Tanzania kweli bado. Yaani mambo ya muhimu kama haya ya kupata mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya Juu wenye vigezo badala kupewa kipaumbele kwa kutenga fungu kubwa zaidi, ikiwa ni hata kwa kuomba msaada wafadhili kutoka nje wawasaidie, serikali wao wanaelekeza nguvu yao katika mambo mengine yasiyo hata na tija kubwa kwa taifa., mfano.safari za mheshimiwa nje ya nchi akisindikizwa na timu yake ya watu wapatao 60 hivi.
Sina hakika mpaka sasa safari zake za nje zimefikia ngapi na zimegharimu kiasi gani cha mapesa ya walipakodi. Kama mtakumbuka vizuri gazeti la M.wa.na.ha.li.si miaka minne iliyopita lilishawahi kuanika uozo huu.
Kwa kukumbushia kidogo,Kwa viwango vya serikali, watu wanaosafiri kwenye msafara wa rais hulipwa kiasi cha kati ya dola 350 na 500 (Sh. 600,000 kwa siku). Sasa zidisha mara jumla ya idadi yao: halafu zidisha na siku wanazokaa huko nje: gharama za hoteli na usafiri:na jumla ya safari zote: HAKIKA UTACHOKA.