Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Wizara ya Afya Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri

Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe [email protected]

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
swali vipimo vya malaria katika hosp za serikali havifanyi kazi au nimekutana na changamoto hiii naambiwa sina malaria nina blood infection, mpaka nilipojikuta ICU hosp fulani nikakutwa na malaria 4147 nipo tayari kushirikianq nanyi tuokoe wengi
 
Je ni kweli kwamba kwa sasa huduma za kwa watoto chini ya miaka mitano sio bure tena?
 
Nimeenda JKCI kuomba nipewe dawa zangu za mwezi ingawa haujatimia tangu nipewe sababu nilipata ajali zikatumbukia mtoni
Wamekataa na kuniambia niandike barua kwa Mkurugenzi ******* ambaye muda wote yupo kwenye makongamano nk hakuwepo na hakuna msaada ingawa NHIF nimelipia 1300000- kwa mwaka
Bure kabisa
 
Je ni kweli kwamba kwa sasa huduma za kwa watoto chini ya miaka mitano sio bure tena?
Ni bure kiongozi, na wazee kuazia miaka 65 ni bure ingawa hapa inaangalia na appearance yako kama kweli ni maskin au laa ☺️☺️
 
Nimeenda JKCI kuomba nipewe dawa zangu za mwezi ingawa haujatimia tangu nipewe sababu nilipata ajali zikatumbukia mtoni
Wamekataa na kuniambia niandike barua kwa Mkurugenzi ******* ambaye muda wote yupo kwenye makongamano nk hakuwepo na hakuna msaada ingawa NHIF nimelipia 1300000- kwa mwaka
Bure kabisa
Hapa walikuwa sahihi tu mkuu, maana ulitaka uwadondoshee jumba bovu.
 
Inakuwaje hospitaali binafsi zinakuwa na dawa ila Kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati zenu mbona hakuna dawa wakati wananchi wanalipa kodi?

Dawa pekee ambayo uhakika ni paracetamol tu shida nini?
Oyaa toka hapo sebuleni kwa shemeji yako uliponing'iniza poumbou uende ukajishughulishe.
 
Wizara Kwa wengi, wanaomba hii gharama ya elfu kumi(10,000/)Kumuona daktari,ifutwe Maana mtu anaumwa Tena hana uhakika wa gharama zingine Bado nauli,madawa,vipimo nk.
Hiyo ni kama kodi ya kichwa kimtindo kwa hospital za Serikali ndio maana Bima zao zinakua na changamoto kubwa wamerundika Tozo nyingi nyingi tu..ukienda Hospital za rufaa ndio utashangaa hizo Tozo kama unatibiwa nje ya Nchi..
 
Ndugu wana JamiiForums,

Tunashukuru kwa maoni yenu na Ushauri mnaotupa kila siku. Kupitia thread hii, tutapokea maoni, Ushauri, na malalamiko yenu. Tunawahakikishia kuwa tutachukua hatua stahiki kwa haraka zaidi.

Unaweza kututumia pia Private Message(PM) na utajibiwa kwa haraka sana.

Fuatilia ukurusa rasmi wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazeena Watoto (Idara Kuu Afya) wa Jamii Forums (Wizara ya Afya Tanzania) kupatea habari mbalimbali kuhusu Sekta ya Afya Nchini Tanzania.

Tufuatilie pia kwenye mitandao yetu ya:

Instagram @wizara_afyatz
Twitter @wizara_afyatz
Facebook “Ministry of Health, Gender, Elderly & Children”

Website www.moh.go.tz
Official Blog www.afyablog.moh.go.tz
Barua pepe [email protected]

Anuani
S.L.P 743 Dodoma
Tanzania

#TunaboreshaSektayaAfya

View attachment 1588107
USHAURI:
Wizara iendelee kusisitiza watu wenye mighahawa, hotels na restaurants kupima afya, kukagua wanaponunua vyakula, wanapopika na hata sahani wanazowekea vyakula , pasi kushahu maji wanao oshea kama yanatirirka na mghahawa LAZMA uwe na choo.

MSIZINGATIE HILI: -
Wizara isiweke vikwazo wka ammalishe wanaopika chakula Buza na kuweka kwenye ndoo za plastiki walizookota viwanda vya rangi, wasifuatilie sponji na sabuni za kusuhuzia sahani, wasifuatilie hao wakinamama wanao uza vyakula juu ya kinyesi fresh kinachotiririka Kariakoo, waache mnaana ni wanyonge.
 
Labda lishaongelewa vile sijasoma maoni yote...

Je mna mipango gani ya kuwa na viwanda vya madawa nchini mwetu ili gharama ya madawa ipungue?
Naamini, kama tunavoona ongezeko la madaktari bingwa (HEKO KWENU), BASI lazma tuna watafiti na wanasayansi tosha kututengenezea madawa, mfano ya mti muarobaini nk

Je mulimuendeleza yule profesa wa UDSM alotutengenezea dawa ya corona wakati imeanza 2011? nilizitumia Dzm, na zilikuwa nzuri kutibu na kukinga
 
Back
Top Bottom