Lavan Island
JF-Expert Member
- Oct 24, 2015
- 2,377
- 2,048
Punguzeni na gharama za vipimo haiwezekani kipimo kiwe dola mia wakati nchi zote kwa wasafiri ni bure.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Samia na serikali yake naona wanazichezea ndevu za Corona. Udhibiti wa mipaka yetu ni sifuri, tutapukutika kama majani ya mti wa kiangazi. Leo taarifa ya kuja chanjo, jana ilikuwa taarifa ya kuanza ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza chanjo. Mitaa mijini imegeuzwa magulio, umati wa watu ni mkubwa sana na serikali inashangilia.SERIKALI imetangaza kuwa tayari mchakato wa kuingiza na kutoa chanjo ya ugonjwa COVID-19 (Corona) umekamilika huku ikisisitiza tahadhari zaidi ziendelee kuchukuliwa na wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo Julai 4,2021 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Profesa Abel Makubi kwenye mkutano wake na wandishi wa habari ambapo amesisitiza kuwa chanjo hiyo ni hiari.
Prof. Makubi amesema Serikali itatoa chanjo hiyo bure bila kuwatoza wananchi huku akionya kuwa hawataruhusu uingizwaji holela wa chanjo hiyo au kutoza fedha kwa ajili ya kuchoma chanjo hiyo.
Amesisitiza ofisi zote za serikalini nchini wananchi wanaoenda wakiwemo watumishi na kuzingatia taratibu zote za kitabibu za kujikinga na ugonjwa huo ikiwemo kuvaa barakoa kabla ya kuingia kwenye Ofisi hizo pamoja na kuwepo kwa maji tiririka kwa ajili ya kunawa mikono.
" Tunatoa ushauri kwa Ofisi zote za Umma nchini kuzingatia taratibu za kujikinga na Corona kwa kuweka vifaa vya maji tiririka ili kila mwananchi anaeingia aweze kunawa mikono lakini pia tunasisitiza uvaaji wa Barakoa," Amesema Prof Makubi.
Aidha Prof. Makubi amesema miongozo na utaratibu huo ufuatwe pia mashuleni kwa kuhakikisha kunakua na Maji tiririka na uvaaji wa barakoa