Wivu!!!!

Wivu!!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,891
Imefika mahali hebu tuende kinyume kidogo na mazoea au namna jamii inavyotuambia namna ya kuyatazama mambo,kuna hii hisia inaitwa Wivu,imesababisha madhara sana jamii kama kujiua,kuwa wendawazimu n.k,Kwanza wivu ni nini?Tafsiri halisi ni nini?Watu hudai kama "unampenda" mtu lazima uwe na wivu nae,kama ni kinyume chake humpendi,Hivi kuna uhusiano kati ya upendo na wivu?Kama upo ni upi?Ni mbaya au mzuri?Kama ni mzuri kwanini unaleta madhara?Najiuliza haya kwa sababu sijawahi ona uzuri wa wivu,naona madhara tu,hebu tujiulize na tutoke kwenye mazoea!
 
Neno wivu nahisi kama lina maana nyingi, kwa mfano:- Kuna jamaa yangu ana mahusiano ya kimapenzi na Bint mzuri sana wa miaka16, majuzi nilimkarisha nikamuonya kwamba kutembea na watoto wadogo siyo vizuri kwani anawaharibia fyucha yao maana bado uwezo wao ni mdogo sana wa kuhimili changamoto za kimapenzi wakati huohuo kupambana na masomo na pili nilimtahadharisha kwamba inaweza kumletea matatizo makubwa ya Kisheria pindi akikamatwa redihended. Kuna namna alinipuuza na kunisema kwa washkaji kwamba nina "wivu".
 
wivu..........ukizidi unakuwa kero! yeah wivu kidogo lazima katika mapenzi!
 
Mbona hamfafanui maana ya wivu?Au hakuna anaejua!
 
Wivu by definition, ni hali ya kutokuwa na furaha au kukasirika kwa kuona mtu mwingine ana kitu fulani au yupo na mtu fulani ambaye wewe ungependa kuwa naye na unahofu kwamba huyo mtu aliyenaye anaweza akampata moja kwa moja na wewe kumkosa kabisa.

Wivu in nutshel ni chachu katika mapenzi. Haiwezekani uwe na mpenzi wako halafu usimuonee wivu hata kidogo. Kinachotakiwa ni kuwa na wivu wa kiasi, usipitilize na mara nyingine kufanya situational analysis kabla ya kufanya maamuzi.
 
Horse Power,kwa namna ulivyoainisha WIVU hauna mahusiano na kupenda coz accordin to you ni hali ya kutokujiamini na kama hujiamini ni tatizo kuwa na kama ni tatizo halipaswi kuwa na mahusiano na upendo kwani upendo hauchangamani na matatizo!
 
JICHO LA 3,hiyo ndo tafsiri?
 
kama we eiyer huwa nakuonea wivu kweli kabla hata sijajiunga natamani nikuite baba wa watoto wangu hahaha sababu huwa unaandika sense
 
Imefika mahali hebu tuende kinyume kidogo na mazoea au namna jamii inavyotuambia namna ya kuyatazama mambo,kuna hii hisia inaitwa Wivu,imesababisha madhara sana jamii kama kujiua,kuwa wendawazimu n.k,Kwanza wivu ni nini?Tafsiri halisi ni nini?Watu hudai kama "unampenda" mtu lazima uwe na wivu nae,kama ni kinyume chake humpendi,Hivi kuna uhusiano kati ya upendo na wivu?Kama upo ni upi?Ni mbaya au mzuri?Kama ni mzuri kwanini unaleta madhara?Najiuliza haya kwa sababu sijawahi ona uzuri wa wivu,naona madhara tu,hebu tujiulize na tutoke kwenye mazoea!
leo eiyer upo nondo maana mmi pia sijawahi kuwaza na kupata jibu la mahusiano ya upendo na wivu, nashkuru kwa kunipa mawazo kidogo.
 
Yah, wivu una uhusiano wa moja kwa moja na upendo kaka! Kitu ukikipenda unataka kiwe chako tu wala hutamani mwingine akimiliki, ndio maana sisi wapendwa tunaambiwa na maandiko yetu matakatifu kuwa, MUNGU NI PENDO, afu tena MUNGU WETU NI MWENYE WIVU, kwamba hataki pendo lake ukashee na miungu mingine.
Kwa kutokea hapo nafunga kwa kusema kama huna wivu kwa unaempenda basi humpendi, na binadamu wote tulioumbwa kwa mfano wa Mungu ni tuna WIVU.
 
dah........!!!!!
 
Nadhani uhusiano upo kati ya wivu na kupenda ila cha kujiuliza ni uhusiano gani??? huwezi kumuonea wivu dada yako ila mpenzi wako; upo hapo.
Ukiangalia kwa huu mtazamo utajua kuna connection kati ya wivu na kupenda ila how can you describe it?

Lakini inabidi uzingatie kuwa wivu si sawa na upendo ila una uhusiano na kupenda. Yani vyote vina "co exist" ila si "same thing".

Horse Power,kwa namna ulivyoainisha WIVU hauna mahusiano na kupenda coz accordin to you ni hali ya kutokujiamini na kama hujiamini ni tatizo kuwa na kama ni tatizo halipaswi kuwa na mahusiano na upendo kwani upendo hauchangamani na matatizo!
 
Wivu nm 1. hali au tabia ya mtu kusononeka au kukasirika muda mtu amwonapompenzi au rafiki yake ana uhusiano wa mapenzi na mtu mwengine. 2. ngoa, kijicho, chonda, gere. [Kamusi ya Kiswahili Sanifu].
3. [nyongeza yangu] Wivu mwema: Kutamani kile alicho nacho mwenzako na ukafanya juhudi ya kupata kama kile bila ya kuonesha chuki wala husuda kwa aliyenacho.
Kwa maana hizo hapo juu, rafiki yako anadhani una wivu wa maana ya 1.
 
Back
Top Bottom