A
Anonymous
Guest
Lalamiko langu linahusu Wizara ya Afya kuhusu ukosefu wa mrejesho kwa waombaji waliofanikiwa kupata nafasi ya kushiriki Kongamano la CPHIA litakalofanyika nchini Ethiopia mwezi Novemba.
Wizara ilitoa tangazo la fursa hiyo na kueleza kuwa waombaji watakaofanikiwa kuchaguliwa watagharamiwa na wizara. Hata hivyo, hadi sasa, wengi wa waliochaguliwa hawajapata taarifa kuhusu hatua zinazofuata, ikiwemo maandalizi ya safari na utaratibu wa kugharamiwa.
Kwa upande wangu, nimefanikiwa kupata nafasi ya kushiriki, ambapo waandaaji wa CPHIA wameniondolea ada ya usajili (registration fee) na kunitumia barua rasmi ya mwaliko (invitation letter). Hata hivyo, bado hatujapata maelekezo kutoka Wizara ya Afya kuhusu hatua zinazofuata.
Kwa kuwa zimesalia siku chache kabla ya kongamano hilo kuanza, tunaomba Wizara ya Afya itoe ufafanuzi na mrejesho wa haraka kuhusu hatma ya washiriki waliochaguliwa na utaratibu wa kugharamia ushiriki wao, kama ilivyoelezwa kwenye tangazo la awali.