Wivu ni ugonjwa, na wahusika ni watu wakaribu siku zote

Wivu ni ugonjwa, na wahusika ni watu wakaribu siku zote

Mimi sio mtu wa kujichanganya nina mshikaji mwingine ninae share nae updates na anawauzia washikaji ambao nishawatema.

Sijali kwa sababu mimi na yeye tumeshibana ikifika mahala mjomba hapa na zama awezi kuniacha wala mimi siwezi kumuacha so nimeamua kumchukulia kama mtu mmbea tu.

What is your experience ongeeni tujifunze hayo ni mambo ya maisha na wengine tujifunze.
 
Kwa sababu, Watanzania wengi ni Masikini.
Na umasikini Kwa sehemu ndio huleta hayo yote uliyoyataja.

Masikini wa kiuchumi
Masikini wa akili na maarifa (hawa ndio balaa zaidi)
Masikini wa kiroho.

Yaani kumkuta Mtanzania asiyekosa moja Kati ya hayo ni 1/100
Inasikitisha zaidi watu awataki kutoa changamoto zao za makazini, majirani zao au za kifamilia.

Ni mazingira ambayo na wengine wajifunze kuishi nayo au walichomoka vipi.

Hayo mambo kwenye jamii zetu ayakwepeki.
 
Mkuu mimi naua sana Kingi na vijiwe vya draft huwa naenda hasa napokua Home Tanzania ila kijiwe chetu njoo na hoja zako zilizoshiba hatukutengi ila zile hoja za hovyo unachanywa Live..inshort napenda draft kwa kuwa jamaa mnakua huru kutaniana huku mkicheza bila kujali Elimu,Kipato unakuta mchimba chumvi anamtania mtu mwenye cheo cha Kaptein jeshini na anajua huyo angetaniwa wapi..Mzee Zerote Steven alipokua RPC mbeya alikua anakuja kuua Kingi ili mambo yake ya kikazi yawe marahisi na alifanikiwa..
Ni kweli mkuu nakubaliana na wewe, vipo vijiwe ambako watu wanataniana na kufurahia. Hawa roho zao ni tajiri; wapo watu hawapendi kuona au kusikia mtu fulani anafanikiwa kwa nyanja yoyote ile. Mkuu nakupa hongera kwa kijiwe chako kuwa na watu wastaarabu bila kujali utofauti wa elimu, kazi, au cheo. Na mimi pia ni mtaalam sana wa kuuwa (kunyonga) king, lakini nimekatishwa tamaa, na hivi tunavyoongea nina kipindi nimeacha kwenda kijiweni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani Mimi wivu na chuki haviniumizi kichwa kabisa ninachojua hawatoweza kuharibu kusudi la Mungu kwenye maisha yangu na mwisho hawazuii Mimi kupata Hela, watajijua atiiiiii
 
Hao ndio wengi hata password ya kazi au biashara hawatoi ili wanaokula Keki wawe wachache...
Mimi pia password ya biashara Sijui bure Labda nikuuzie ...

Biashara ushindani/Maisha ushindani Na ukitusua kivyako sikumind Wala nini...

Kama wewe mwanangu nitakupa ...ila kama siyo...

Usifananishe wanangu na wanao ...
 
Kwa kweli naomba michango zaidi ya wadau, kuelewa ushuhuda wao nijifunze.

Binafsi nina mshikaji ambae sisi ni washindani (aniwezi eniwei mie ndio nilie mfunza ujanja kabla ya yeye kuamia kwenye biashara ambazo sizo kwangu) ila zina hela.

Pamoja na hayo ushindani wetu ahukuwahi koma kwa wanaotujua tulipotoka walituacha kwa wasiotujua kwa kuangalia biashara ipi ina hela wakaona kama vile kuna wivu kwa upande wangu. Bila ya kufahamu pamoja na siasa zetu huyo mtu awezi kuona na kwema akakubali alikadhalika vita yetu tunaijua wenyewe.

Kilicho nishangaza mimi ni baadhi ya ndugu zangu kuchukua propaganda za adui yangu ni kuniponda mimi bila ya kufahamu huyo mtu mimi nammudu tukikutana wenyewe na ugomvi wetu tunaujuwa wenyewe.

Sasa ndio nikajua kumbe adui zaidi anaweza kuwa mtu wa ndani kushinda wa nje.

Story ni ndefu

Please share you are experience na wewe nani unadhani ana wivu na wewe na unatushauri vipi katiba experience yako kwenda mbele.
Ni afadhali hizo chuki na wivu wakufanyie watu wa mbali kuliko kufanyiwa na ndugu. Wivu kutoka kwa ndugu unaumiza zaidi. Halafu kwa kuwa uko naye, anaweza kukufanyia vitendo hivyo bila wewe mwenyewe kugundua. Unakuja kugundua, tayari mambo yameharibika.

Wivu wa ndugu huchangia hata kuharibu maisha ya mwingine moja kwa moja, kwakuwa ni vigumu kumgundua, unaweza kumwamini kumbe mwenzako moyoni mwake anawaza mengine.

Kuna wakati wazazi huwaamini watoto wao wakubwa na kuwataka wawasaidie wadogo zao. Sasa utakuta dogo yuko very bright, halafu mkubwa wake hakukujaliwa hilo. Sasa huyu mkubwa anaanza kuhisi huyu dogo huko mbele atakuja kuwa machachari, kwa hiyo nimkandamizie hukuhuku chini.

Hapo mkubwa atafanya hira yoyote ile ambapo dogo ataonekana kakosea. Mkubwa atalibebea bango hilo jambo na kuonekana hufai mbele ya jamii na kuwaambia watu amekushindwa, kumbe yote hayo kasababisha yeye.

Nadhani wanajamii forum wengi humu ni watu wazima; tuwe waangalifu sana na wazaliwa wetu wa kwanza, hasa katika suala la itelligence, ikitokea ana jealousy, na mdogo wake yuko vizuri, usimwamini kwa wadogo zake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia password ya biashara Sijui bure Labda nikuuzie ...

Biashara ushindani/Maisha ushindani Na ukitusua kivyako sikumind Wala nini...

Kama wewe mwanangu nitakupa ...ila kama siyo...

Usifananishe wanangu na wanao ...
Sawa sawa mkuu swala hapo unagawa wapo wasiotoa hata kwa hela..
 
Ni kweli mkuu nakubaliana na wewe, vipo vijiwe ambako watu wanataniana na kufurahia. Hawa roho zao ni tajiri; wapo watu hawapendi kuona au kusikia mtu fulani anafanikiwa kwa nyanja yoyote ile. Mkuu nakupa hongera kwa kijiwe chako kuwa na watu wastaarabu bila kujali utofauti wa elimu, kazi, au cheo. Na mimi pia ni mtaalam sana wa kuuwa (kunyonga) king, lakini nimekatishwa tamaa, na hivi tunavyoongea nina kipindi nimeacha kwenda kijiweni.

Sent using Jamii Forums mobile app
Upo mkoa gani mkuu
 
Nipo kwangu Iringa (Ipogolo) nawaza tu.

Ni kwanini kuna watu wanawafuata watu wasio wajua; na wakifika moja kwa moja wanawachukulia poa kwa hadithi walizo okota kwengine.

Niamini kama umewahi kuishi na watu nchi zingine ni watanzania tu ndio wenye hizi tabia za kuwavaa watu kwa hadithi za wengine (to be specific wengi wao ni watu wa kutoka familia duni).

Kwanini hili kundi la hawa watu duni wanadhani wana uhalali wakuwafuata watu wasio wajua na wahusika wanatakiwa kuongea nao.

Ni kama ulaya kuna ndugu zangu waliopo kwa miaka mingi wanashangaa na wao kuna watanzanis waliofika huko ambao hawana miaka 15 na zaidi wana hizo tabia.

Watu wanabaki vipi unamvaa mtu usiemjua au kutambulishwa kwake rasmi na mtu mwingine wa karibu yake.

Yaani watanzania wanaweza mvaa tu mtu wasiemjua from no where; halafu wanachukulia poa. Hakuna jamii nyingine yoyote ipo hivyo, ata kwa bongo huo sio utaratibu wa mitaa ye kishuani popote ndani ya mikoa ya Tanzania.

We vipi, wengine wao ulaya unakuta wamesukuma vikete; sitaki kusema washikaji zangu wa kijamaika na kibongo uhuni.

Unajiuliza wabongo vipi mbona wanavaa watu wasio wajua kama wana wajua.
Mkuu hata mimi huwa nashangaa sana! Hasa sisi hohahe wanga tunamatatizo sàna.

Ila kinachotakiwa usijiweke wazi kwa watu
 
Hii siyo mada ya Dorothy Gwajima tujadili maisha yetu ya kila siku watanzania.

Usitake kusema wewe huna ndugu ambae mafanikio yanamkera.

Kama ndugu awatoshi ujakutana na mijitu mtaani ambayo huijui kabisa imenuna tu kwa mafanikio yako mpaka ukajiuliza huyu nae vipi. Sasa shida zake we umechangia vipi.
OK OK sawa
 
Kindetawili

Tega:

Mayor Quimby ana roho mbaya sana.

Waulize sasa watu wanao mjua huyo Mayor..

Katika watu 100 ukibahatisha mmoja ndio anamajua huyo Mayor na anatakwabia yupo tofauti na anavyoongelewa.

Wakati huo huo utakutana na watu 1000 ambao awajawahi kumuona ila wanajua mafanikio yake.

Hao watu 1000 kutokana na habari za wengine watakwambia Max ni mtu mmbaya kutokana na hadithi za watu wengine.

Sasa unaweza shindanisha utetezi wa mtu mmoja anae mjua max na watu 1000 wasiomjua Mayor kwa kusikia na wanaosema mtu ni mtu wa ovyo kwa kusikia tu.

Sijapata kuona watanzania wana wivu aisee na chuki.

Lengo la mada ni kwa wewe msomaji kama una tabia za chuki na wivu jitazame.
Usiwaponde, wasaidie especially unapokuwa una exposure ya maisha mengine kama vile kuishi nje ya nchi. Udhaifu mkubwa walionao diaspora ni kwamba huwa wanakuwa na tendency ya kuwaponda waTanzania badala ya kuwasaida
 
Back
Top Bottom