Lady Whistledown
JF-Expert Member
- Aug 2, 2021
- 1,147
- 2,008
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Butusyo Mwambelo amesema Mkoa huo unamatatizo yanayosabishwa na Migogoro ya Kimapenzi na Ardhi
Kaimu kamanda ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa huduma za msaada wa kisheria mkoani hapa inayotolewa na kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC. "Njombe hii kuna matatizo. Matatizo ni mengi sana sijawahi ona nimefanya kazi Iringa,nimefanya Rukwa nimefanya Mbeya lakini Njombe watu wanauana wanandugu.
Jeshi la polisi tunashida, tunaokota miili ya watu na ukifuatilia wanauana kwa sababu ya matatizo ya ardhi,wanagombaniana mipaka, kaka anamuua mdogo wake,kaka anamuua kaka yake kwa sababu ya urithi ndugu zangu mtusaidie"amesema Mwambelo.
Ameongeza kuwa"Si wanawake wala wanaume,wanawake wajane wanapata shida wananyanyasika sisi hapa tunadawati la jinsia na watoto,kuna wanaume wananyanyasika na wake zao wanateseka wanashindwa wakimbilie wapi,kuna wanawake wananyanyasika na wanaume zao,tatizo ni kwamba wengi wanauana kwa wivu wa kimapenzi wanaacha watoto wananyanyasika nawaombeni wanasheria mtusaidie"amesema.
Pia Mwambelo ameomba LHRC kiweka kituo mkoani hapa ili kusaidiana na jeshi la polisi ili amani iweze kitawala.
Kwa upande wa matibu tawala mkoa wa Njombe Judica Omari kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka, ametumia fursa hiyo kuwaomba wananachi wa Njombe kujitokeza kuwasilisha malalamiko yao.
Naye mkurugenzi wa uchechemuzi na maboresho LHRC wakili Fulgence Massawe,amesema jumla ya migogoro 210,000 imeshughulikiwa ikiwa migogoro ya ardhi 75,000,mashauri ya ajira na kazi 63,000,mirathi 44,100 na matunzo ya watoto maswala ya ndoa 27,300 imeshughulikiwa.
"Katika kipindi cha kuadhimisha miaka 27 LHRC imeweza kuwafikia jumla ya watu 540,000 ikiwa wanawake 216,000 na wanaume 324,000"amesema Massawe.
Chanzo: Nipashe