Bado hakuna amsha amsha za kutosha kuhamasisha watu wachanjwe South Africa wamechanja 34% wakati TZ hata 1% ya waliochanja haifiki.Wizara ya Afya imesema hivi karibuni kumekuwa na tishio la kutokea Wimbi la Nne kutokana na taarifa za ongezeko la visa vipya na kuwepo kwa wasafiri wengi ndani na nje ya Nchi katika kipindi cha sikukuu za mwisho wa mwaka
Kutokana na kuibuka aina mpya ya Kirusi cha Corona kiitwacho Omicron, kinachosemekana kuwa na uwezo wa kusambaa haraka, Serikali imesisitiza Wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjo
Pia, imehimiza uvaaji barakoa, unawaji mikono kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vipukusi, kufanya mazoezi na kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima
Hii ina maana madhara ya hiki kirusi kipya yatakuwa makubwa TZ kuliko SA sababu waliochanjwa wachache sana.
TZ kuanzia mwezi January mpaka March 2022 tutaona madhara makubwa ya hiki kirusi kipya ambacho ni hatari kuliko Delta.
Chanjo zipo za kutosha wizara husika haifanyi efforts kubwa kuhamasisha watu wachanje mnamwachia Mama sio sawa kabisa.