Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,891
Imefika mahali hebu tuende kinyume kidogo na mazoea au namna jamii inavyotuambia namna ya kuyatazama mambo,kuna hii hisia inaitwa Wivu,imesababisha madhara sana jamii kama kujiua,kuwa wendawazimu n.k,Kwanza wivu ni nini?Tafsiri halisi ni nini?Watu hudai kama "unampenda" mtu lazima uwe na wivu nae,kama ni kinyume chake humpendi,Hivi kuna uhusiano kati ya upendo na wivu?Kama upo ni upi?Ni mbaya au mzuri?Kama ni mzuri kwanini unaleta madhara?Najiuliza haya kwa sababu sijawahi ona uzuri wa wivu,naona madhara tu,hebu tujiulize na tutoke kwenye mazoea!