwa wewe ni mtu makini, watakuchukia mno na kukutenga. Yote hii inatokana na chuki na wivu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu mimi naua sana Kingi na vijiwe vya draft huwa naenda hasa napokua Home Tanzania ila kijiwe chetu njoo na hoja zako zilizoshiba hatukutengi ila zile hoja za hovyo unachanywa Live..inshort napenda draft kwa kuwa jamaa mnakua huru kutaniana huku mkicheza bila kujali Elimu,Kipato unakuta mchimba chumvi anamtania mtu mwenye cheo cha Kaptein jeshini na anajua huyo angetaniwa wapi..Mzee Zerote Steven alipokua RPC mbeya alikua anakuja kuua Kingi ili mambo yake ya kikazi yawe marahisi na alifanikiwa..
 
Sisi Watanzania tuna chuki ya asili Wazee unakuta mtu hataki maendeleo ya mtu mwingine na wanatamani maendeleo wasikie kapata wasiemjua kuliko wanaemfahamu unakuta jamaa limejitengenezea sumu mwilini kisa kuchukia watu hata wasiomhusu...hawapendi kuishi kwa kufanya yao tuu na wakiwa na shida wanamfata tena awasaidie hapo wakiambiwa subiri hata siku mbili ni majungu mwanzo mwisho kama vile waliweka bank...
 
Kwa sababu, Watanzania wengi ni Masikini.
Na umasikini Kwa sehemu ndio huleta hayo yote uliyoyataja.

Masikini wa kiuchumi
Masikini wa akili na maarifa (hawa ndio balaa zaidi)
Masikini wa kiroho.

Yaani kumkuta Mtanzania asiyekosa moja Kati ya hayo ni 1/100
 
Wivu kwa sasa ni tatizo kubwa sana kwenye jamii zetu !! Na utashangaa hata aliyekuzidi nae ni full wivu tuu !!!
Kwakweli inashangaza, mie naamini aliekuzidi akiwa na wivu ameona alipo woga wake anadhani pengine ungepata nafasi alizopata kwa kukufahamu ungemzidi.

Tatizo zaidi ni wivu watu wasio kujua ujawahi ata kuongea nao (wala sio watu wanasiasa unaowakejeli kule kwenye jukwaa la siasa) kwanza ni mawaziri so kuwapa vipande vyao ni wajibu wetu.

Ila huku mtaani tunapo angaika na kupata mkate wetu, kwanini mie niumie na mtu kama Jerry Slaa kwa mfano wakati simjui na wala sababu zilizomfikisha halipo.

Sasa unakuta kuna rijitu alikujui eti lina vita na wewe ndio najiuliza we vipi, mzima kweli.
 
Kwa kweli naomba michango zaidi ya wadau, kuelewa ushuhuda wao nijifunze.

Binafsi nina mshikaji ambae sisi ni washindani (aniwezi eniwei mie ndio nilie mfunza ujanja kabla ya yeye kuamia kwenye biashara ambazo sizo kwangu) ila zina hela.

Pamoja na hayo ushindani wetu ahukuwahi koma kwa wanaotujua tulipotoka walituacha kwa wasiotujua kwa kuangalia biashara ipi ina hela wakaona kama vile kuna wivu kwa upande wangu. Bila ya kufahamu pamoja na siasa zetu huyo mtu awezi kuona na kwema akakubali alikadhalika vita yetu tunaijua wenyewe.

Kilicho nishangaza mimi ni baadhi ya ndugu zangu kuchukua propaganda za adui yangu ni kuniponda mimi bila ya kufahamu huyo mtu mimi nammudu tukikutana wenyewe na ugomvi wetu tunaujuwa wenyewe.

Sasa ndio nikajua kumbe adui zaidi anaweza kuwa mtu wa ndani kushinda wa nje.

Story ni ndefu

Please share you are experience na wewe nani unadhani ana wivu na wewe na unatushauri vipi katiba experience yako kwenda mbele.
 
Back
Top Bottom