Wivu!!

Wivu!!

Huwezi amini, pamoja na maelezo yoooooooooooote hayo, mi nimepapenda zaidi hapo kwenye red.

:focus:
Ila sometimes kuridhika nako kunasaidia kuondokana na wivu usio wa lazima.
Hehehe kisa cha kupenda nyekundu?!?

Back to topic..nakubaliana na wewe.Mara nyingi wivu hua unasababisha na kutoridhishwa na mambo binafsi..kitu ambacho ni kizuri kwasababu kinaweza kumfanya mtu ajitahidi kuongeza juhudi kwenye mambo yake
 
Sijui nina wivu ngoja nikajicheki kwenye kioo vizuri leo.
Jiangalie ukiwa unamfikiria mtu ambae unadhani ana zaidi yako...ukikunja ndita bila kukusudia au ukibinua midomo BADILIKA!
 
ukiona una kama vinywele nywele juu ya macho yako yote mawili ujue hiyo ni dalili ya wivu.
Ahaaa ahaaa wewe Hus huo ni utabiri kutoka wapi mara hii umeishakuwa Sheikh Yahya au ulienda Loliondo kama alivyosema DC.
 
Dah! Mi niliwahi kushikwa na wivu mkali nilipokuwa O level, kuna dogo huyo A zote alikuwa anapata yeye. Hata kutuachia na wenzie!
Advance tukachaguliwa tena shule moja, uzuri yeye alichagua kombi tofauti na yangu. Nilishukuru kweli maana dogo alizidi!!!
Miakili kama kachanjiwa....Hahaha!

Pole sana. Kuna jamaa tulikuwa naye O-level, yeye alikuwa ni mkali saaana ila alikuwa hataki kutufundisha. Tulimkalia tukamtukana hadi akabadilika. Tulimweleza kuwa yeye akipata A na mimi nikapata F hawezi kufaidi lolote. Ila akitumia nguvu kidogo wakati anafanya mazoezi yake ya kawaida akatusaidia kupata B itakuwa bora kwetu na hatapungukiwa kitu. Huwezi kuamini, timu yetu sote tulifaulu vizuri.

Ila watu wengi huwa tunafikiria kwamba tukiwasaidia wenzetu basi tunapoteza. Ni upuuzi wa hali ya juu. Kama mtu ameumbwa kukupita basi atakupita tu, hata kama hutamsaidia!
 
  • Thanks
Reactions: CPU
Jiangalie ukiwa unamfikiria mtu ambae unadhani ana zaidi yako...ukikunja ndita bila kukusudia au ukibinua midomo BADILIKA!
Weee Lizzy wewe ngoja nifanye hilo zoezi leo kesho nitakupa majibu
 
Pole sana. Kuna jamaa tulikuwa naye O-level, yeye alikuwa ni mkali saaana ila alikuwa hataki kutufundisha. Tulimkalia tukamtukana hadi akabadilika. Tulimweleza kuwa yeye akipata A na mimi nikapata F hawezi kufaidi lolote. Ila akitumia nguvu kidogo wakati anafanya mazoezi yake ya kawaida akatusaidia kupata B itakuwa bora kwetu na hatapungukiwa kitu. Huwezi kuamini, timu yetu sote tulifaulu vizuri.

Ila watu wengi huwa tunafikiria kwamba tukiwasaidia wenzetu basi tunapoteza. Ni upuuzi wa hali ya juu. Kama mtu ameumbwa kukupita basi atakupita tu, hata kama hutamsaidia!

huyo dogo pia alikuwa mchoyo wa matirio. Lol!
Halafu halikuwa hawezi kufundisha mtu hata kama kitu anakiweza vipi. Anaweza akakuelekeza kitu usimwelewe hata kidogo ila mwingine unamwelewa.
 
Ahaaa ahaaa wewe Hus huo ni utabiri kutoka wapi mara hii umeishakuwa Sheikh Yahya au ulienda Loliondo kama alivyosema DC.

nimeoteshwa na mwalimu wangu wa chuo. Mwambie babu DC naye asiwe na wasiwasi na utabiri wangu. Nafanya mpango nipate venyu nitoe haka kahuduma.
 
Mhhh,

Mwaka huu serikali yenu itapumua. Watoa huduma mkiwa wengi maana yake hata watu wa kulalamika hawatakuwepo!!

DC
 
huyo dogo pia alikuwa mchoyo wa matirio. Lol!
Halafu halikuwa hawezi kufundisha mtu hata kama kitu anakiweza vipi. Anaweza akakuelekeza kitu usimwelewe hata kidogo ila mwingine unamwelewa.
Hiyo ni kwasababu sio kila mtu ana kipaji cha kufundisha!
 
Lizzy,

Kuna wengine alikuwa anakudanganya na kukupa majibu yasiyo sahihi makusudi. Yaani kukusaidia hataki ila sasa anaamua kukufelisha!
 
Hahahaha!Si bora akatae tu?Ila hiyo ni roho ngumu kupitiliza!Mi ilikua mtu akiniomba nimueleweshe hesabu nafanya ubaoni maana wenyewe wananiomba ili kila ambae hakuelewa hilo swali afaidike.Hata kama ningetaka kuwadanganya ningeishia kutolewa nishai maana anaejua angenirekebisha/kosoa!
 
Hehehe niambie kwanini ili nikwambie kama unaruhusiwa kuendelea au uache haraka!
Yule mshikaji mtaa wa pili pale anapenda sana kuja kushinda kwenu sasa sielewi intentions zake ni nini
 
Back
Top Bottom