Wivu ni ugonjwa, na wahusika ni watu wakaribu siku zote

Mimi sio mtu wa kujichanganya nina mshikaji mwingine ninae share nae updates na anawauzia washikaji ambao nishawatema.

Sijali kwa sababu mimi na yeye tumeshibana ikifika mahala mjomba hapa na zama awezi kuniacha wala mimi siwezi kumuacha so nimeamua kumchukulia kama mtu mmbea tu.

What is your experience ongeeni tujifunze hayo ni mambo ya maisha na wengine tujifunze.
 
Inasikitisha zaidi watu awataki kutoa changamoto zao za makazini, majirani zao au za kifamilia.

Ni mazingira ambayo na wengine wajifunze kuishi nayo au walichomoka vipi.

Hayo mambo kwenye jamii zetu ayakwepeki.
 
Ni kweli mkuu nakubaliana na wewe, vipo vijiwe ambako watu wanataniana na kufurahia. Hawa roho zao ni tajiri; wapo watu hawapendi kuona au kusikia mtu fulani anafanikiwa kwa nyanja yoyote ile. Mkuu nakupa hongera kwa kijiwe chako kuwa na watu wastaarabu bila kujali utofauti wa elimu, kazi, au cheo. Na mimi pia ni mtaalam sana wa kuuwa (kunyonga) king, lakini nimekatishwa tamaa, na hivi tunavyoongea nina kipindi nimeacha kwenda kijiweni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani Mimi wivu na chuki haviniumizi kichwa kabisa ninachojua hawatoweza kuharibu kusudi la Mungu kwenye maisha yangu na mwisho hawazuii Mimi kupata Hela, watajijua atiiiiii
 
Hao ndio wengi hata password ya kazi au biashara hawatoi ili wanaokula Keki wawe wachache...
Mimi pia password ya biashara Sijui bure Labda nikuuzie ...

Biashara ushindani/Maisha ushindani Na ukitusua kivyako sikumind Wala nini...

Kama wewe mwanangu nitakupa ...ila kama siyo...

Usifananishe wanangu na wanao ...
 
Ni afadhali hizo chuki na wivu wakufanyie watu wa mbali kuliko kufanyiwa na ndugu. Wivu kutoka kwa ndugu unaumiza zaidi. Halafu kwa kuwa uko naye, anaweza kukufanyia vitendo hivyo bila wewe mwenyewe kugundua. Unakuja kugundua, tayari mambo yameharibika.

Wivu wa ndugu huchangia hata kuharibu maisha ya mwingine moja kwa moja, kwakuwa ni vigumu kumgundua, unaweza kumwamini kumbe mwenzako moyoni mwake anawaza mengine.

Kuna wakati wazazi huwaamini watoto wao wakubwa na kuwataka wawasaidie wadogo zao. Sasa utakuta dogo yuko very bright, halafu mkubwa wake hakukujaliwa hilo. Sasa huyu mkubwa anaanza kuhisi huyu dogo huko mbele atakuja kuwa machachari, kwa hiyo nimkandamizie hukuhuku chini.

Hapo mkubwa atafanya hira yoyote ile ambapo dogo ataonekana kakosea. Mkubwa atalibebea bango hilo jambo na kuonekana hufai mbele ya jamii na kuwaambia watu amekushindwa, kumbe yote hayo kasababisha yeye.

Nadhani wanajamii forum wengi humu ni watu wazima; tuwe waangalifu sana na wazaliwa wetu wa kwanza, hasa katika suala la itelligence, ikitokea ana jealousy, na mdogo wake yuko vizuri, usimwamini kwa wadogo zake!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi pia password ya biashara Sijui bure Labda nikuuzie ...

Biashara ushindani/Maisha ushindani Na ukitusua kivyako sikumind Wala nini...

Kama wewe mwanangu nitakupa ...ila kama siyo...

Usifananishe wanangu na wanao ...
Sawa sawa mkuu swala hapo unagawa wapo wasiotoa hata kwa hela..
 
Upo mkoa gani mkuu
 
Mkuu hata mimi huwa nashangaa sana! Hasa sisi hohahe wanga tunamatatizo sàna.

Ila kinachotakiwa usijiweke wazi kwa watu
 
OK OK sawa
 
Usiwaponde, wasaidie especially unapokuwa una exposure ya maisha mengine kama vile kuishi nje ya nchi. Udhaifu mkubwa walionao diaspora ni kwamba huwa wanakuwa na tendency ya kuwaponda waTanzania badala ya kuwasaida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…