Kwenye mapenzi: Wivu kati ya wawili ndani ya mahusiano unaweza kua kirutubisho au chachu ya mapenzi.Ukionyesha kwa kiasi utamfanya mwenzi wako ahisi kwamba unampenda na kumjali...sisemi kwamba ni kitu pekee kinachofanya hivyo bali ni kichocheo kizuri iwapo hakitazidishwa na kusababisha kero.Wivu unapozidi unaonyesha mapungufu yako kanakwamba hujiamini kitu ambacho kinaweza kupelekea mwenzako nae ahisi kwamba HUMUAMINI.
Dear Lizzy, kwa kadiri nilivyoifahamu hii mada, kuna wivu wa aina mbili - wivu mzuri na wivu mbaya. Wivu mzuri ni ule unaokusukuma kufikia hatua aliyofikia mwenzako, mbaya ni ule wa husuda na chuki ambao matokeo yake mwenye wivu huwacha kujiendeleza na kubakia kuumia roho, kupika fitina na kumwaga majungu.
Lakini bado siuelewi huu wivu wa mapenzi/kwa mpenzi wako. Ni nini hasa? Kuuliza uliza "umeenda wapi?", "kwa nini umechelewa kurudi?", ulikuwa unazungumza na nani?", kutaka kujua ameenda wapi na nani", "kupekua mikoba na mifuko ya suruali", "kusoma sms na msgs kwnye simu na internet", "Sitaki uzungumze, uwe na urafiki na fulani" n.k. Ikiwa ni moja, baadhi au yote katika haya hatuoni kuwa ni kero? Ni aina gani ya matendo ya wivu "mzuri" baina ya wapenzi ambayo yatazidisha mapenzi badala ya kuwa kero?