Wivu wa Wassira kwa Warioba hadi kwenye Katiba Mpya. Wapinzani hatumaanishi Katiba ni mali ya Mzee Warioba

WanaCCM wana matatizo sana, Mzee Wasira akihojiwa TBC amesema haya...

''Wapinzani wanasema wanataka katiba ya Warioba, Warioba hana katiba, kazi yake ilikuwa ni kukusanya maoni na sheria ya mabadiliko ya katiba ya wakati ule inasema baada ya maoni kukusanywa yanafikishwa katika Bunge maalum na ndio litakaloandika katiba pendekezwa''

Mzee Wasira ana Chuki Binafsi mbona kuna Mapendekezo ya Nyalali mbona kuna Tume ya Jaji Kisanga?

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Nashukuru...lakini hao wapinzani huwa hawasemi 'katiba ya Warioba' husema 'katiba iliyopendekezwa na tume ya Warioba', sasa ndugu Muuza Kangala...amemnukuu Mzee Wassira akisema 'hakuna katiba ya Warioba' ni mzee yuko sahihi kama kuna mtu anasema kuna katiba ya Warioba
Kwa kuwa siyo mtihani wa lugha yuko sahihi. Ni lugha za mitaani!
 
Wanapoyaita madaraja majina au stendi za mabasi unakuta ni yao? Logically hii katiba itaitwa kwa "nickname" ya warioba maana yeye pamoja na wahusika wengine ndio wamesimamia utekelezaji wake.
 
WanaCCM wana matatizo sana, Mzee Wasira akihojiwa TBC amesema haya...

''Wapinzani wanasema wanataka katiba ya Warioba, Warioba hana katiba, kazi yake ilikuwa ni kukusanya maoni na sheria ya mabadiliko ya katiba ya wakati ule inasema baada ya maoni kukusanywa yanafikishwa katika Bunge maalum na ndio litakaloandika katiba pendekezwa''

Wasira anataka waite Katiba ya Wasira
 
WanaCCM wana matatizo sana, Mzee Wasira akihojiwa TBC amesema haya...

''Wapinzani wanasema wanataka katiba ya Warioba, Warioba hana katiba, kazi yake ilikuwa ni kukusanya maoni na sheria ya mabadiliko ya katiba ya wakati ule inasema baada ya maoni kukusanywa yanafikishwa katika Bunge maalum na ndio litakaloandika katiba pendekezwa''

WASSIRA anatamani SANA tena SANA VYEO hivi
1.Urais
2.Uwaziri Mkuu
3.Katibu Mkuu ccm
4.SPIKA
5.Basi hata UBUNGE
 
Huyu mzee wa Gombe asituzengue ,kwani tukisema Tume ya Nyalali au Bunge la Sitta au Makinda kwani wao ndio wamiliki?
 
Back
Top Bottom