JICHO LA 3,hiyo ndo tafsiri?
leo eiyer upo nondo maana mmi pia sijawahi kuwaza na kupata jibu la mahusiano ya upendo na wivu, nashkuru kwa kunipa mawazo kidogo.Imefika mahali hebu tuende kinyume kidogo na mazoea au namna jamii inavyotuambia namna ya kuyatazama mambo,kuna hii hisia inaitwa Wivu,imesababisha madhara sana jamii kama kujiua,kuwa wendawazimu n.k,Kwanza wivu ni nini?Tafsiri halisi ni nini?Watu hudai kama "unampenda" mtu lazima uwe na wivu nae,kama ni kinyume chake humpendi,Hivi kuna uhusiano kati ya upendo na wivu?Kama upo ni upi?Ni mbaya au mzuri?Kama ni mzuri kwanini unaleta madhara?Najiuliza haya kwa sababu sijawahi ona uzuri wa wivu,naona madhara tu,hebu tujiulize na tutoke kwenye mazoea!
leo eiyer upo nondo maana mmi pia sijawahi kuwaza na kupata jibu la mahusiano ya upendo na wivu, nashkuru kwa kunipa mawazo kidogo.
Yah, wivu una uhusiano wa moja kwa moja na upendo kaka! Kitu ukikipenda unataka kiwe chako tu wala hutamani mwingine akimiliki, ndio maana sisi wapendwa tunaambiwa na maandiko yetu matakatifu kuwa, MUNGU NI PENDO, afu tena MUNGU WETU NI MWENYE WIVU, kwamba hataki pendo lake ukashee na miungu mingine.
Kwa kutokea hapo nafunga kwa kusema kama huna wivu kwa unaempenda basi humpendi, na binadamu wote tulioumbwa kwa mfano wa Mungu ni tuna WIVU.
Horse Power,kwa namna ulivyoainisha WIVU hauna mahusiano na kupenda coz accordin to you ni hali ya kutokujiamini na kama hujiamini ni tatizo kuwa na kama ni tatizo halipaswi kuwa na mahusiano na upendo kwani upendo hauchangamani na matatizo!